Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kwa nchi inayoongozwa na chama dora kama CCM ni ngumu sana upinzani kuchukua nchi. Nakubaliana na aliyoyasema Mzee Kayettan Ngobale Mwiru!!!!
 
Walio tunga katiba na yeye alikuwa mjumbe. Wapinzani walipo sema katiba mbovu yeye aliwapuuza Leo analalamika ajue anacho kilalamikia ndicho alicho kitengeneza bila kujua kesho yake itakuwaje? Tujue tunacho kiaanda Leo ndio matokeo ya kesho
Nyie ni watu sio mawe hivyo watu wanatakiwa kubadilika kutokana na wakati. Ni aibu mtu uliyesoma kumlaumu mtu eti mbona zamani alikuwa na msimamo ule na leo ana msimamo huu.
Mwanzilishi wa sheria ya muundo wa utawala wa Chama kimoja ni Mwalimu Nyerere, lakini ndiye huyohuyo aliye shinikiza kuwa sasa wakati umefika kuwa na vyama vingi. Mbona hamkumshangaa
 
Ni wakati muafaka kwa wapinzani kusimamia matakwa yetu wananchi kudai tume huru na katiba mpya.Bila tume huru na katiba mpya 2020 sitapiga kura kabisa na nitashangaa wapinzani kushiriki uchaguzi 2020 wakiwa na tume hii na katiba hii ya sasa.
 
Nilichokiona kuna makundi mawili huko, kuna wale wanaotaka uongozi kupitia chadema wakati sio wapenzi wa chadema, ndio maana huwa hawashiriki ata kwenye chaguzi za ndani, wao wanadili na vijana tu, regardless ni chadema au sio wanachadema kwa lengo moja tu , kupata ikulu na post za juu za nchi, na kundi la pili linalodili na internal affairs kuhakikisha wale wanajiita wafia chama wanaendelea kutawala chama, regardless ata mtu mmoja akishika vyeo kumi, ni ruhusa.
 
Hakuna point hapo mbona wakati yuko kule alipotoka akuyasema hayo mambo ya tume huru na katiba ina maana kipindi kile hakukua na vyama vya upinzani mwisho ni ndoto tena ya mchana kwa vyama vya upinzani kuchukua madaraka kwasababu kuna watu wana tamaa ya uongozi katika hivyo vyama vya upinzani awataki kuachia uenyekiti vyengine viko kifamilia mkwe na baba mkwe wako kibiashara zaidi wala siyo kiharakati
 
Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.
Kingunge kasahau kabisa walikuwa wanapambana na wakoloni. Hajui kuwa waliopo madarakani sasa ni walewale waliopambana na wakoloni wakawatoa. Sasa anataka kurudisha ukoloni? Anasema aligombana na baba yake, kwa nini hasemi kagombana na mwanaye kwa kufuata tamaa ya pesa?
 
Nilichokiona kuna makundi mawili huko, kuna wale wanaotaka uongozi kupitia chadema wakati sio wapenzi wa chadema, ndio maana huwa hawashiriki ata kwenye chaguzi za ndani, wao wanadili na vijana tu, regardless ni chadema au sio wanachadema kwa lengo moja tu , kupata ikulu na post za juu za nchi, na kundi la pili linalodili na internal affairs kuhakikisha wale wanajiita wafia chama wanaendelea kutawala chama, regardless ata mtu mmoja akishika vyeo kumi, ni ruhusa.

Na hakuna hata mmoja anayeifikiria Tanzania na watu wake....Opportunists
 
Wewe inaonekana hujitambui, ivi Kingunge katika yote aliyo ongea kuna ambalo alikua halifahamu kabla ya kuingia kwenye uchaguzi2015.Yeye na maMvi wote waroho wa madaraka. Kwakuwa maMvi au Kingunge wameshakua madarakani zaidi ya miaka 30 na katiyao hakuna hatammoja aliyeacha alama kamakiongozi wa watu kwamiakaiyo yote.

Labda wanachofanana ni ufisadi, maMvi alifukuzwa kwa aibu na kamati yabunge iliyoundwa kuchunguza sakata la richmond na Kingunge familia yake ndio iliyokuwa inakusanya kodi kwenye kituo cha mabasi Ubungo na maegesho ya magari hapa jijini DAR. Kwa watanzania wanao fahamu ao wakina maMvi na Kingunge wote tabia zao zinafanana na sasa wameungana na DJ ili kuendelea kulifilisi taifa.
 
Ila Lowassa strategist sana; kukaa na vijana hao ni kuwapa motisha kubwa ya kumpigania baadae.Tabia hii ndio iliyomfanya Lowassa asurvive kwa muda mrefu ndani ya CCM kwa sifa yake kubwa ya kumaintain friends.
 
Hakuna haja ya kupoteza muda, tume haipo huru afu unategemea nini
 
Huyu mzee si alikuwa kwenye bunge la katiba, wanazingua, waongee wengine si hawa
Ni mwanzilishi, mlezi, mtetezi, chief strategist & propagandist na think tank iliyozaa mfumo huu huu anaoulalamikia sasa. Amekula wee na kufaudu mumo kwa mumo wakampa ulaji pale stendi ya Ubungo yeye na wanae. Walipomnyang'anya tu huyooo akalamba hela za Eddo akageuza gia angani. Bunge la katiba JK anaichakachua katiba mpya laivu yuko kimyaaa leo hii ati ndiye mwanaharakati.

Wanasiasa wa Tanzania hawa wachumia tumbo tu na ni wachache sana ambao wameweka matakwa ya taifa mbele. Haiwezekani mtu utumikie mfumo ule ule kwa miaka 70 na jioni kabisa huku ndo ujifanye mwanaharakati. Hopeless kabisa!!!
 
Back
Top Bottom