Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

kama hilo litakua suluhisho la matatizo yetu yote kama watanzania na iondolewe. lakini madhara yake yanaweza kua makubwa sana kuliko faida.
Ndiyo maana nikasema jambo linaweza likawa la umuhimu lakini lisiwe la kipaumbele kwa wakati uliyopo,ila ndiyo watu waanangali jinsi gani ya kuikomoa ccm na serikali yake.
 
Kama ni hivyo haya mapambano yake hayawezi kuwa endelevu, akimaliza muda wake ataondoka nayo! It shall have been some effort to futility!
Mkuu jamaa walivyokuwa wanaimba wimbo wao wa ccm ni ileile we ulidhani wanatania?
 
Waheshimiwa wabunge wetu wenye uzalendo wa kweli na nchi hii, nawashauri hivi.

Katika bunge hili la bajeti anzisheni hoja ya kumwondolea kinga rais wetu mpendwa mstaafu JK. Sio hilo tu bali pia kukifuta kabisa kipengele hicho kwenye katiba ili marais wote wastaafu tangu Mwinyi Mkapa na Kikwete waweze kusaidia katika mapambano haya ya kuwabana wote waliotufikisha hapa.

Tujenge utamaduni mpya wa kutokuwa na Miungu watu katika nchi. Hili jambo limekuwa linawafanya marais waliopita kuwa na kiburi cha kufanya lolote kwa sababu tu wanajua wana kinga ya kutoshitakiwa kwa lolote.

Tumekuwa tukimsikia Rais Pombe Magufuli akilaumu sana watumishi wa umma chini ys utawala iliopita kwa kuifanya nchi hii shamba la bibi. Ni wazi kwamba Magufuli anajua vizuri kuwa tatizo si watumishi bali ilikuwa ni uongozi ulioruhusu watumishi kujifanyia watakavyo.

Hata hivyo pamoja na rais Magu kulijua hilo hawezi kufanya lolote kwani katiba imemfunga mikono. Ndio maana nawasihi wabunge wamfungue mikono Mh rais kwa kuwaondolea kinga hawa wastasfu ili yeyote atakayedhika kiti hiki hata huko mbeleni ajue hawezi kufanya atakavyo.

Ukawa hasa muichangamkie hii hoja. Hata km ccm wataipiga chini mtakuwa mmeacha kumbukumbu sahihi.

Haiwezekani rais kila siku alalame kwamba hii nchi imekuwa inafanyiwa mambo ya hovyo kwelikweli halafu eti wasitokee watu wa kumsaidia rais kuwahoji hawa viongozi walioifanya hii nchi ikafiks pabaya kiasi hicho!

Kazi kwenu wabunge. Ondoeni kinga ya rais kutoshitakiwa!
 
Sheria ile ilikuwa nzuri kwa viongozi waadilifu ili kama alikuwa ametoa maagizo ya kumuumiza mtu au kikundi Fulani kwa manufaa ya nchi asijepata usumbufu baadae au kupata woga katika maamuzi yake.
Bahati mbaya wakaingia wengine wabinafsi na kuitumia vibaya kings hiyo kwa manufaa yao na wapambe wao badala ya taifa. Ni wakati sasa wa kuifuta na kubaki na kings ya jambo la kitaifa tuu, lakini akitenda kibinafsi ashughulikiwe kama Mtanzania yeyote, maana sasa imeanza kuwa kinga mpaka kwa wake na watoto wao
 
Hakika kinga kwa rais kutoshitakiwa inatumika vibaya. Kumbuka ya Homeshopping centre_? Sasa Lugumi, ya Kiwira pia. Na taasisi huko ikulu km kins WAMA na Fursa sawa kwa wote EOTF kumbe vilikuwa vichaka vya kupigia dili!
 
Nilichojifunza ni kuwa hii mada huwa haina wachangaji wengi na sababu ni huenda watu wameshalisema sana jambo hili mpaka wamechoka au hatulipi uzito au tumelogwa!
 
Hivi chadema pale ufipa wanalipa kodi kwa shilingi ya kitanzania au dola ya kimarekani?
 
hili ccm hawawezi kukubali,mtu msafi hawezi ogopa hili.Ndio maana mkwere siku ya usafi alisema mnapiga kelele tu,mimi nishamaliza muda wangu najipumzikia na wala sigombei tena.
 

Kauli ya mwanahabari nguli nchini, Jenerali Ulimwengu kutaka Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ashtakiwe mahakamani kwa kuitia hasara Serikali imeibua mjadala mzito, huku wasomi wakisema ipo haja ya kubadili Katiba ili mkuu wa nchi aweze kushtakiwa baada ya kuondoka madarakani.

Wasomi hao walisema ile kauli ya “hakuna aliye juu ya sheria” inapaswa kufuatwa na watu wote, wakitolea mfano Rais wa Brazil, Dilma Roussef aliyeng’olewa na Bunge baada ya kutuhumiwa kukiuka sheria za usimamizi wa akaunti ya bajeti ya nchi hiyo.

Kwa sasa nafasi yake inashikiliwa na aliyekuwa makamu wake, Michel Temer.

Hata hivyo, baadhi ya wasomi wamesema jukumu hilo la kumshtaki rais mstaafu inafaa liachwe mikononi mwa Bunge.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa kinga rais mstaafu ya kushtakiwa kwa jambo lolote alilofanya alipokuwa madarakani na imetoa mlolongo mrefu rais aliyeko madarakani kuondolewa.

Juzi wakati akizungumza katika Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Jenerali ambaye pia ni mwanasheria wa kujitegemea alisema Kikwete anapaswa kushtakiwa kwa kuisababishia hasara Serikali kutokana na kuruhusu mabilioni ya shilingi kutumika katika mchakato wa Katiba ambayo haikupatikana.

Mbali na fedha zilizotumiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa kukusanya maoni, kununulia magari, kulipia pango la ofisi, nyingine zilitumika kurekebisha ukumbi wa Bunge uweze kubeba wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na kulipa posho ya Sh300,000 kwa siku kwa wajumbe 620 kwa muda wa siku 130.

“Itabidi (Kigoda cha Mwalimu) mumuite (Kikwete) mwaka ujao, aje aeleze fedha za wananchi zilizotumika katika mchakato ule zilikuwa na sababu gani,” alisema huku akishangiliwa na umati wa watu.

Jenerali aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya za Hai na Ilala na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, alisema kama mawaziri wa zamani wamepandishwa kizimbani kwa kusababisha hasara, hata Kikwete anapaswa kupelekwa mahakamani kwa kusababisha hasara kwa Serikali na kuzima matumaini ya wananchi, jambo linaloweza kusababisha machafuko nchini.

Ibara ya 46 sehemu ya (1) ya Katiba inasema wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.

Sehemu ya (3) inasema isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A (10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.

Ibara ya 46A sehemu ya (1) inasema bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

Sehemu ya (2) imeweka masharti kwamba bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais; (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; (b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20 (2) ya Katiba.

Mbali ya Katiba ya sasa kumwekea kinga Rais mstaafu, Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba na Katiba Inayopendekezwa zilinakiri kipengele hicho kinachompa Rais mstaafu kinga ya kutoshtakiwa bila kubadili chochote.

Maoni ya wasomi
Mhadhiri wa Shule ya Siasa ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk James Jesse alisema ili kuondoa kile alichokiita ‘kusumbuliwa’, jukumu la kumshtaki Rais mstaafu au aliyepo madarakani linapaswa kuachwa mikononi mwa Bunge.

“Katiba imeeleza wazi kwamba ataondolewa madarakani kwa azimio la Bunge. Binafsi nadhani utaratibu huo ndiyo mzuri hata kama atakuwa amemaliza muda wake, hoja ya kumshtaki ianzie bungeni,” alisema .

Naye Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia, Innocent Shoo alisema, “Tukizingatia demokrasia za kisasa, rais akitoka madarakani hapaswi kuwa na kinga ya kushtakiwa. Hii inatakiwa iwezekane hata akiwa madarakani ili kuzingatia utawala wa sheria.”

Katika ufafanuzi wake, Shoo alisema kuwa kutokuwajibika na utamaduni wa kutokujali ni utambulisho wa viongozi wengi barani Afrika huku akinukuu kauli ya Rais wa Marekani, Barack Obama, kwamba “Afrika inatakiwa kuwa na taasisi imara siyo mwanaume mwenye nguvu.”

Shoo alisema nchi nyingi barani Afrika hazina chaguzi huru, haziheshimu haki za binadamu na uhuru wa watu na taasisi mbalimbali, mambo aliyodai kuwa yanafaa kumfanya Rais kushtakiwa.

“Umeona kilichotokea Brazil? Ule ni mfano hai kuwa rais anaposhindwa kufuata sheria na taratibu ashtakiwe tena ashtakiwe hata akiwa madarakani,” alisisitiza.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua), Profesa Damian Gabagambi alisema, “Anapaswa kushtakiwa anapomaliza utawala wake na hasa kama wakati akiwa rais alikuwa akifanya mambo ya kulihujumu taifa.”

Profesa Gabagambi ambaye alikuwa mmoja wa wataalamu walioandaa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), alisema kushtakiwa siyo kufungwa kwa kuwa mtuhumiwa atakwenda mahakamani na kujitetea.

“Hii itasaidia viongozi wakati wa utawala wao kuheshimu utawala bora na kufuata sheria na Katiba ili kukwepa kushtakiwa, mara wamalizapo kipindi chao cha kuongoza,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch alisema Katiba inampa Rais kinga ya maisha, jambo ambalo si sahihi huku akieleza kuwa wazo la Kikwete la kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya lilikuwa zuri ila liliharibiwa na wanasiasa.

“Kinga aliyonayo rais ndiyo inayompa kiburi na ndiyo sababu akiwa madarakani akishauriwa hataki, ila akimaliza muda wake anajuta kwa uamuzi aliouchukua,” alisema Olouch huku akisisitiza kuwa hayo ni maoni yake binafsi si ya CWT.

Akitolea mfano wa kilichomkumba Rais wa Brazil, Oluoch ambaye alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, alisema hata kama nchi nyingine nazo zina kinga kwa marais wao, si lazima Tanzania kubaki na kinga hiyo kwa kuwa kila nchi ina utamaduni na ustaarabu wake.

“Rais wa Tanzania yupo juu ya sheria. Mfano Benjamin (MkapaRais wa Awamu ya Tatu) amesema anajutia uamuzi wake wa ubinafsishaji na kutowekeza katika elimu. Hayo ni baadhi tu ya makosa wanayoyafanya viongozi wetu,” alisema Oluoch.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema kuondoa kinga ya Rais baada ya utawala wake ni hatari kwa usalama na demokrasia ya nchi.

Alisema kwa kuwa kila kiongozi hufanya maamuzi ya kisiasa ambayo wakati mwingine hayatimii, kuondolewa kwa kinga hiyo kunaweza kukaleta matatizo ya kisiasa kwa siku za mbele.

“Kuna mtu atakuja kung’ang’ania ikulu endapo atatambua kuwa yupo kwenye hatari ya kufikishwa mahakamani,” alisema Profesa Mukandala na akashauri zianzishwe taasisi makini na imara zitakazokuwa zinamshauri Rais juu ya maamuzi mbalimbali anayoyafanya akiwa madarakani.

Alisema hakuna haja ya kuwafikisha mahakamani viongozi wa ngazi hiyo, kama makosa yao yalitokana na mtazamo wa kisiasa na kukumbusha kuwa hata Rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere alishindwa kutekeleza mkakati wa kuanzisha Vijiji vya Ujamaa kama ulivyoratibiwa sawa na ilivyotokea kwenye Katiba Mpya kipindi cha Rais Kikwete.

Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, kimeunga mkono kauli ya Jenerali kuhusu Kikwete kushtakiwa kuhusiana na mchakato wa Katiba ambayo haikupatikana.

Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani alisema CUF inaunga mkono kwa asilimia 100 kauli hiyo, kwa sababu sehemu kubwa ya matatizo yaliyojitokeza na yanayojitokeza Zanzibar yamesababishwa na kutopatikana kwa Katiba Mpya.

“CUF tungekuwa na uwezo hata leo tungetaka ashtakiwe haraka iwezekanavyo. Kwa sababu Kikwete ni mmoja wa watu aliyevuruga uchaguzi Oktoba 25, mwaka jana,” alisema Bimani.

Lakini Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vua Ali Vuai alisema maoni ya Jenerali si sahihi na si ya kiungwana kwa kuwa yana lengo la kuleta uchochezi kwa wananchi dhidi ya Kikwete.

“Huu ni upotoshaji kwa wananchi, kwa sababu Kikwete amefanya mambo makubwa nchini. Sioni sababu ya kusema fedha nyingi zimetumika wakati mchakato huu bado unaendelea, ukisubiri kupiga kura za maoni.

Chanzo: Mpekuzi
 
JK mjanja sana. Hakuna anayeweza kumuweka kati na kumsulubu.
Wataishia kuaibika wanaotaka kumshitaki JK.
 
Hata akiukumiwa utasikia akatumikie jamii mwezi hospital saizi itakuwa ya Lugalo then anakuja wiki moja issues imeisha bongo raha kweli
 
Kwa sheria ipi.na nani ana uwezo wa kumshtaki kikwete na hata Kama sheria ni msumeno au mnaropoka tu humu
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema kuondoa kinga ya Rais baada ya utawala wake ni hatari kwa usalama na demokrasia ya nchi.

Alisema kwa kuwa kila kiongozi hufanya maamuzi ya kisiasa ambayo wakati mwingine hayatimii, kuondolewa kwa kinga hiyo kunaweza kukaleta matatizo ya kisiasa kwa siku za mbele.

“Kuna mtu atakuja kung’ang’ania ikulu endapo atatambua kuwa yupo kwenye hatari ya kufikishwa mahakamani,” alisema Profesa Mukandala na akashauri zianzishwe taasisi makini na imara zitakazokuwa zinamshauri Rais juu ya maamuzi mbalimbali anayoyafanya akiwa madarakani.

Alisema hakuna haja ya kuwafikisha mahakamani viongozi wa ngazi hiyo, kama makosa yao yalitokana na mtazamo wa kisiasa na kukumbusha kuwa hata Rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere alishindwa kutekeleza mkakati wa kuanzisha Vijiji vya Ujamaa kama ulivyoratibiwa sawa na ilivyotokea kwenye Katiba Mpya kipindi cha Rais Kikwete.

Kama hii ndio namna ya profesa kufanya reasoning sijutii kamwe kutokufika chuo kikuu.

Yaani, Profesa Mukandala anaamini kuwa, rais akiondolewa kinga ndio atang'ang'ania madarakani lakini hakuweza kuona kuwa rais akiwekewa kinga anaweza pia kung'ang'ania madarakani kwa kuwa anajua hata jaribio lake likishindwa au kufanikiwa hatashitakiwa na yeyote yule?

Yaani, Profesa Mukandala anashauri zianzishwe taasisi imara na makini za kumshauri rais na bado haoni haja ya rais huyo huyo kubanwa kwa sheria fulani endapo atakataa kusikiliza ushauri wa taasisi hizo!!!

Yaani, Profesa Mukandala anaona kuwa 'kwa kuwa Mwalimu Nyerere alishindwa' basi kila rais ajaye naye anapata haki ya kushindwa na katika hili labda niulize: Mwalimu Nyerere ndio 'marking scheme' ya utendaji wa viongozi wetu wajao?

Hivi profesa anaweza kuainisha hatari za kiusalama na kidemokrasia zinazoikumba Marekani, South Africa na Brazil (kwa kutaja chache) kwa kuwa viongozi wao wa juu wanabanwa na sheria?

Ee Mungu tuhurumie!
 
Kama hii ndio namna ya profesa kufanya reasoning sijutii kamwe kutokufika chuo kikuu.

Yaani, Profesa Mukandala anaamini kuwa, rais akiondolewa kinga ndio atang'ang'ania madarakani lakini hakuweza kuona kuwa rais akiwekewa kinga anaweza pia kung'ang'ania madarakani kwa kuwa anajua hata jaribio lake likishindwa au kufanikiwa hatashitakiwa na yeyote yule?

Yaani, Profesa Mukandala anashauri zianzishwe taasisi imara na makini za kumshauri rais na bado haoni haja ya rais huyo huyo kubanwa kwa sheria fulani endapo atakataa kusikiliza ushauri wa taasisi hizo!!!

Yaani, Profesa Mukandala anaona kuwa 'kwa kuwa Mwalimu Nyerere alishindwa' basi kila rais ajaye naye anapata haki ya kushindwa na katika hili labda niulize: Mwalimu Nyerere ndio 'marking scheme' ya utendaji wa viongozi wetu wajao?

Hivi profesa anaweza kuainisha hatari za kiusalama na kidemokrasia zinazoikumba Marekani, South Africa na Brazil (kwa kutaja chache) kwa kuwa viongozi wao wa juu wanabanwa na sheria?

Ee Mungu tuhurumie!
we unadhani kwanini chuo kikuu chetu kumeporomoka ?
 
JK mjanja sana. Hakuna anayeweza kumuweka kati na kumsulubu.
Wataishia kuaibika wanaotaka kumshitaki JK.
lowasa na jk dugu moja wataendelea kuimba fisadi fisadi fisadi hakuna atakayekamatwa kati yao badala yake wezi wa kawaida ndo watakaa lupango


aka kina masamaki
 
Back
Top Bottom