Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Huyo Kingunge alijua ni tatizo kwann wasingelimaliza wakati wakiwa ccm tena wakati huo yy na washirika wake wamekuwa ktk nyadhifa kubwa kabisa hapa nchini-kumbe ukiwa nje ya uwanja ndo unajidai kuwa na busara sana na kwa kuwa watawaliwa nao pia wanavitambaa vyeusi machoni pao na wasione kitu, kazi kubwa ni kupiga makofi pwa pwa pwa, na misifa kibao-sehemu yoyote ambayo hakuna uaminifu hata kama utachagua tume huru, bado wakishindwa watasema tume imehongwa-hata ukisema matokeo yapingwe mahakamani-bado watasema majaji wetu wamehongwa-cha msingi hapo ni kuaminiana kwa kila jambo. Kama hata Marekani ambao mifumo yao iko vizuri bado wanaamini kuibiana kura sembuse Tz, tuliona matokeo ya Kenya kuhojiwa mahakamani lakini kilichotokea ni kuruhusu Uhuru kuapishwa na kutupiliwa mbali madai ya Laila na wenzake pia hawakuridhika na maamuzi ya hiyo mahakama.
 
Ni mwanzilishi, mlezi, mtetezi, chief strategist & propagandist na think tank iliyozaa mfumo huu huu anaoulalamikia sasa. Amekula wee na kufaudu mumo kwa mumo wakampa ulaji pale stendi ya Ubungo yeye na wanae. Walipomnyang'anya tu huyooo akalamba hela za Eddo akageuza gia angani. Bunge la katiba JK anaichakachua katiba mpya laivu yuko kimyaaa leo hii ati ndiye mwanaharakati.
Wanasiasa wa Tanzania hawa wachumia tumbo tu na ni wachache sana ambao wameweka matakwa ya taifa mbele. Haiwezekani mtu utumikie mfumo ule ule kwa miaka 70 na jioni kabisa huku ndo ujifanye mwanaharakati. Hopeless kabisa!!!
Wenzetu husema "it is better late than never". Wangeangalia mbele wangeona lakini ukiwa mtawala unafikiria jinsi ya kuhadaa wapinzani wako unasau huenda siku moja ukawa mpinzani. EL, FS, KNM na Masha nao ni zamu yao kujua mabaya ya kile walichokua wanasimamia-safari hii tunaisoma wote namba lakini waliobaki huko CCM wasipoangalia iko siku zamu yao itafika. Bado namuunga mkono hata kama alichelewa.
 
HUYO babu anatudhihaki,mbona tulipolalama sana kutaka tume huru ya uchagui ndo walikuwapinzani kutetea tume ya chama kimoja,,ameona nini,wanajamvi
Anafanana na askari mmoja aliyepokea rushwa kwa dereva wa basi bovu,akaruhusu liendelee na safari akiwa mji mwingine,
huko mbele mama mzazi wake akapanda basi hilohilo,na mbele kidogo likapata ajali na kupinduka kwakukosa breki na mama yake akafari,sote twajua wa bunge ,wa bunge la katiba walifurahia masilahi ya ya vikao,wakatetea ubovu wakatiba ambao mwisho wa siku utawaumiza wao wenyewe,watoto wao na hata vizazi vijavyo tusipopamba kudai katiba mpya ambamo pia tumehuru ya uchaguzi imo,

isitoshe mpaka hivi majuzi tuu wakati wa bunge la katiba, wote hao EL, Sumaye, Kingunge walikuwa against UKAWA, nashindwa kuelewa hii nguvu wanaipata wapi.?

siasa za Tanzania ni za kinafiki sana na zenye kuangalia maslahi binafsi. halafu eti wanasiasa wanafiki wa aina hii ndo wanataka tuandamane tuvunjwe miguu kwa ajili yao, mi nasema hivi yeyote anayeingia madarakani ndo ninamuunga mkono.

wadhulumiane huko wawezavyo, yule mdhulumaji anayewazidi nguvu wadhulumaji wenzie mi ndio namuunga mkono, sitaki stress mie maisha yenyewe mafupi haya. akhaaaa.!
 
Ajenda kuu ya upinzani na hasa ukawa ni lazima iwe tume huru ya uchaguzi kama kweli tunataka haki yetu ya ushindi ilindwe
Kama tume si huru kivile hizo nafasi za ubunge zinapatikana kwa tume ipi? au kwa kuwa wataliwa tumefungwa vitambaa vyeusi machoni petu, wakati mwingine na cc tuwe tunatafakari pia, mbona ni rahisi sana hata kupata hiyo tume huru bila hata mgogoro ila kwa kuwa tamaa kubwa ni kwenda ikulu kwa hiyo zinatafutwa njia rahisi2 ili watu wafike ikulu -hivi tukiamua nguvu zote tukazielekeza kupata wabunge wa kutosha bila huo uraisi-hatujapata hiyo tume huru hatujapata hiyo katiba mpya? lakini kwa kuwa wanasiasa wanacheza na akili zetu wataliwa-basi tuendelee kucheza huo mziki wa kulalamika muda wote.
 
Kingunge yuko sahihi. Yaani hata ikiwa upinzani umepata kura 90% ya kiti cha urais ila tume ikisema mgombea wa ccm ndo ameshinda hakuna anayetakiwa kuhoji! Huo ni upuuzi kabisa. Sheria za enzi ya mfumo wa chama kimoja zitatumikaje kwenye mfumo wa sasa wa vyama vingi? Rais huyo huyo ndo mwenyekiti wa chama na huyo huyo ndo mgombea urais na ndo huyo huyo anateua mwenyekiti wa tume ambaye ndiye mtangaza matokeo ya urais! Kuna haja ya kwenda kupanga foleni eti unapiga kura?
 
Hawa wazee wanafiki sana,hawana hata aibu nyuso zao,walikwepo kwenye bunge la katiba,na ndio vyanzo vikuu vya kukwama,kwanza waondoke watuachie chadema yetu
 
Kwa nchi inayoongozwa na chama dora kama CCM ni ngumu sana upinzani kuchukua nchi. Nakubaliana na aliyoyasema Mzee Kayettan Ngobale Mwiru!!!!
Siku ambayo Tanzania itatengeneza katiba mpya na kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi basi CCM itaondoka madarakani mchana kweupe
 
Kingunge yuko sahihi. Yaani hata ikiwa upinzani umepata kura 90% ya kiti cha urais ila tume ikisema mgombea wa ccm ndo ameshinda hakuna anayetakiwa kuhoji! Huo ni upuuzi kabisa. Sheria za enzi ya mfumo wa chama kimoja zitatumikaje kwenye mfumo wa sasa wa vyama vingi? Rais huyo huyo ndo mwenyekiti wa chama na huyo huyo ndo mgombea urais na ndo huyo huyo anateua mwenyekiti wa tume ambaye ndiye mtangaza matokeo ya urais! Kuna haja ya kwenda kupanga foleni eti unapiga kura?
Sheria za kipuuzi kabisa matokeo ya uraisi huwezi kuhoji popote
 
Ni wakati muafaka kwa wapinzani kusimamia matakwa yetu wananchi kudai tume huru na katiba mpya.Bila tume huru na katiba mpya 2020 sitapiga kura kabisa na nitashangaa wapinzani kushiriki uchaguzi 2020 wakiwa na tume hii na katiba hii ya sasa.
Nakuunga mkono kabisa bila Tume huru ya Uchaguzi basi upinzani wasahau kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
 
hapana ...we ndio unakosea...ukiwa kwenye taasisi flani inapaswa utetee msimamo ya hiyo taasisi...na ndicho alichokua alifanya ngombale...
Hawa ndo wameturudisha nyuma sana wakiwa huko CCM
 
Hawa wazee wanafiki sana,hawana hata aibu nyuso zao,walikwepo kwenye bunge la katiba,na ndio vyanzo vikuu vya kukwama,kwanza waondoke watuachie chadema yetu
Hawa wakiwa huko CCM wametukwamisha mambo mengi sana leo wamehamia upinzani wanajifanya wana uchungu na Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi
 
Mkuu, naomba tafsiri ya time huru ya uchaguzi, na ni sifa zipi zitajustfy kuwa hii ni time ya uchaguzi, ukiweza pendekeza na muundo Wa tume huru ya uchaguzi...

Ukijib hayo utanisaidia sana mkuu,
Tume huru ni tume ambayo haiwezi kuingiliwa kwa vyovyote na mtu yeyote.Ni tume ambayo mwenyekiti wa tume anaajiriwa na kufanya interview na kuidhinishwa na bunge na kukubalika na pande zote na asiwe ni mwanachama wa chama chochote na asiwe mteule wa rais(Je waweza kwenda kinyume na mteule wako).Muundo wa tume iwe na wajumbe toka vyama vyote!!.Zanzibar pamoja na figisu zote tume yao kwa kiasi kikubwa ilikuwa huru!!!. Nafikiri umenipata vema!! Happy exmas and ny!!!!😉😉😉😉😉😀😀😀😀
 
64eb70c9fbf66f89dcd8f5fc1e18eaa3.jpg
Mkuu naona mabwana wanavyochangamkia chai bila hata itifaki,wanaiwahi chai kabla hata ya mwenyekiti!
 
UKAWA walikataa Rasimu Katiba Mpya iliyokuwa na Tume huru ya Uchaguzi kwa kuwa tu iliondolewa kipengele cha Serikali 3 ule ulikuwa ukosefu wa Ujanja wa kisiasa ambao Jakaya alitaka kuwaachia Zawadi
 

Salaam JF




Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli ya Kingunge imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Mbali na mwenyekiti kuteuliwa na Rais, wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ni wakurugenzi wa wilaya ambao pia huteuliwa na Rais kwa kuwa NEC haina wafanyakazi wake kote nchini.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

Kingunge, aliyetumia muda mrefu kueleza historia ya maisha yake katika siasa na jinsi alivyopambana katika harakati za kudai uhuru, alisema hali ya sasa ni mbaya kuliko wakati wa wakoloni wa Kiingereza ambao walikujwa wakali, kwa sababu CCM haifuati Katiba wala sheria.

“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.

Kingunge ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo ya waziri anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na mkuu wa mkoa alisema, “(Pia) Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana.”

Alisema pamoja na kwamba Chadema inapendwa na wananchi wengi na Edward Lowasa aliyegombea urais kwa tiketi chama hicho, anapendwa, bado ni vigumu kushinda kwa sababu mfumo uliopo sasa.

“Tufanye yoyote, lakini tuhakikishe, ama tunapata Katiba Mpya au vipengele hivi vya sheria vinafanyiwa marekebisho. Kwa maoni yangu, kundi hili lililo madarakani bila shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi, halitataka mabadiliko,” alisema.

Alisema enzi zao walifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitolea kwa nguvu na wengine, na yeye akiwamo, waliacha kazi za mishahara mikubwa na kujiunga na Tanu kupigania uhuru.

“Tulifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitoa mhanga. Wengi tu waliacha kazi, mtu anamaliza chuo kikuu anasema sitaki kazi anaingia Tanu kusaidia. Kwa hiyo tukawa na jeshi kubwa la vijana waliohakikisha nchi inapata uhuru,” alisema.

“Ninyi mnapambana katika mazingira magumu na wazee wenzenu walipambana katika mazingira hayo. Haikuwa rahisi. Wapo wengi walitusaliti, wengine hawakufanya lolote. Baba yangu tuligombana, nilipoacha kazi kwenda kuitumikia Tanu. Miezi sita hatukuzungumza.”


Akizungumza mkutano huo, Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwatia moyo vijana walioshtakiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, akisema bado jeshi kubwa la vijana linahitajika.

“Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Si haki kusema unakwenda mahali pengine, mwenzako amepasafisha, safisha pa kwako. Nimefurahia moyo huo. Kama alivyosema Ngombale, tunataka jeshi kubwa zaidi, watu wengi zaidi,” alisema Lowassa.

Chanzo: Mwananchi
 
Hicho ndicho nilichokuwa nakiota.refa asichaguliwe na rais.wala serikali isitoe fungu kuiendesha tume.
 
Mi sijui kwanini mwenyekiti (Aikaeli) yupo kimya kuhusu suala hili Kama kushinda opposition wanashinda ila hawatangazwi dawa ni TUME HURU YA UCHAGUZI na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom