Hivi ndugu zangu ni kwanini uwezo wetu wa kufikilia unakuwa duni sana kiasi hichi.
Unataka kuniambia hawa wabunge na viongozi wengine wote hawaoni upungufu wa sheria hii kuwa ni mwanzo wa maovu kama haya, angalia mambo ambayo mkapa kayafanya mpaka anaona aibu kuongea na watu, lakini eti sheria inamlinda.
Nadhani sheria hii ilikuwa inastaili enzi hizo za Baba wa Taifa waliokuwa waadilifu na wazalendo kweli ambao mpaka sasa tunatamani wangekuwepo, lakini sio enzi hizi za akina mkapa kikwete, tunaoomba hata wapate matatizo yoyote na watoweke muda wowote kwa jinsi walivyotutesa na wanavyoendela kututesa watanzania,
Na ni kwanini hata wabunge wasishirikiana hata katika hili jamani, hii katiba yetu mbona mbovu namna hii jamani, watu wanaiangalia tu kwa sababu ndo inawapa ulaji tu sio
Poa, ila iko siku itafika tu na mambo yataenda kama tunavyotaka