Kwa jinsi Mazingira yanavyokwenda, na Mchezo mchafu sana Unaosukwa na Magufuli na CCM, hali sio nzuri kabisa kwa Ukawa 2020.
Mtego Mkubwa uliopo ni kuwa Wabunge wengi Siasa ubunge kwao ni sehemu ya Ajira. Hata tume na katiba ikiwa mbovu kiasi gani, Ili mradi kuna uwezekano wa wao kushinda ubunge, ukiwakataza Kugombea Ubunge watakimbilia CCM wapo wachache Majasiri, Lakini Wasaliti kama Joshua Nasari watakimbilia CCM kwa Speed ya supper sonic.
Pia huo ni mtego Mbaya sana Kwani Tumeona CCM ni kama mafisi wasiojali kula kiungo cha Myama ambaye bado anatembea au nyama ya Mzoga ambao umeoza kiasi cha kutoa usaha! Kugomea Uchaguzi kwao itakuwa ni sherehe na njia ya Mkato ya Kuiua Chadema. Na kwa Chadema kushiriki Uchaguzi Kutakuwa ni Mhururi wa Kuwasafishia CCM ushindi haramu wa urais ambao sina shaka watajitangazia hata kama kura za Urais watapata tano. Mfano halisi ni Zanzibar. Hata hivyo kama Chadema hawako tayari kufanya mambo kadhaa Muhimu, Ninaona ni Bora washiriki Uchaguzi hivyo hivyo. Lakini Pia hofu mbaya zaidi Ni kuwa Magufuli kwa kukataza mikutano na akaona no body pushed away hard enough, msishangae bila aibu 2020 akalazimisha wagombea wa CCM watangazwe washindi majimbo ya Upinzani hata kama mpizani ameshinda kwa asilimia 98 na yule wa CCM asilimia 2.
If a man will swim with crocodiles and they do nothing, he will be used of it! CCM na Magufuli wameget away na Uhuni Mwingi, kunyanganya Komputer za Ukawa 2015 Kimya, Kufuta Matokeo ya Zanzibar, Kimya, Kukataza Mikutano ya Vyama Kimya, Kumsindikiza na Polisi Lipumba Kuvunja Ofisi za Cuf, Kimya. Tutashuhudia Vituko 2020.
Mimi Nina Suluhisho la Uhuni huu, Bila Shuruti CCM wenyewe wataomba iwepo Katiba mpya na Tume mpya ya Uchaguzi, Nitawatafuta Ukawa- Chadema only once, wakipuuza thats it. Baada ya hapo wanitafute wao au 2020 wabakie na Wabunge Watatu (3)