Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Serikali ndio yenye watawala waliojiwekea kinga. Ndio huwapa uwezo WA kufanya uyasemayo. Kuweka kisu shingoni mwao utasubiri mpaka yesu aje.
Sisi wananchi tukidemand hilo,haliwezekani???
 
Nchini korea kusini,tumeshuhudia Rais wa zamani wa nchi hiyo akikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo jela cha miaka 15 kwa kupokea rushwa!
Kwa nchi hiyo pekee,Lee ni Rais mstaafu wa 4 kuhukumiwa kifungo kwa uhujumu uchumi!
Pia suala kama hilo limeshatokea nchi mbalimbali kwa marais wastaafu na mawaziri wakuu kukutwa na hati kwa makosa ya rushwa na ufisadi!
Kwa mantiki hiyo,Tanzania siyo kisiwa!Ni wakati sasa kwa serikali kupeleka muswada ili kuwe na uwajibikaji!
Nchi za Africa ndizo zinazoongoza duniani kwa kuwa na corrupt government!Hasa ukizingatia ni juzi tu China imesema yenyewe haipaswi kulaumiwa kwa viongozi wa nchi za africa kwa kuwa corrupt kwani wao sio waliowaweka madarakani,hii ilitokana na china kushutumiwa kuzihadaa nchi za Africa na kuwapa mikopo mikubwa isiyolipika kisha kushikilia vitega uchumi vya nchi hizo!

Kwa Muktadha huu,ni vema Rais Mzalendo JPM akachukua hatua ili kuweka misingi ambayo hata akiondoka,kusiwe na Rais atakayedhani anaweza kula rushwa huku akijua ana kinga ya kutoshtakiwa!!!
Wakati ni sasa,badala ya kuhangaika na visheria visivyokuwa na kichwa wala miguu kama sheria ya takwimu,ni vema tukafanya remarkable reforms kwenye sehemu nyeti kama hizo!
Unategemea mwenye kisu ajichinje mwenyewe?
 
Siku Magufuli akifanya hivo nitaamini kuwa yeye ni mzalendo Nambari one toka Tanzania iwepo
 
Wenzetu korea walifanyaje mpaka wakawa na sheria hizo?
Soma historia za mataifa hayo,halafu ujiulize,je,upo tayari kupita njia iliyowafikisha hao wenzetu huko?

Kama haupo tayari,basi kaa kimya,usubiri kuzeeka then ufe,uwaachie watoto wako pia wakiendelea kuota ndoto kama ya kwako,na wao watazeeka na watakufa,itabaki hivyo mpaka wawepo watu watakaopitia njia walizopitia wenzetu unaowasema!
 
Nways,nadhani kama tuna uthubutu tunaweza!
 
Back
Top Bottom