Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kwa maoni yangu, kama kuna watu wanazungumzia kuunda jeshi ili kushindana kisiasa hawako sahihi. Watu wa ai..na hiyo wanatakiwa kukandamizwa kwa nguvu zote ili waache uchu wa kututawala ulio vuka mipaka. Akina kingunge walisha onja asali. JPM wachunge sana nchi ibaki salama.
 
Salaam JF




Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli ya Kingunge imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Mbali na mwenyekiti kuteuliwa na Rais, wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ni wakurugenzi wa wilaya ambao pia huteuliwa na Rais kwa kuwa NEC haina wafanyakazi wake kote nchini.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

Kingunge, aliyetumia muda mrefu kueleza historia ya maisha yake katika siasa na jinsi alivyopambana katika harakati za kudai uhuru, alisema hali ya sasa ni mbaya kuliko wakati wa wakoloni wa Kiingereza ambao walikujwa wakali, kwa sababu CCM haifuati Katiba wala sheria.

“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.

Kingunge ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo ya waziri anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na mkuu wa mkoa alisema, “(Pia) Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana.”

Alisema pamoja na kwamba Chadema inapendwa na wananchi wengi na Edward Lowasa aliyegombea urais kwa tiketi chama hicho, anapendwa, bado ni vigumu kushinda kwa sababu mfumo uliopo sasa.

“Tufanye yoyote, lakini tuhakikishe, ama tunapata Katiba Mpya au vipengele hivi vya sheria vinafanyiwa marekebisho. Kwa maoni yangu, kundi hili lililo madarakani bila shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi, halitataka mabadiliko,” alisema.

Alisema enzi zao walifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitolea kwa nguvu na wengine, na yeye akiwamo, waliacha kazi za mishahara mikubwa na kujiunga na Tanu kupigania uhuru.

“Tulifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitoa mhanga. Wengi tu waliacha kazi, mtu anamaliza chuo kikuu anasema sitaki kazi anaingia Tanu kusaidia. Kwa hiyo tukawa na jeshi kubwa la vijana waliohakikisha nchi inapata uhuru,” alisema.

“Ninyi mnapambana katika mazingira magumu na wazee wenzenu walipambana katika mazingira hayo. Haikuwa rahisi. Wapo wengi walitusaliti, wengine hawakufanya lolote. Baba yangu tuligombana, nilipoacha kazi kwenda kuitumikia Tanu. Miezi sita hatukuzungumza.”


Akizungumza mkutano huo, Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwatia moyo vijana walioshtakiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, akisema bado jeshi kubwa la vijana linahitajika.

“Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Si haki kusema unakwenda mahali pengine, mwenzako amepasafisha, safisha pa kwako. Nimefurahia moyo huo. Kama alivyosema Ngombale, tunataka jeshi kubwa zaidi, watu wengi zaidi,” alisema Lowassa.

Chanzo: Mwananchi

kwani ndio anajua leo hilo? mbona watu wengi walilifahamu hilo siku nyingi. lakini mwaka 2020 wapinzani wataingia kama kawaida kwenye uchaguzi kwa vile kuna vyama vingi vimewekwa na ccm hata wakikataa ukawa ngoma itakuwa ndiyo imetoka.
 
Bora umeongea ukweli basi wapizani msisimamishe mgombea wa uraisi 2020
Kusimamisha mgombea ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu
 
Lowassa ameshasema nyie pigeni kura. Suala la kulinda kura tumwachie yeye
 
sasa kama malando atatangaza matokeo, kule zenji maalim atatangaza pia, NEC ya nini tena
 
its true the ground isn't fair enough for the opposition but the moment he was in systems hakuyaona hayo!?hawa wazee wanafiki sana
 
Huyu mzee anawachanganya tu UKAWA,hawajui wadai katiba mpya au tume.
Operesheni kata funua ilikuwa ije na mkakati wa kufanya vurugu nchi nzima,babu anawaambia wadai tume huru tu,waache kwanza katiba.
Hapa ndipo unaona akili ya wapinzani wa Tanzania ilivyo na urojo.Katiba pendekezwa walioapa kuipinga ina mambo ya tume huru na matokeo ya urais kuhojiwa lakini hawakujali hilo.
Bahati mbaya sana,awamu hii haina kipaumbele cha katiba wala tume huru,Wagome tu
 
Kama vyama vya upinzani havitadai tume huru ya uchaguzi hata mm siumizi kichwa kuchagua.tunafanyana watoto maana mshindi anajulikana hata kabla ya kura kwann niumize kichwa changu.sahivi wqmekaa kimya haf ikifika 2020 watasema wameibiwa kura.
 
Nyie ni watu sio mawe hivyo watu wanatakiwa kubadilika kutokana na wakati. Ni aibu mtu uliyesoma kumlaumu mtu eti mbona zamani alikuwa na msimamo ule na leo ana msimamo huu.
Mwanzilishi wa sheria ya muundo wa utawala wa Chama kimoja ni Mwalimu Nyerere, lakini ndiye huyohuyo aliye shinikiza kuwa sasa wakati umefika kuwa na vyama vingi. Mbona hamkumshangaa
hahahahah alishindikiza .au.alishindikizwa mkuu? ilkuwa.lazma mult party system iazishwe mkuu na sio nyerere
 
Huyu mzee si alikuwa kwenye bunge la katiba, wanazingua, waongee wengine si hawa
Huyu babu angekuwa anataka aheshimiwe kwa analoongea kama kina Warioba basi angelibakia neutral, lakini katika umri alionayo bado ni mtafutaji kwenye vyama vya siasa, kwa hapo kajishushia hadhi sana. Hakuna ataloongea kwa sasa watu wakamsikiliza. Ameshapitwa na wakati toka alivyopoteza busara ya kisiasa, ni wazi huyu ndie miongoni wa waliokuwa wakimpotosha Mwalimu.
 
"Kwa maoni yangu, kundi hili lililo madarakani bila shinikizo kubwa toka kwa wananchi hakuna mabadiliko" nukuu toka kwa Kingunge Ngombale Mwiru. Hapa nakubaliana na Mzee huyu 100% maana kelele zingine zinataka mabadiliko kwa hisani toka kwa kundi hili la CCM. Lazima shindikizo, vuguvugu, malumbano n.k kuwabana kundi hili la watawala.
 
Edo anasema TB JOSHUA kamwambia 2020 wanaingia Ikulu,yeye anasema WASAHAU kushinda uchaguzi,wataingiaje ikulu bila kushinda uchaguzi?au wataingia kunywa chai na kutoka?
wewe.una mwamini nani mkuu mtu wa Mungu au mtoa roho.watu?
 
kiongozi umemaliza kila kitu asante sana hakuna jipya hapo watu kama hawa ni wakupuuza kabisa ametumika miaka yote bila kusema chochote leo ndiyo anajifanya kuzungumzia agenda za tume huru na katiba utadhani hakuwepo madarakani aise hiki ni kituko cha kufungia mwaka
meno yote yameisha yupo.ccm na hakusema chochote ....nakumbuka horance kolimba alipo.sema ccm haina idra wala mwelekeo hui mzee alimwambia kolimba aende bungeni akaongee hayo maneno....
kilicho Mkuta sitaki.kusema.........

Leo hiiiii mzeee huyu. ......eti.....katba mpya ..duh au yesu kaludi....jamani?[emoji125]
 
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Kanu Kenya iliondoka bila katiba mpya, wala tume huru
 
Back
Top Bottom