Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Mahakama ya mafisadi ni demagogue nashangaa wanaoitilia maanani.
Kama ipo ianze na kesi ya uuzaji nyumba za Serikali na iwabane wale waliojiuzia nyumba zaidi ya moja , kumbuka wengine walijuzia nyumba kibao wakazigawa mpaka Kwa ma-small house wao.
 
YEYE NI RAIS ALAFU AWANYANYASE WENZAKE MARAIS WALIOPITA NA WAKATI NA YEYE ANAJUA ATAPITA NA HUKU ANAELEWA UNACHOPANDA UTAVUNA. HATA MIE NINGEKUWA YEYE NINGEFANYA ANAVYOTAKA KUFANYA.
 
kama ana kashfa nzito kwa nini sasa hawampeleki mahakamani? ina maana hizi mahakama tulizonazo haziwezi kusikiliza tuhuma zake mpaka iunde mahakama maalum ya mafisadi? na hao majaji watakuwa ndio hao hao wa mahakama za sasa au na wao wataagizwa toka nje ya nchi ili kuleta utofauti?
Richmond ni ya Kikwete .
 
YEYE NI RAIS ALAFU AWANYANYASE WENZAKE MARAIS WALIOPITA NA WAKATI NA YEYE ANAJUA ATAPITA NA HUKU ANAELEWA UNACHOPANDA UTAVUNA. HATA MIE NINGEKUWA YEYE NINGEFANYA ANAVYOTAKA KUFANYA.
Amejihami mapema baada ya kuambiwa kuwa endapo atawaandama wataungana na kumhujumu na yeye pia kupitia wale Watumishi waliowapa madaraka Enzi zao.
 
Mnafahamu sheria na katiba inasemaje? Hapo angewashtaki mngesema anavunja katiba na dikteta. Uwezo mdogo

Wewe ndiyo uwezo wako mdogo. Kama katiba inawalinda kulikuwa na haja gani ya Rais kutoa hiyo kauli kwamba atawalinda....?! Au na yeye hafahamu katiba??!!
 
hapa anaanisha makandokando, mauchafu yote yanayohusiana na marais wastaafu moja kwa moja au isiwe moja kwa moja hayataguswa, hii inatufungua macho kuhusu sakata la Lugumi kuwa wahusika hawataguswa
 
tuvute subira kidogo tuone
huu ni mwaka wa 55 tokea uhuru sasa sijui subira ipi maana kama ni mtoto alizaliwa ameishafika umri ambao anaweza kustaafu. bado tuendelee kuvuta pumzi lol!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kama ipo ianze na kesi ya uuzaji nyumba za Serikali na iwabane wale waliojiuzia nyumba zaidi ya moja , kumbuka wengine walijuzia nyumba kibao wakazigawa mpaka Kwa ma-small house wao.
hahahaha hii ikienda mahakamani nitajua kweli inamaanisha maana waziri alikuwa nani vile?????????????
 
Badilisheni katiba ili muwafumge hao mnaotaka. Mbona kila siku mnalia jamaa hafuati katiba, leo mnataka asiifuate awapeleke wenzake mahakamani?

Na ndicho hasa alichopaswa kukifanya!

Hii nchi utakuwa ni mwendawazimu kudai utapambana na rushwa kubwa kubwa a.k.a ufisadi pasipo kuingia sebuleni hadi kwenye master bedrooms za marais wastaafu especially mzee Mkapa na Kikwete!!

Hizi kelele za sijui Lowassa fisadi sijui nini ......ni kujilisha upepo tu wa siasa za kufarijiana!!
 
Hivi mlivoambiwa CCM ni ile ile inamaana hamkuelewa?

Ndo hivo sasa.... mmeipenda wenyewe, chaguo lenu wenyewe.....

Kilichobaki ni kuisoma namba tu
Mbona ubajenga imani kuwa kila kiongozi wa juu tz ni fisadi au pengine na wewe fisadi hivi unajua serikali inavyoendeshwa au ni jobless
 
Mbona ubajenga imani kuwa kila kiongozi wa juu tz ni fisadi au pengine na wewe fisadi hivi unajua serikali inavyoendeshwa au ni jobless
Asa hapo ndo umeandika nini?

Hivi shuleni ulienda kujifunza ujinga?
 
Anamaanisha atawalinda kwenye maovu yao yote ya ufisadi walipokuwa madarakani. Kama utakumbuka Salma Kikwete na Ridhwan ni shareholders wa UDA ambayo imekwapuliwa kinyemela kutoka halmashauri ya jiji la Dar na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali katika ripoti yake ya mwaka aliandika kuhusu ufisadi huu. Jamaa kaamua ile ripoti iendelee kupigwa na vumbi pale Ikulu ili kuendelea kuwakingia kifua wakwapuzi wa shirika la UDA, na huyu ndiye aliyejinadi kwamba kajitoa kafara ili kupambana na ufisadi nchini.
Chama cha Majipu kina utamaduni, sera na utaratibu wa kulindana. Mtakatifu ameeleza bayana tu kwa wale waliolishwa ahadi hewa ya kupambana na ufisadi na kutumbua majipu.

Link Kaduma: JPM arejeshe nyumba za Serikali
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Cc Askofu Gwajima
Wewe ni Kilaza #1,
Rudia tena kusikiliza meseji ya Gwajima. Hakusema Magu amshitaki rais Mstaafu, bali abadilishe katiba ili Rais ashitakiwe. So hata Gwajima anajua kua kwa Katiba ya sasa rais hawezi kushitakiwa.
 
Sasa kama nilajulikana kuna sababu gani ya Mtukufu Rais kulizungumzia kana kwamba yeye ndiye mwenye madaraka ya kuamua kuwashtaki au la? Ni nani mwenye akili zilizopo likizo kati ya UKAWA na Mtukufu?
kweli kabisa.madaraka ya kuona kama mtu ana kosa ama hana kosa ,ashitakiwe ama la. Si wajibu wa Rais. Na inapofika raisi anaujulisha umma kwamba atamlinda mtu anawapa ujumbe hao wa mahakama ambao wanateuliwa na raisi wanyamaze. Hapo ndipo swala la akiba ya maneno linakuja.
 
Ukweli ni kuwa kama siyo sheria kunibana basi ningekuwa nimeshafungua kesi kadhaa dhidi ya rais Magufuli kutokana na mwenendo wa matamko yake.

Kwanza nikiri kuwa yapo maeneo machache ambayo rais anafanya vizuri kama mkuu wa nchi na eneo hilo ni nidhamu ya kazi ingawa imechangishwa na uoga hivyo kukosa matokeo chanya kwa kiwango kikubwa juu ya ukuaji wa uchumi. Lakini kwa ukweli ulio mchungu kabisa, rais Magufuli kama ataendelea hivi basi huenda akawa ni rais wa bahati mbaya kabisa kwa nchi kuwahi kuwa naye na mbaya zaidi huenda hadi mwaka 2020 tukajikuta tuna taifa lenye taswira tofauti kabisa na wengi wetu wakabaki wakijiuliza kulikoni?

Kauli nyingi sana za rais Magufuli zinaliweka taifa katika mashaka makubwa sana, zinavutia mgawanyiko wa hali ya juu.

Kama kiongozi mkuu wa nchi pale unapoongea au kufanya jambo, ni tofauti kabisa na watu wengine hata kina Lowassa, Mbowe na Maalim Seif. Kiongozi wa nchi kama atashindwa kuchochea umoja basi ni heri ajiuzulu mapema kwani ameshindwa kuwa mkuu wa nchi kwa hatua za awali kabisa, umoja haujengwi kwa kuwatisha watu wenye ufuasi mkubwa nchini wala kuwatisha wafuasi wao. Kuendelea kuyatisha makundi mbalimbali kuna siku yanaweza kuungana na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kujibu mapigo na hapo ndipo yanapotokea mambo kama ya kaskazini mwa Uganda, Mashari mwa Congo na Sudan ya kaskazini vs Sudan ya kusini.

Sasa basi, kwa kuwa mheshimiwa rais anaonyesha kutokubadilika huku kasi hiyo ikizidi, ni bora akabanwa na mhimili wa kutekeleza sheria na ule mwingine wa kutunga sheria ingawa umeingiliwa ila bado unaweza kujipa meno ikiwa utakuwa kitu kimoja kwa wengi wao.

Ikiwa wabunge wataungana na kubadili sheria ama kuonyesha waziwazi kuwa yapo matamshi wasiyokubaliana nayo kutoka kwa rais (najua kwa sasa wapo wengi kutoka CCM) basi wanaweza kubadili sheria na kuifanya mahakama iwe na meno juu ya rais aliyeko madarakani na hapo kama nchi tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwa mustakabali wa taifa. Ama kwa kuonyesha tu uimara wao na kupaza sauti.

Haya yakiendelea hivi, basi ni majaaliwa mbeleni.
 
Back
Top Bottom