Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Comrade yuko sawa kabisa ila anamsha hisia zilizolala, yaani mara hii amesahau nguvu waliyoitumia kuhujumu ile rasimu ya katiba ya Warioba ambayo ilikuwa na hicho anachokisema tume huru, hawa watu wanatufanya watanzania kama hatuna uwezo wa kufikiri vile.
tena wanatufanya kama mazezeta
 
Napenda tukumbushane wanasiasa wa ukawa na ccm kuwa bila kushikamana kama nchi huenda kila kitu kitakuwa ovyo mpaka siku moja watoto wetu watatuona kama akina chifu a.k.a Mangungu,
Hebu bila Kupepesa Macho nielezeni wana jamvi,hivi kweli Magufuli ana nia ya kututoa hapa tulipo au ni Hekaya za Abunuasi.
Kumbukeni kateua mtu baada ya Jaji Lubuva hii inamaanisha,Hakuna swala la Tume huru mpaka kusiko julikana.
Wapinzani nao a.k.a Ukawa badala ya Kuongelea swala la Tume huru wamekazania Maisha Magumu ambalo ni swala la Mpito,hebu jiulizeni, ni lini ukawa wamegusia swala la Tume huru ya Uchaguzi.
Pia richa ya Tume huru tulitegemea pale Dimani wazungumzie swala la Katiba mpya
Kwa taarifa yenu Teuzi zote zinazoendelea ni mkeka wa Kutuchapa 2020.
Nina imani hatuna upinzani hapa Tanzania na wala ccm siyo suruhisho,sasa kama taifa nini kifanyike.
Jibu sio uchochezi wala kutukana pale leaders,jibu ni Kuanza na Tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya.
 
Kwanza kabla ya yote niwashukuru kwakumchagua Lowassa 2015.

Ili KUSHINDA urais 2020 inatakiwa katiba ya warioba itinge na umetumbuliwa binging tumekwisha nilikuwa na maana kwamba time ya uchaguzi isiwe ya kuteuliwa kwamba Leo magu amemteua jaji wa kusimamia uchaguzi halafu kesho/2020 huyo jaji aliyeteuliwa na Sizonje aseme nyama Sizonje nimeshindwa ameshinda Lowassa.

Karibu tujadili kama inawezekana
 
Nyoosha vizuri andiko lako una haraka ya kwenda wapi? au unaandika ukiwa umeshikiwa gobole kichwani?
 
Najiuliza Sana Hilo swali nashindwa kupata majibu sahihi..

Mapambano ya uchaguzi mkuu kikwazo kikuu ni tume huru ya uchaguzi na vyombo vya ulinzi na usalama..

Ushahidi mzuri ni uchaguzi mkuu uliopita na ule wa 2010 ambapo inasemekana wapinzani waliporwa ushindi wao..

Zanzibar ndio tusiseme kabisaa kwani ccm haijawah shinda hata siku moja..

Sasa najiuliza hivi wapinzani hawajui adui yao mkubwa Kama ni tume ya uchaguzi?... Au Tanzania hakuna upinzani? Wote ni ccm tu..?

Nawaambieni wapinzani sitaki Tena kusikia eti mumeibiwa kura zenu.. sitaki na ninasema Kama ni hivyo Mimi sijisumbui Tena kupiga kura wakati refa wa mchezo huo ameteuliwa na timu mojawapo inayoshindana..

Natoa hoja wadau..!!
 
Yani mtu mzima unaleta mada halafu unasema inasemekana huoni aibu kuleta hoja za kusemekana?
 
Wapinzani hawajawahi kushinda uchaguzi hata siku moja wanachofanya ni upotoshaji tu hakuna lingine la maana hata moja.
 
Mkuu, matarajio ya watanzania ilikuwa tume huru ya uchaguzi ipatikane kupitia katiba mpya. ilivyo ni kuwa mkuu wa nchi amesema upatikanaji wa katiba mpya sio kipaumbele chake.

Kwa maana nyingine ni kuwa 2020 tutaingia kwenye uchaguzi chini ya tume yenye mfumo ule ule ambapo watendaji wake ni wateule wa rais aliyeko madarakani,huku pia akiwa ndiye mwenyekiti wa taifa wa chama tawala.

naungana nawe kuwa kwa mfumo huo na bila kutumia njia nyingine kudai tume huru ya uchaguzi upinzani kushinda itakuwa muujiza.
 
Najiuliza Sana Hilo swali nashindwa kupata majibu sahihi..

Mapambano ya uchaguzi mkuu kikwazo kikuu ni tume huru ya uchaguzi na vyombo vya ulinzi na usalama..

Ushahidi mzuri ni uchaguzi mkuu uliopita na ule wa 2010 ambapo inasemekana wapinzani waliporwa ushindi wao..

Zanzibar ndio tusiseme kabisaa kwani ccm haijawah shinda hata siku moja..

Sasa najiuliza hivi wapinzani hawajui adui yao mkubwa Kama ni tume ya uchaguzi?... Au Tanzania hakuna upinzani? Wote ni ccm tu..?

Nawaambieni wapinzani sitaki Tena kusikia eti mumeibiwa kura zenu.. sitaki na ninasema Kama ni hivyo Mimi sijisumbui Tena kupiga kura wakati refa wa mchezo huo ameteuliwa na timu mojawapo inayoshindana..

Natoa hoja wadau..!!

Simple! Ama hakuna mpinzani wa kweli nchi hii na hawa waliopo ni wasanii wachumia tumbo tu au wamepandikizwa kutudanganya sisi na wafadhili kuwa kuna upinzani Tanzania.

Hii nguvu wanayotumia kudandia matukio ya kila siku wangeelekeza kwenye kudai mabadiliko ya sheria za uchaguzi na Tume Huru wangeisaidia sana demokrasia ya Tanzania.
 
Wapinzani hawajawahi kushinda uchaguzi hata siku moja wanachofanya ni upotoshaji tu hakuna lingine la maana hata moja.
True! Haiwezekani kila siku wanalalamika kuibiwa kura kwenye uchaguzi halafu uchaguzi ukishapita hawachukui hatua zozote kudhibiti wizi huo wa kura siku za usoni.
 
Najiuliza Sana Hilo swali nashindwa kupata majibu sahihi..

Mapambano ya uchaguzi mkuu kikwazo kikuu ni tume huru ya uchaguzi na vyombo vya ulinzi na usalama..

Ushahidi mzuri ni uchaguzi mkuu uliopita na ule wa 2010 ambapo inasemekana wapinzani waliporwa ushindi wao..

Zanzibar ndio tusiseme kabisaa kwani ccm haijawah shinda hata siku moja..

Sasa najiuliza hivi wapinzani hawajui adui yao mkubwa Kama ni tume ya uchaguzi?... Au Tanzania hakuna upinzani? Wote ni ccm tu..?

Nawaambieni wapinzani sitaki Tena kusikia eti mumeibiwa kura zenu.. sitaki na ninasema Kama ni hivyo Mimi sijisumbui Tena kupiga kura wakati refa wa mchezo huo ameteuliwa na timu mojawapo inayoshindana..

Natoa hoja wadau..!!
Kwani we ni tume ya uchaguzi hadi unajua kuwa ccm haijawahi shida Zanzibar
 
Najiuliza Sana Hilo swali nashindwa kupata majibu sahihi..

Mapambano ya uchaguzi mkuu kikwazo kikuu ni tume huru ya uchaguzi na vyombo vya ulinzi na usalama..

Ushahidi mzuri ni uchaguzi mkuu uliopita na ule wa 2010 ambapo inasemekana wapinzani waliporwa ushindi wao..

Zanzibar ndio tusiseme kabisaa kwani ccm haijawah shinda hata siku moja..

Sasa najiuliza hivi wapinzani hawajui adui yao mkubwa Kama ni tume ya uchaguzi?... Au Tanzania hakuna upinzani? Wote ni ccm tu..?

Nawaambieni wapinzani sitaki Tena kusikia eti mumeibiwa kura zenu.. sitaki na ninasema Kama ni hivyo Mimi sijisumbui Tena kupiga kura wakati refa wa mchezo huo ameteuliwa na timu mojawapo inayoshindana..

Natoa hoja wadau..!!

Wapinzani walishawajulia wapiga kura wao. Kila uchaguzi ukifanyika na wakashindwa, wanasingizia neno TUMEIBIWA KURA halafu na wapiga kura nao wanawaamini hivyo. Hakuna hata mpinzani mmoja analifikiria hilo.

Wakishapata posho zao, wala hawana habari. Mara watakwambia nchi tunaichukua asubuhi na mapema, tuandamane, twende kushitaki katika vyombo vya kimataifa na wananchi musiwe na wasiwasi vyombo vya kimataifa vimesema kuwa tunapewa nchi muda siyo mrefu!

Tatizo kubwa ni tume huru na marehemu Cchristopher Mtikila alishawaonya kuwa tusiende kwenye uchaguzi mkuu bila kubadilisha tume. walimkatalia.
 
Kuna mtu aliongea point kubwa mpaka nikamshangaa. Alisema kuwe na katiba mpya au kusiwepo nao wananchi tukiamua kuitoa CCM madarakani tunatioa itake isitake. 1986 Marcos wa Ufilipino aliiba kura akajitangaza msindi.

Wananchi walivyoingia mtaani kuandamana akaamuru wapigwe na jeshi. Jeshi lilipotoka mtaani na vifaru kuwapiga wananchi wamama na masista wa kanisa katoliki waliongoza njia huku wakiwa uchi na kuwaambia wale wanajeshi ikiwa hamkutoka kweye bnyuchi zetu na mtuue na la, ikiwa mlipitia huko tuungane kuundoa huu utawala kandamizi.

Wanajeshi na wanachi wakaandamana kuelekea Macapagal palace na ndio ukawa mwisho wa Ferdinand Marcos. Tukiamua tunaweza pia katiba inasema mamlaka ya serikali yatatokana na wananchi. Hii ina maana tunayomamlaka ila hatujijui.
 
tena wasahau sanaaaa na wafute kwenye kamusi lao kuingiya ikulu labda afe lubuva2
 
Binafsi sioni sababu za makada wa CCM chini ya mwavuli wa ukurugenzi kuendelea kusimamia uchaguzi. Ikumbukwe kuwa matokea halali ni yale yanayotangazwa na tume, na ngazi ya majimbo watangazaji ni wakurugenzi wa Halmashauri/Municipal. Kwa jinsi serikali hii ilivyo, wakurugenzi wataogopa kuwatangaza wapinzani kama washindi ili kutetea vibarua vyao.

Ni vema tusiwe na uchaguzi 2020 kuliko kusimamiwa na makada kwenye uchaguzi. Ikitokea vyama vya upinzani vikakubaliana na hali hii basi vitegemee CCM kushinda kwa asilimia 98% kwenye uchaguzi mkuu 2020.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Kenya wana tume huru, lkn cha kushangaza baadhi ya watendaji wa tume iliyo huru wana uawa kama kuku, sasa kuna uhuru wa tume kweli? Marekani bali na kuwa na demokrasia na uhuru wa vyombo vyake bado kuna kelele za udukuzi wa matokeo na wizi wa kura!!! Labda kama tume hiyo watakuwa ni malaika kutoka mbinguni, vinginevyo hamna kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumeshuhudia jirani zetu wa Kenya wakifanya Uchaguzi wao ulio Huru na Haki chini ya usimamizi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka(HEBC) kwa amani na utulivu.

Tume ya Tanzania ya Uchaguzi(NEC) haijawahi kuwa Huru na Chaguzi zetu nyingi ni ujanja,wizi na Uchakachuaji wa kura ili kuibeba CCM iendelee kutawala daima dawamu. Rais wetu John Joseph Pombe Magufuli amekuwa akijinasibu kuwa yeye ni Msema kweli na Mpenzi wa Mungu. Tumeona akianza kufumua Sheria na Mikataba kadha wa kadha kama za Madini zilizokuwa zinaikosesha Serikali mapato makubwa toka kwenye raslimali za Taifa. Katika hili tunampongeza sana.

Kwa mantiki hiyo sasa naomba Rais Magufuli aliangalie hili la Katiba kwa kufanya mabadiliko kwenye Tume ya Uchaguzi Tanz ili kufanya marekebisho kania(NEC). Tunamtaka apeleke muswada kwa HATI YA DHARURA ili kuifanyia marekebisho sheria ya Tume ya Uchaguzi haraka iwezekenavyo ili ifikapo Uchaguzi Mkuu wa 2020 Tanzania tupige kura chini ya Usimamizi wa Tume Huru.

Chini ya Tume Huru ya Uchaguzi naamini mshindi atapatikana kwa Haki na hakutakuwa na malalamiko yoyote ifikapo mwaka 2020. Mshindi awe ni CCM, CHADEMA,CUF au UKAWA basi atakuwa ameshinda kwa Haki! Mambo ya kusingiziana wizi wa kura na kuchakachua hasa kwa upande wa CCM hayatakuwepo tena.

Lakini kama Rais Magufuli analiona hili siyo muhimu basi shime kwa Wapinzani kulianzisha dude kwa kupeleka muswada Binafsi kuhusu Sheria ya Tume ya Uchaguzi ili ifanyiwe kazi kwa dharura. Iwapo Serikali ya Rais Magufuli itakataa na kupuuza ombi hili basi Watanzania wajue kuwa Magufuli hana nia njema na Watanzania na hata hizo kelele za kushupalia makinikia, ufisadi, hewahewa na mikataba yote mibovu ni usanii na kutetea ulaji wa Chama chakle tu.

Wasalaam.
 
Back
Top Bottom