Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Huyu Mzee hajawa mnafiki Kama wengi wanafiki wasiopenda Ukweli , kaamua kuanika ukweli japo anajua utawauma sana wale waliopindisha utaratibu na kufanya mambo kienyeji kisha kulazimisha watu wawaamini kuwa ni watenda Haki , Ukweli utabakia kuwa ukweli Hata Kama Mzee kingunge ataandamwa vipi ukweli utabakia hivyo hivyo ingawa ukweli unauma sana badala ya uongo ambao umeumiza wengi pia.
 
Kwakweli Warioba ni mfano wa kuigwa! Nilitegemea mzee Kingunge angejikita kuimarisha chama na kuondoa kero za katiba ya JMT!

Pole sana kwa mawazo yako mgando,leo hii ndio mnamuheshimu Mzee Warioba na kumuona Kingunge anazeeka vibaya,mmesahau mlivyomfanya Warioba kwenye mchakato wa Katiba Mpya?.

Mzee Kingunge yupo right kabisa na nashukuru sana Mungu mchakato huu wa Urais wa CCM unafanya tunaijua CCM ilivyo na pia ni Watu gani wanaoiharibu Nchi hii kwa maslai yao na familia zao. Muda mrefu tulikuwa tunasubiri ni nani atamfunga Paka[CCM] kengele kwa bahati Mzee Kingunge ameweza kumfunga Paka Kengele kwa kuongea yale walioshindwa watu wengi.

Sikatai Mzee Kingunge ana mapungufu yake kama Binadamu,lakini kwa hili tunapaswa tumuunge mkono sababu naamini huu ni mwanzo wa kuthubutu na hatimae kuwavuruga na kuliondoa hili Dubwasha CCM linalonyonya damu za wanyonge wa Tanzania. Big up Kingunge.
 
Ingeshangaza sana kama Kingunge angebaki bila kuliongelea hili!!
 
babu hivi haujui vikao halali vya kuongea mambo ya chama ndani ya chama?
je kama mzee unazani wazee wengine hawana cha kusema au wewe ndo uanjua zaidi?
umeanza kutumika kama wele wengine wenye recodi za kutumika?

babu kweli ndo maana hauna dini nazani mashetani yako ndo yalikuwa yanakuongoza,
Babu hatumiki wala havihitaji hivyo vikao kwani ndivyo vimefanya mambo ya Ajabu , babu kaamua kutokuwa Mnafiki kaamua kuanika Ukweli japo anajua wengi hawapendi Ukweli na watampinga sana lakini wajanja wamejua Ukweli ngoja wabishi waendelee kumkejeli .
 
Pole sana kwa mawazo yako mgando,leo hii ndio mnamuheshimu Mzee Warioba na kumuona Kingunge anazeeka vibaya,mmesahau mlivyomfanya Warioba kwenye mchakato wa Katiba Mpya?.

Mzee Kingunge yupo right kabisa na nashukuru sana Mungu mchakato huu wa Urais wa CCM unafanya tunaijua CCM ilivyo na pia ni Watu gani wanaoiharibu Nchi hii kwa maslai yao na familia zao.

Muda mrefu tulikuwa tunasubiri ni nani atamfunga Paka[CCM] kengele kwa bahati Mzee Kingunge ameweza kumfunga Paka Kengele kwa kuongea yale walioshindwa watu wengi.

Sikatai Mzee Kingunge ana mapungufu yake kama Binadamu,lakini kwa hili tunapaswa tumuunge mkono sababu naamini huu ni mwanzo wa kuthubutu na hatimae kuwavuruga na kuliondoa hili Dubwasha CCM linalonyonya damu za wanyonge wa Tanzania. Big up Kingunge.

Tanzania ni Nchi ya ajabu sana eti mtu akisema Ukweli anakuwa Adui ya wale waliokosolewa ? Hii ni ajabu sana badala ya kujifunza kupitia hayo mapungufu Yao wanakaa kumkejeli kingunge !

Kwa kweli nampongeza huyo Mzee kwa kusema ukweli japo najua watamwandama kwa mengi lakini nina imani Mungu atamlinda sana , Unafiki usipokemewa mapema utazidi kukuwa na huenda tukawa na wanafiki wengi Nchi ikaendelea kudumaa kimaendeleo.
 
Kingunge anajichanganya, kamati ya maadili inaandaa ripoti kwa ajili ya kamati kuu yes na ndo ilichofanya.

Inawezekana pia kamati kuu kutokana na muda wakaomba kamati ya maadili iwasaidie kuchuja makapi yote. na ndocho walichofanya.

Kingunge alitaka mambo yaende kwa shinikizo la kuhadaa kwa kutumia media kama anavoendelea kufanya. Haipendezi mtu mzima kama yy kushabikia kundi ndani ya chama tena kundi lenyewe sio la watu wasafi
 
Nchi hii ina idadi kubwa ya wanafiki kuliko Nchi yeyote Duniani na Unafiki huu ndiyo umekuwa kikwazo cha maendeleo , wapo watu hawataki kukosolewa Hata wakitenda mabaya hawataki kuambiwa ukweli , ukisema Ukweli unapata maadui wengi.

Kwa muundo huu wa kukumbatia Unafiki kamwe hatutapiga hatua, Mzee kingunge kuonyesha njia sasa ni Wakati wa kila mmoja kuacha Unafiki na kuzingatia taratibu zilizowekwa watu tuache mizengwe mizengwe kwani haitusaidii zaidi ya kuongeza watu wasiopiga kura .
 
Hakuna mwingine mwenye uwezo wa kuelezea udhaifu wa mfumo wa ccm na udhaifu wa wajumbe wake kama alivyofanya Mzee Kingunge.
Haya ni maandalizi tu ya safari maana hata safari yeneyewe haijaanza, njooni wenyewe ccm mtueleza na udhaifu wa mgombea wenu!

Mzee Kingunge, Katiba inayopendekezwa ni zao LA njama. Hukukemea wala kujali, badala yake mkacheza kiduku. Maoni ya wananchi yalipuuzwa nanyi akiwamo huyo El. Mfumo ule ule umekula kwenu, sijui mnamlilia nani? Kilio chenu hakina mashiko, hamtetei haki , mnatetea ufisadi. Mzee Kingunge wa Secretariat ya Propaganda hakuwa hivi. Sio siri kuwa Jua limekuchwea, kapumzike.
 
Tanzania ni Nchi ya ajabu sana eti mtu akisema Ukweli anakuwa Adui ya wale waliokosolewa ? Hii ni ajabu sana badala ya kujifunza kupitia hayo mapungufu Yao wanakaa kumkejeli kingunge ! Kwa kweli nampongeza huyo Mzee kwa kusema ukweli japo najua watamwandama kwa mengi lakini nina imani Mungu atamlinda sana , Unafiki usipokemewa mapema utazidi kukuwa na huenda tukawa na wanafiki wengi Nchi ikaendelea kudumaa kimaendeleo.

Yap,Mzee Kingunge amethubutu na ameweza kusema kile wengi walichokuwa wanaogopa. Ni kweli Mzee Kingunge alikengeuka kwenye mchakato wa Katiba Mpya lakini kwa hili nampongeza sababu anatusaidia kuliondoa hili dude tunalopiga vita Watanzani.
 
Kingunge anajichanganya, kamati ya maadili inaandaa ripoti kwa ajili ya kamati kuu yes na ndo ilichofanya. Inawezekana pia kamati kuu kutokana na muda wakaomba kamati ya maadili iwasaidie kuchuja makapi yote. na ndocho walichofanya. Kingunge alitaka mambo yaende kwa shinikizo la kuhadaa kwa kutumia media kama anavoendelea kufanya. Haipendezi mtu mzima kama yy kushabikia kundi ndani ya chama tena kundi lenyewe sio la watu wasafi

Membe na January hata magufuli wana usafi gani? Nani alipora Mali na mapesa ya Gadafi? Nani alimpora Sugu mladi wa maralia? Nani aliuza nyumba za serikali? Huyo mama migilo nini kilimtoa huko UN? Tambua kuwa ccm hakuna Msaafi wa kiasi cha kumnyooshea mwenzake kidole . Mchakato huu wa kuchuja ulichakachuliwa majina ya bilal na makongoro Nyerere yalikatwa kijanja yakapachikwa ya membe na January faster kienyeji ndiyo maana wajumbe waliwachinjilia mbali mapema, kubali ukatae kingunge kaongea ukweli mtupu japo ukweli utawauma sana, lakini Mzee amekataa kuwa Mnafiki .
 
Wapinzani wanavyolalamika Katiba ya nchi kuvunjwa kwa manufaa ya chama Tawala Kingunge hujawai kukemea.

Kanuni za Bunge zinapovunjwa wazi wazi kwa manufaa ya serikali ya ccm Kingunge hajawahi kukemea.

Polisi wanapovunja Sheria kwa kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tena vilivyofuata taratibu zote za kisheria Kingunge hajawahi kukemea.

Mahakama zinavyotoa hukumu kwa maslai ya chama Tawala Kingunge hajawahi kukemea.

NEC inapopendelea chama cha Ccm waziwazi na kukandamiza vyama vya upinzani Kingunge hajawahi kukemea.

Sasa leo yamemkuta mwenyewe sisi Watanzania wapenda Demokrasia tufanyeje ikiwa huko nyuma hakuwahi kuonyesha kuchukizwa na uvunjifu wa Katiba, sheria na Kanuni mbalimbali za kuongoza nchi.

Kingunge lazima ajue maumivu anayoyapata na kuyasikia kwa kuvunjwa kanuni za Chama chake ni zaidi ya maumivu wanayoyapata watanzania kwa kutofuata katiba na sheria za nchi kwa watawala.

Wewe unalia na Lowassa sisi tunalia na Tanzania yetu ya leo na ya baadae.

Wewe wamegusa maslai yako, sisi wanagusa maslai ya nchi.

Pole Mzee Kigunge, mlianza kwa kukiuka katiba ya nchi kwa kuruhusu mijadala bungeni kinyume cha kanuni za bunge leo yamewarudia mnapata mgombea wenu kinyume cha sheria na taratibu zenu.

Mwalimu alisema ; "ukianza kula nyama za watu huwezi kuacha Ona sasa mmeanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe.
 
Mzee Kingunge, Katiba inayopendekezwa ni zao LA njama. Hukukemea wala kujali, badala yake mkacheza kiduku. Maoni ya wananchi yalipuuzwa nanyi akiwamo huyo El. Mfumo ule ule umekula kwenu, sijui mnamlilia nani? Kilio chenu hakina mashiko, hamtetei haki , mnatetea ufisadi. Mzee Kingunge wa Secretariat ya Propaganda hakuwa hivi. Sio siri kuwa Jua limekuchwea, kapumzike.
Kingunge hamlilii mtu wala hataki chochote yeye alichofanya ni kuanika ukweli ili watu wajue na kujifunza kuwa Hata cc huwa kuna magumashi na hii ndiyo imepelekea Nchi hii kutoendelea miaka yote, Ukweli unauma sana, lakini wenye Akili zao hautawauma bali watautumia kama somo kujifunza kupitia hayo mapungufu .
 
Wapinzani wanavyolalamika Katiba ya nchi kuvunjwa kwa manufaa ya chama Tawala Kingunge hujawai kukemea.

Kanuni za Bunge zinapovunjwa wazi wazi kwa manufaa ya serikali ya ccm Kingunge hajawahi kukemea.

Polisi wanapovunja Sheria kwa kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tena vilivyofuata taratibu zote za kisheria Kingunge hajawahi kukemea.

Mahakama zinavyotoa hukumu kwa maslai ya chama Tawala Kingunge hajawahi kukemea.

NEC inapopendelea chama cha Ccm waziwazi na kukandamiza vyama vya upinzani Kingunge hajawahi kukemea.

Sasa leo yamemkuta mwenyewe sisi Watanzania wapenda Demokrasia tufanyeje ikiwa huko nyuma hakuwahi kuonyesha kuchukizwa na uvunjifu wa Katiba, sheria na Kanuni mbalimbali za kuongoza nchi.

Kingunge lazima ajue maumivu anayoyapata na kuyasikia kwa kuvunjwa kanuni za Chama chake ni zaidi ya maumivu wanayoyapata watanzania kwa kutofuata katiba na sheria za nchi kwa watawala.

Wewe unalia na Lowassa sisi tunalia na Tanzania yetu ya leo na ya baadae.

Wewe wamegusa maslai yako, sisi wanagusa maslai ya nchi.

Pole Mzee Kigunge, mlianza kwa kukiuka katiba ya nchi kwa kuruhusu mijadala bungeni kinyume cha kanuni za bunge leo yamewarudia mnapata mgombea wenu kinyume cha sheria na taratibu zenu.

Mwalimu alisema ; "ukianza kula nyama za watu huwezi kuacha Ona sasa mmeanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe.
Ni kweli unachosema lakini nadhani sasa Mzee kingunge atakuwa anajutia hilo ndiyo maana kaamua kujivua Gamba la UNAFIKI kaanika ukweli ambao nadhani utazua Gumzo weekend yote hii,
 
Okei, huyu babu yawezekana kuna kitu anakijua ambacho sisi raia hatukijui.

yeah, umenena kitu, na ndiyo maana amesema "Lowasa SI fisadi kama tunavyofikiria" Mimi naona alijiuzulu baada ya kubembelezwa ajiuzulu kwa maslah ya chama maana angesema ukweli CCM ingekuwa kwishney ila ipo siku ataweka wazi
 
Kingunge ameamua kusema Ukweli na ukweli pekee ndio unaweza kuwaweka huru wanaCCM. Japokuwa simuungi Mkono Lowassa lakini hakutendewa haki kabisa.

Kama kweli Lowassa na wenzake wenye nguvu na ushawishi ndani ya CCM waliokuwa wanagombea walikuwa hawafai, ilikuwa ni busara sana kuwapa nafasi wajumbe wa Kamati kuu, Halmashauri Kuu au Mkutano Mkuu kuamua hilo na sio kuwakata majina yao kwenye kamati ya Maadili kinyume kabisa na kanuni, taratibu na Katiba ya CCM.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Kwani nin maana ya kamati ya maadili?tena kama wewe ni mwana CCM ishukuru sana hiyo kamati coz kama ingempitisha EL the demise of CCM would be around the corner
 
Mchakato kuwa batili; kingunge kusema ukweli, vyote bure. Hapa ni habari ya "mbwa kala mbwa". Si CCM wala kingunge anayetuletea la maana. Wanafiki wamezidiana kete, period.
 
Hahahahaha!!
Mi naomba Mzee Kingunge uwaambie wale waliokuwa wanawasukuma pasipo nyie kujua mnasukumiwa wapi mkazama na kuingia waZima wazima kwamba WALIKOSEA TIMING"
 
Back
Top Bottom