Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wenzetu husema "it is better late than never". Wangeangalia mbele wangeona lakini ukiwa mtawala unafikiria jinsi ya kuhadaa wapinzani wako unasau huenda siku moja ukawa mpinzani. EL, FS, KNM na Masha nao ni zamu yao kujua mabaya ya kile walichokua wanasimamia-safari hii tunaisoma wote namba lakini waliobaki huko CCM wasipoangalia iko siku zamu yao itafika. Bado namuunga mkono hata kama alichelewa.Ni mwanzilishi, mlezi, mtetezi, chief strategist & propagandist na think tank iliyozaa mfumo huu huu anaoulalamikia sasa. Amekula wee na kufaudu mumo kwa mumo wakampa ulaji pale stendi ya Ubungo yeye na wanae. Walipomnyang'anya tu huyooo akalamba hela za Eddo akageuza gia angani. Bunge la katiba JK anaichakachua katiba mpya laivu yuko kimyaaa leo hii ati ndiye mwanaharakati.
Wanasiasa wa Tanzania hawa wachumia tumbo tu na ni wachache sana ambao wameweka matakwa ya taifa mbele. Haiwezekani mtu utumikie mfumo ule ule kwa miaka 70 na jioni kabisa huku ndo ujifanye mwanaharakati. Hopeless kabisa!!!
HUYO babu anatudhihaki,mbona tulipolalama sana kutaka tume huru ya uchagui ndo walikuwapinzani kutetea tume ya chama kimoja,,ameona nini,wanajamvi
Anafanana na askari mmoja aliyepokea rushwa kwa dereva wa basi bovu,akaruhusu liendelee na safari akiwa mji mwingine,
huko mbele mama mzazi wake akapanda basi hilohilo,na mbele kidogo likapata ajali na kupinduka kwakukosa breki na mama yake akafari,sote twajua wa bunge ,wa bunge la katiba walifurahia masilahi ya ya vikao,wakatetea ubovu wakatiba ambao mwisho wa siku utawaumiza wao wenyewe,watoto wao na hata vizazi vijavyo tusipopamba kudai katiba mpya ambamo pia tumehuru ya uchaguzi imo,
Kama tume si huru kivile hizo nafasi za ubunge zinapatikana kwa tume ipi? au kwa kuwa wataliwa tumefungwa vitambaa vyeusi machoni petu, wakati mwingine na cc tuwe tunatafakari pia, mbona ni rahisi sana hata kupata hiyo tume huru bila hata mgogoro ila kwa kuwa tamaa kubwa ni kwenda ikulu kwa hiyo zinatafutwa njia rahisi2 ili watu wafike ikulu -hivi tukiamua nguvu zote tukazielekeza kupata wabunge wa kutosha bila huo uraisi-hatujapata hiyo tume huru hatujapata hiyo katiba mpya? lakini kwa kuwa wanasiasa wanacheza na akili zetu wataliwa-basi tuendelee kucheza huo mziki wa kulalamika muda wote.Ajenda kuu ya upinzani na hasa ukawa ni lazima iwe tume huru ya uchaguzi kama kweli tunataka haki yetu ya ushindi ilindwe
Siku ambayo Tanzania itatengeneza katiba mpya na kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi basi CCM itaondoka madarakani mchana kweupeKwa nchi inayoongozwa na chama dora kama CCM ni ngumu sana upinzani kuchukua nchi. Nakubaliana na aliyoyasema Mzee Kayettan Ngobale Mwiru!!!!
Sheria za kipuuzi kabisa matokeo ya uraisi huwezi kuhoji popoteKingunge yuko sahihi. Yaani hata ikiwa upinzani umepata kura 90% ya kiti cha urais ila tume ikisema mgombea wa ccm ndo ameshinda hakuna anayetakiwa kuhoji! Huo ni upuuzi kabisa. Sheria za enzi ya mfumo wa chama kimoja zitatumikaje kwenye mfumo wa sasa wa vyama vingi? Rais huyo huyo ndo mwenyekiti wa chama na huyo huyo ndo mgombea urais na ndo huyo huyo anateua mwenyekiti wa tume ambaye ndiye mtangaza matokeo ya urais! Kuna haja ya kwenda kupanga foleni eti unapiga kura?
Nakuunga mkono kabisa bila Tume huru ya Uchaguzi basi upinzani wasahau kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020Ni wakati muafaka kwa wapinzani kusimamia matakwa yetu wananchi kudai tume huru na katiba mpya.Bila tume huru na katiba mpya 2020 sitapiga kura kabisa na nitashangaa wapinzani kushiriki uchaguzi 2020 wakiwa na tume hii na katiba hii ya sasa.
Hawa ndo wameturudisha nyuma sana wakiwa huko CCMhapana ...we ndio unakosea...ukiwa kwenye taasisi flani inapaswa utetee msimamo ya hiyo taasisi...na ndicho alichokua alifanya ngombale...
Hawa wakiwa huko CCM wametukwamisha mambo mengi sana leo wamehamia upinzani wanajifanya wana uchungu na Katiba mpya na Tume huru ya UchaguziHawa wazee wanafiki sana,hawana hata aibu nyuso zao,walikwepo kwenye bunge la katiba,na ndio vyanzo vikuu vya kukwama,kwanza waondoke watuachie chadema yetu
Tume huru ni tume ambayo haiwezi kuingiliwa kwa vyovyote na mtu yeyote.Ni tume ambayo mwenyekiti wa tume anaajiriwa na kufanya interview na kuidhinishwa na bunge na kukubalika na pande zote na asiwe ni mwanachama wa chama chochote na asiwe mteule wa rais(Je waweza kwenda kinyume na mteule wako).Muundo wa tume iwe na wajumbe toka vyama vyote!!.Zanzibar pamoja na figisu zote tume yao kwa kiasi kikubwa ilikuwa huru!!!. Nafikiri umenipata vema!! Happy exmas and ny!!!!😉😉😉😉😉😀😀😀😀Mkuu, naomba tafsiri ya time huru ya uchaguzi, na ni sifa zipi zitajustfy kuwa hii ni time ya uchaguzi, ukiweza pendekeza na muundo Wa tume huru ya uchaguzi...
Ukijib hayo utanisaidia sana mkuu,
Mkuu naona mabwana wanavyochangamkia chai bila hata itifaki,wanaiwahi chai kabla hata ya mwenyekiti!
