Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli ya Kingunge imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Mbali na mwenyekiti kuteuliwa na Rais, wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ni wakurugenzi wa wilaya ambao pia huteuliwa na Rais kwa kuwa NEC haina wafanyakazi wake kote nchini.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

Kingunge, aliyetumia muda mrefu kueleza historia ya maisha yake katika siasa na jinsi alivyopambana katika harakati za kudai uhuru, alisema hali ya sasa ni mbaya kuliko wakati wa wakoloni wa Kiingereza ambao walikujwa wakali, kwa sababu CCM haifuati Katiba wala sheria.

“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.

Kingunge ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo ya waziri anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na mkuu wa mkoa alisema, “(Pia) Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana.”

Alisema pamoja na kwamba Chadema inapendwa na wananchi wengi na Edward Lowasa aliyegombea urais kwa tiketi chama hicho, anapendwa, bado ni vigumu kushinda kwa sababu mfumo uliopo sasa.

“Tufanye yoyote, lakini tuhakikishe, ama tunapata Katiba Mpya au vipengele hivi vya sheria vinafanyiwa marekebisho. Kwa maoni yangu, kundi hili lililo madarakani bila shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi, halitataka mabadiliko,” alisema.

Alisema enzi zao walifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitolea kwa nguvu na wengine, na yeye akiwamo, waliacha kazi za mishahara mikubwa na kujiunga na Tanu kupigania uhuru.

“Tulifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitoa mhanga. Wengi tu waliacha kazi, mtu anamaliza chuo kikuu anasema sitaki kazi anaingia Tanu kusaidia. Kwa hiyo tukawa na jeshi kubwa la vijana waliohakikisha nchi inapata uhuru,” alisema.

“Ninyi mnapambana katika mazingira magumu na wazee wenzenu walipambana katika mazingira hayo. Haikuwa rahisi. Wapo wengi walitusaliti, wengine hawakufanya lolote. Baba yangu tuligombana, nilipoacha kazi kwenda kuitumikia Tanu. Miezi sita hatukuzungumza.”

Akizungumza mkutano huo, Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwatia moyo vijana walioshtakiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, akisema bado jeshi kubwa la vijana linahitajika.

“Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Si haki kusema unakwenda mahali pengine, mwenzako amepasafisha, safisha pa kwako. Nimefurahia moyo huo. Kama alivyosema Ngombale, tunataka jeshi kubwa zaidi, watu wengi zaidi,” alisema Lowassa.
View attachment 449805
hata siku moja ichi ya kiafrika kiongozi haondoki madarakani kwa makaratasi...Mbona inasemekana Zanzibar Maalim Seif alishinda lakini uchaguzi ukafutwa.. Kifupi hata iwepo tume huru ya uchaguzi CCM haiwezi kuachia madaraka.. i.e hata uchaguzi ujao ikiwepo tume huru ya uchaguzi na upinzani ukashinda asilimia 90% uchaguzi utafutwa na CCM kwa kukingiwa kifua na jeshi... Mpinzani ataendelea kuwa mpinzani mpaka JESUS atakaporudi... OVERRRR..
 
Kadiri anavyozeeka ndio akili yake inazidi kua mbaya. eti huyu ndio alikua mkuu wa itikadi na propaganda ccm na tanu leo amekula matapishi yake hadi kavimbiwa.
Kama waipenda nchi yako, Toa maoni yako juu swala hili. Kuhama chama ni haki na hiyari na mtu mbinafsi. Kuwa chama tofauti ni hiyari na sio dhambi. Tujifunze kupingana bila kupigana.
 
Huwa nasikia aibu sana watu kama hawa wakiongea tena wakiwa upinzani.
hawa hawa ndo walitunyima katiba mpya.. ndo hawa hawa walimfanya jk abadili nia njema aliyokuwa nayo. aliipokea rasimu ya walioba kwa mikono miwili na kuikubali, wakakaa naye wakambadilisha.

Hawana maana kabisa, kingunge, sumaye, huwa nawaona kama wanaigizia huko upinzani. kidooogo lowasa huwa namuelewa.
 
heshima na adabu ni vitu vya bure. Unatakayeyotemlaumu Kingunge wewe umefanya nini kupigania na kusimamia nchi yako? kama wewe sio mzigo na hasara Tanzania wewe ni nani kuhoji,integrity ya mzee huyu?
Kama tunataka kuja kuongoza Tanzania lazima tuwe watu wafikra na sio utapiamlo kama wako na ujinga na uzandiki ulikuja kwa kupewa buku saba kumtukana mtu hakujui.
At the age of above 80 yrs ndo fikira za mabadiliko zianze kukuingia? Ni ngumu sana kuaminiwa na yeyote mwenye free mind. ingekuwa ni kumrudia Muumba kwenye umri huo pengine tungeamini kwamba ni hofu ya kifo, otherwise ni vigumu kuzuia watu wasiamini kwamba kale kawimbo walikomwimbia Kikwete kwenye NEC 'tunaimani na Lowasa' kalitungwa na Ngombale na kwa hivyo anasimamia asigeuke jiwe.
 
hata siku moja ichi ya kiafrika kiongozi haondoki madarakani kwa makaratasi...Mbona inasemekana Zanzibar Maalim Seif alishinda lakini uchaguzi ukafutwa.. Kifupi hata iwepo tume huru ya uchaguzi CCM haiwezi kuachia madaraka.. i.e hata uchaguzi ujao ikiwepo tume huru ya uchaguzi na upinzani ukashinda asilimia 90% uchaguzi utafutwa na CCM kwa kukingiwa kifua na jeshi... Mpinzani ataendelea kuwa mpinzani mpaka JESUS atakaporudi... OVERRRR..
ha ha ha... mkuu umefuatilia vizuri chaguzi za inch zote za Africa.. hujui kilichotokea Zambia, Nigeria Kenya.... au hizi inch ni za ulaya???
 
Namkumbuka sana huyu mzee wetu alivyokuwa anazungusha mikono juu ya jukwaa huku anasema mabadlikooooooo!

Alishasahau kwamba mabadiliko hayaji kwa kuzungusha mikono tu bali kwa kutoka jasho la damu ikibidi!! Swali linakuja hapa, jasho la damu analo[emoji1493][emoji1493]
 
Huyu mzee si alikuwa kwenye bunge la katiba, wanazingua, waongee wengine si hawa
Wote Sumaye, Lowassa, Mgeja, Kingunge, Makongoro et all" Manzi ga nyanza" hawafai kujifanya wanatetea haki ya Wanyonge kama wanavyodai maana walikuwa huko wanakodai hakufai!!
 
Bila tume huru ya uchaguzi! I will never vote again!
Mkuu, naomba tafsiri ya time huru ya uchaguzi, na ni sifa zipi zitajustfy kuwa hii ni time ya uchaguzi, ukiweza pendekeza na muundo Wa tume huru ya uchaguzi...

Ukijib hayo utanisaidia sana mkuu,
 
ha ha ha... mkuu umefuatilia vizuri chaguzi za inch zote za Africa.. hujui kilichotokea Zambia, Nigeria Kenya.... au hizi inch ni za ulaya???
Mkuu kwa utaalamu wa takwimu kama kuna wasichana 100 na wavulana 2... tunaweza kusema hatuna wavulana.. Hizo nchi za Africa viongozi/vyama waliokubali kuondoka madarakani kwa hiari ni wachache sana ... angalia mataifa waliotuzunguka viongozi wote wamegoma kuchomoka, MKUU kwa Tanzania wapinzani wataendelea kusugua benchi mpaka JESUS aje kuna viashiria vingi sana jaribu kutafakari kwa makini sana utapata jibu sahihi.....JIPIME KWANZA..
 
Mkuu, naomba tafsiri ya time huru ya uchaguzi, na ni sifa zipi zitajustfy kuwa hii ni time ya uchaguzi, ukiweza pendekeza na muundo Wa tume huru ya uchaguzi...

Ukijib hayo utanisaidia sana mkuu,

wajumbe wa tume wasiwe wateule wa rais
vyama viwe na uwakilishi kwenye tume
wajumbe wa tume wasiwe na wajibu wowote kwa rais
Bajeti ya tume isichezewe
 
Kingunge Ngomale Mwiru
Edward Ngoyai Lowasa
hawa ni mashujaa wa Taifa hili
Mungu awape afya na nguvu ili waendelee kutumia taifa lao
 
haka kazee kanafiki sana aisee, kamezaliwa, kamekulia, kameolea mpaka kamezeekea CCM na inasemekana kalikuwa na ushawishi mkubwa sana huko CCM. kalishindwa kushawishi hayo yafanyike, leo kamekaa pembeni na mapengo yake kanaanza kubwabwaja ujinga.

kama kalijua umuhimu wa tume huru, kwa nini hakakukomaa kipindi kapo CCM.? hivi vizee vya dizaini hizi ni vya hatari sana, pengine ukute hata ni kachawi. kalikuwa wapi siku zote hizo.? bora aseme mwingine sio haka jamani. mweeeeeh.!
 
Namkumbuka sana huyu mzee wetu alivyokuwa anazungusha mikono juu ya jukwaa huku anasema mabadlikooooooo!

Kiongozi unakumbukumbu sana,hata mimi namkumbuka sana yule aliyeahidi kilimo cha umwagiliaji wa ubuyu kule Singida,nashangaa kwa nini hajatekeleza ahadi yake hadi sasa.
 
Huyu mzee si alikuwa kwenye bunge la katiba, wanazingua, waongee wengine si hawa
HUYO babu anatudhihaki,mbona tulipolalama sana kutaka tume huru ya uchagui ndo walikuwapinzani kutetea tume ya chama kimoja,,ameona nini,wanajamvi
Anafanana na askari mmoja aliyepokea rushwa kwa dereva wa basi bovu,akaruhusu liendelee na safari akiwa mji mwingine,
huko mbele mama mzazi wake akapanda basi hilohilo,na mbele kidogo likapata ajali na kupinduka kwakukosa breki na mama yake akafari,sote twajua wa bunge ,wa bunge la katiba walifurahia masilahi ya ya vikao,wakatetea ubovu wakatiba ambao mwisho wa siku utawaumiza wao wenyewe,watoto wao na hata vizazi vijavyo tusipopamba kudai katiba mpya ambamo pia tumehuru ya uchaguzi imo,
 
haka kazee kanafiki sana aisee, kamezaliwa, kamekulia, kameolea mpaka kamezeekea CCM na inasemekana kalikuwa na ushawishi mkubwa sana huko CCM. kalishindwa kushawishi hayo yafanyike, leo kamekaa pembeni na mapengo yake kanaanza kubwabwaja ujinga.

kama kalijua umuhimu wa tume huru, kwa nini hakakukomaa kipindi kapo CCM.? hivi vizee vya dizaini hizi ni vya hatari sana, pengine ukute hata ni kachawi. kalikuwa wapi siku zote hizo.? bora aseme mwingine sio haka jamani. mweeeeeh.!
hapana ...we ndio unakosea...ukiwa kwenye taasisi flani inapaswa utetee msimamo ya hiyo taasisi...na ndicho alichokua alifanya ngombale...
 
HUYO babu anatudhihaki,mbona tulipolalama sana kutaka tume huru ya uchagui ndo walikuwapinzani kutetea tume ya chama kimoja,,ameona nini,wanajamvi
Anafanana na askari mmoja aliyepokea rushwa kwa dereva wa basi bovu,akaruhusu liendelee na safari akiwa mji mwingine,
huko mbele mama mzazi wake akapanda basi hilohilo,na mbele kidogo likapata ajali na kupinduka kwakukosa breki na mama yake akafari,sote twajua wa bunge ,wa bunge la katiba walifurahia masilahi ya ya vikao,wakatetea ubovu wakatiba ambao mwisho wa siku utawaumiza wao wenyewe,watoto wao na hata vizazi vijavyo tusipopamba kudai katiba mpya ambamo pia tumehuru ya uchaguzi imo,
tatizo hamuelewi Dhana ya collective responsibility
 
Back
Top Bottom