Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Waacheni wajadili mwisho mwisho maana mzee wa majipu ameanza kudhibiti mijadala
 
Mjadala mkubwa kwa hivi sasa nchini ni kauli ya Jenerali Ulimwemgu kutaka rais mstaafu Kikwete kufikishwa mahakamani kwa kutumia vibaya fedha za umma kwenye mchakato uliokwama wa katiba mpya. Kwanza watu wanatakiwa kujua kwa Jenerali anajua zaidi yao kwamba Kikwete hawezi kushitakiwa kwani katiba yetu hairuhusu rais mstaafu kushitakiwa mahakamani

Tumeona marais wastaafu kama Kaunda, Mubarack, Bagbo na wengine wakifikishwa mahakamani. Kama tunasema mahakamani ni sehemu ya kutoa haki ni kwa nini hatutaki marais wetu wafikishwe huko? Wakiwa madarakani wanawapeleka wengi huko na ukiwauliza wanakwambia kwani kuna ubaya gani, kama huna hatia si unaachiwa tu? Sasa tunaogopa nini kuwapeleka wastaafu wetu? Kama hawana hatia siwanaachiwa tu?

Kwa upande wa Kikwete na kama katiba ingekuwa inaruhusu kuna shida gani angepelekwa mahakamani? Alianzisha yeye mchakato, ulipokwama ni kweli alijitahidi kuukwamua na ulipokwama hawezi kukosa kulaumiwa kama ambavyo asingekwepa sifa kama ungefanikiwa. Anatuhumiwa kujaza watu wa chama chake kwenye BMK na ndiyo waliokwenda kuzomea na kuhakikisha matakwa ya chama chao yanapita.

Kama mnakumbuka wakati akipokea katiba pendekezwa uwanja wa Jamuhuri Dodoma alitolea mfano wa jini kwenye chupa. Alisema wakati mwingine unalibembeleza jini likirudi kwenye chupa unafunika chupa, umemaliza mchezo. Alimanisha kuwadanganya vyama vya siasa chini ya TSD walipokubali kurudi nyuma baada ya kukutana nao na kuwaaidi kurudisha katiba pendekezwa bungeni akafunga chupa.

Watanzania tujifunze kutetea uhuru wa maoni. Badala ya kumtetea Jenerali mwananchi wa kawaida tunamtetea Kikwete mtu mwenye nguvu na vyombo vya kumtetea. Hivi Jenerali ana kosa gani? Kutoa maoni kama mtanzania? Kuna kosa gani rais mstaafu kufikishwa mahakamani kama katiba ingeruhusu? Alikuwa anajadili mkwamo wa kikatiba na inawezekana hawa wakubwa ndiyo maana hawataki katiba mpya kwa sababu wanataka kinga ziendelee!
 
Natarajia watu watazingatia uhuru wangu wa kujieleza pia
 
Rangi ya mtu mweusi inaakasi ubongo wake na ule usemi wa Africa is a black continent.Nchi za Ulaya wenzetu maraisi wanashitakiwa ila huku Afrika ni shiida.Waafrika tubadilike.
 
Raisi wetu akishtakiwa ni tatizo.
Kwanza waliongoza wakiwa na kinga hivyo kuna mambo walijaribu tu kwa kuwa walijua hata wakishindwa sheria haiwabani. Mfano mzuri ni hilo la katiba mpya, raisi alijaribu tu kutaka kupanua demokrasia, matokeo yake ccm na ukawa wakamuangusha raisi kwa kulinda maslahi ya vyama vyao, laiti kama angejua asingeanza au angeumalizia tu no matter what!
Imapofikia wakati tunaomba raisi ashtakiwe, then tutapaswa kumuacha afanye kazi kwa kuangalia utashi wake zaidi kuliko sasa, huku ukawa wanataka nini sijui, huku Zitto etc!
Ila hata kama tunataka raisi ashtakiwe ni kwa kushindwa kuachieve au kwa makosa ya jinai, ubadhirifu na mengine ya aina hiyo?
Kama tunataka raisi ashtakiwe kwa under achievements then kila mtanzania then awe subjected ktk sheria hiyo, Mwl wanafunzi wakifeli ndani! Daktari wagonjwa wakifa naye afungwe etc!
Hilo pia liwakute hata viongozi wengine wa vyama vya kisiasa! Taasisi za umma etc!
 
nijibu kulingana na swali lilivyoulizwa na jibu langu ni hivi HAKUNA UBAYA HATA CHEMBE.
 
Wanasheria naomba kuuliza: Hivi rais akiwa madarakani akafanya kosa ambalo linathibitisha kuwa alikuwa na mens rea sheria inasemaje. Mfano: Unaingia madarakani nyuma tulikuwa na ugomvi, unasema piga risasi huyo maadamu hakuna atakaye kuuliza, Je bado kinga itatumika kumlinda akitoka madarakani. AU rais anaiba hela anapeleka ulaya kwa kumwamrisha gavana, je sheria itamlinda?
 
Umekosea mlango wa kuingilia
Hapa ni siasa tu!
Peleka sehemu ya msaada wa sheria humuhumu JF.
 
Ndio maana tunapendekeza katiba mpya ipitishwe ili hata wazito waweze kuwajibishwa, walijitungia sheria kulinda maslai yao hivyo mabadiliko ya katiba yataendana na mabadiliko ya baadhi ya vifungu vya sheria
 
Hata rasimu ya Warioba ile original ilikuwa bado ina mkinga rais asishitakiwe na sikumbuki kama kuna mjumbe yeyote hata wa UKAWA aliyezungumzia hili wote walikuwa busy na idadi ya serikali za muungano.
 
Mara nyingi wanasheria huwa sio wanasiasa

Wanasheria wa nchi gani?

Are you serious?

Kuna haja ya TCRA kuzima na akili feki sababu mtu mwenye ubongo feki hata akitumia simu original bado ni tatizo.
 
Tena katiba ingekuwa wazi kabisa 'raisi akifanya PUMBA akiwa madarakani basi atanyongwa akitoka madarakan'i! tungekuwa tunapata maraisi waangalifu sana
 
Hata rasimu ya Warioba ile original ilikuwa bado ina mkinga rais asishitakiwe na sikumbuki kama kuna mjumbe yeyote hata wa UKAWA aliyezungumzia hili wote walikuwa busy na idadi ya serikali za muungano.
Kama umeipitia rasimu ya katiba pendekezwa sura ya Nane sehemu ya kwanza kipengele b (Rais) kifungu cha 94(1) Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii. Isome hiyo attached file ni rasimu_ya_katiba_inayopendekezwa_na_bunge_maalum
 
Attachments

Wanasheria wa nchi gani?

Are you serious?

Kuna haja ya TCRA kuzima na akili feki sababu mtu mwenye ubongo feki hata akitumia simu original bado ni tatizo.
Asante mkuu kwa kuwa wewe unaakili nyingi
Tcra hawatakuzima
 
Back
Top Bottom