Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Ninyi kuwaona wote wanaowapinga kuwa si raia una ni sawa?
Kwenye JMT raia wote tunatakiwa tiwena hadhi sawa bila ya kuwa na madaraja.
Mkuu umeeleza vyema sana.Isipokuwa unapotumia neno "NINYI" Si vizuri mana mimi si WAO mimi ni mimi tu.

Kitendo cha KUNYANYASA mtu yeyote kwa KISINGIZIO cha kujua URAIA wake kwa sababu AMEKOSOA serikali ni MAKOSA makubwa sana yasiyostahili katika Tanzania ya leo.
Nakubaliana nawe. MADARAJA hayastahili kabisa.
 
Kweli kabisa madini hayaibiwi kwa sababu ya ukuta?
 
Tena kwa staili hii ya sasa ya kukomoana na kulipizana visasi,kabisa na mimi naona ndiko tunakoelekea siku za usoni.
Hamna jambo baya kama kuwa na roho ya kisasi. Kinachohitajika ni uvumilivu mkuu.
Ila kwa MAFISADI wakatia wao ukifika haitakuwa ni kisasi bali ni SHERIA.
 
Heshima Mkuu ni two way traffic. Kama aliyemo ndani ya Taasisi husika haheshimu taasisi husika usitegemee na yeye avune heshima. Mbona Baba wa Taifa Watanzania wengi bado wanamuheshimu na kumuenzi kwa miaka mingi sasa!?
Ni kweli nakubaliana nawe katika mambo ya heshima na kuheshimiana.
 
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu Sana
 
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu Sana
Katiba ni HAKI ya Mtanzazania. Hatuna haja ya kuwa na katiba iliyojaa UJAMAA JAMAA wa miaka ya nyuma.
 
Sheria HAINA HURUMA.
Angalia mama wa watu huko Korea Kusini. Miaka 24 BILA HURUMA.
Ndo maana wamefanikiwa kuliko sisi tunalindana. Hilo la kulindana halitadumu.
Ndo litakalokuja kila mwenye kukinywea kikombe atakinywa japo wanaupofu siku zaja watajibu,kuhusu matumizi mabaya ya Madaraka, matumizi mabaya ya fedha za umma,ukiukaji wa haki za binadamu,kupotea kwa watu,nk uzuri technology utunza kumbukumbu na ushahidi, haijalishi ni kipindi gani lkn haki itasimama,pale kinga zitakapoondolewa.Zuma akutegema,Grace Mugabe Kwa heshima ya Mugabe ila akirudi Kwa Muumba ataisoma namba,wasiojulikana wa dikteta mlozi wa Gambia wanasakwa na kukamatwa popote walipo Gambia wanapelekwa jela,waliomuuwa Thomas Sankara kwa amri ya compaore washakamatwa,Mobutu pona yake kufia Morocco zaidi ishu ya Lumumba ilikuwa inalala nae.
 
Wale wanaotaka raisi afanye miaka 7 wasisahau na kuongeza kifungu kitakachosema raisi ashtakiwe kwa makosa atakayofanya akiwa madrakani
 
Binadamu hujisahau sana. Historia HUTUNZWA na haifutiki.

Mfano mwingine , ni wa wale waliohusika na mauaji ya kimbali ya Wayahudi kwa amri ya Hitler. Miaka ilienda mpaka ika fika 40 lakini mwishowe walitafutwa WAKAKAMATWA wakiwa wazee sana.

Hata hivyo sheria haiangalii UZEE inaangalia USHAHIDI na historia.Mwishowe walihukumiwa bila kujali kama walikuwa wanatembelea wheel chair ama la.
Hata Angola Binti wa Rais mstaafu ambaye ni TAJIRI sana kulingana na gazeti la Forbes. Tayari anachingizwa na MKUU wa MASHTAKA ya serikali bilakujali alikuwa mtiti wa nani.

Ukitoka madarakani wewe ni raia. na ni lazima ujibu.
 
Wale wanaotaka raisi afanye miaka 7 wasisahau na kuongeza kifungu kitakachosema raisi ashtakiwe kwa makosa atakayofanya akiwa madrakani
Hilo LA MAKOSA ya AKIWA kazini hayo HAITAKUBALIKA. KWA SABABU RAIS YEYOTE NI LAZIMA ALINDE NCHI.

Isipokuwa kama ALIKIUKA Katiba ya nchi, na KUJINUFAISHA kwa UFISADI ama MAUAJI YA kisiasa hilo si moja ya KUAPO cha rais yeyote yule duniani. Hapo Mtuanaweza KUSHTAKIWA.

Lakini kama alifanya makosa ya kawaida katika utenda kazi wake ASISHITAKIWE. Maana haitakuwa nchi tena bila sheria na utii.
 
Mwalimu Nyerere, alipobaini kuwa wimbi la vyama vingi litamwaibisha. akasema BADUKUSHENI katiba na muweke kipengele cha vyama VINGI. Akaheshimika sana
Kusoma nyakati kunasaidia sana.
 
kwani ule mchakato wa kuibadilisha umeishia wapi!?
 
Mkuu hapo umekosea. Heshima si utumwa. Ni vizuri tuiheshimu taasisi ya URAISI hata kama hukubalini naye.
Ni MTANZANIA mwenzetu na wala si hivyo usemavyo.
Tujadili hoja badala ya matusi na kubezana. Ama vipi mkuu?

Watanzania hawanaga roho mbaya ww! huyo unayemtetea ni muhutu...ana roho ya kunjo mufete.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…