Moja ya mapendekezo yanayopelekwa bungeni ni polisi kutoadhibiwa Kwa jinai pale wanapotekeleza majukumu Yao wakiwa undercover na kusababisha jinai . Kwa mfano polisi yupo undercover akapiga mtu RISASI akidhani ni mwalifu awezi kushtakiwa.
Ikitokea polisi Kuna maandamano au Kuna Jambo lolote la kutafuta haki linaendelea polisi wakataka kulizima na katika kulizima ikatokea jinai basi huyo askari atochunguzwa wala kufikishwa mahakamani Kwa tuhuma zozote.
Aina hizi za Sheria zinaletwa Tanzania Wakati Nchi nyingine ikiwemo Kenya walishafuta kesi hizi na Kinga za aina hii na kuziondolea mbali ambapo Kenya hata Rais akitenda jinai anashtakiwa. Tumeona Afrika Kusini na mataifa mengi yanayojali haki ya kuishi na haki ya Kila mtu yupo chino ya Sheria wakiongoa hizi Sheria. Kwa Tanzania Rais, Makamu, Waziri Mkuu, spika, judge, na Sasa police nao Wana Kinga. Kwa maana nyingine Wananchi pekee ndio wasio na Kinga ila watumishi wa umma wengi na wanasiasa wamewekewa Kinga.
Kwanini tunawaza kuhalalisha uhalifu Kwa watu wanaolipwa mishahara? Hivi hii Kinga ingekuwepo Leo Waziri Mkuu angeenda kuunda Tume ya issue ya Mtwara? Kwanini tusitegemee Kuanzia kesho kutwa Sheria ikipita basi Kila mauaji ya dola tunaambiwa yanafanyika undercover? Kwanini Sheria kama hizi zinapelekwa kwa hati ya dharura? Kuna uharaka Gani?