Kama wenyewe hawajitendei haki unadhani watatenda haki kwa wengine jiulize! !?
Mkuu hapa umenena haya ni maneno mazito ni lazima watz nao walitambue hili....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama wenyewe hawajitendei haki unadhani watatenda haki kwa wengine jiulize! !?
Kingunge ameamua kusema Ukweli na ukweli pekee ndio unaweza kuwaweka huru wanaCCM. Japokuwa simuungi Mkono Lowassa lakini hakutendewa haki kabisa.
Kama kweli Lowassa na wenzake wenye nguvu na ushawishi ndani ya CCM waliokuwa wanagombea walikuwa hawafai, ilikuwa ni busara sana kuwapa nafasi wajumbe wa Kamati kuu, Halmashauri Kuu au Mkutano Mkuu kuamua hilo na sio kuwakata majina yao kwenye kamati ya Maadili kinyume kabisa na kanuni, taratibu na Katiba ya CCM.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
na sasa hivi wamemkimbia mzee wa watu....wakati ule angekuwa amezungukwa kila kona
![]()
Mnao mdharau Mzee Kingunge hamjui kitu na mpo kama bendera fuata upepo! Kingunge ni mzee makini sana na mnaofurahia jambo hili mtakuja jutia siku moja!
Hakunaaaaaaa!! #$!&@#×®©=+
Hicho mnachokiita KITENGO kilifanya what had to be done kwa maslahi ya CHAMA.
Msifumbie macho mikakati miovu ya EL na genge lake hasa kipindi hiki cha kuomba udhamini.
Wametembeza hela.
Tunakaa na watu wanaotusimulia namna hela yao ilivyopotea kwa jina la EL kukatwa...msijifanye hamuoni hilo.
Tusijifanye pia kuwa tumesahau uchaguzi wa CCM wa 2012 ulijaa rushwa na kupanga timu.
Huku Kamati kuu, NEC na Mkutano mkuu pesa ilishatembea.
Viongozi si wapuuzi wapeleke jina huko tayari watu walishanunuliwa!!!
Genge hili lilisha-manupulate mfumo uliopo, zikiwemo kanuni kwa pesa ndio maana walikuwa na jeuri ya kudai hawaoni wa kukata jina-limekatwa sasa kwa maslahi ya CHAMA!!!
Cha msingi tunachopaswa kujifunza toka Dodoma sio kulilia ukatwaji wa watu; cha msingi ni kujifunza kuwa kuna wakati inabidi kufanya lolote kunusuru.
CCM baada ya miaka mingi imetoa mgombea ambae hakununua uongozi na hilo ndio muhimu...Wote mnaolia, pamoja na Kingunge mkumbushwe uongozi haununuliwi!!!!
Kama mtu huyo ana uwezo kama mnaodai, hapakuwa na sababu ya kutumia hela zote zile kumnadi kuchukua tu fomu...pesa hizo wakati hospitali wajawazito wanalala chini!!!
Umefika wakati muwe wazalendo
Makubwa haya, sasa ni dhahiri CCM vipande vipande.
Kwa hiyo huko CCM Fisadi ni Lowasa peke yake ni watu wangapi tunasikia tetesi zao kama anavyochafuliwa Lowasa peke yake bila ushahidi wowote kuwa wamekwapua hiki na kile kuanzia Mkuu wa Kaya mpaka mawaziri wake lakini hatusikii wakiimbwa kama EL?Pinda hajawa na kashfa ya Sukari,Mkulu hajatajwa kwenye Escrow,Membe hajatajwa kwenye kashfa ya Libya,Magufuli hajatajwa kwenye kashfa ya Nyumba pamoja na wizara yake?kama ni hivyo inakuwaje leo hii aonekane Lowasa ndio dampo la kila baya la Nchi hii,umesema kwenye mchakato wa udhamini amenunua watu,je una ushahidi gani au kisa alikuwa anapata watu wengi kuliko wenzake?. Acheni unafiki,kila mtu alifanya rafu kuanzia familia kuu kumbeba mtu mmoja mpaka kuhonga watu hela,kilichotakiwa ni usawa na haki kwa kila mgombea na ndicho Mzee Kingunge analia nacho.

Mmmh kumbe walioumia ni wengi aseee, poleni bana ndio hivyo.
Lakini mbona mnalalamika wakati jamaa ni mtu wa maamuz magumu????
Halafu imekuaje amekatwa wakati alishasema hakuna wakumkata!!!!!
Mh hatari
Namshauri huyu Mzee (Dingi) akapumzike, yeye na Lowasa ni mafisadi hivyo wanaelea chombo kimoja baharini, wanalindana. Eti huyu alikuwa mfuasi wa Nyerere kiasi cha kutoamini dini yoyote. Wanahabari walipaswa kumuuliza juu ya ufisadi mkubwa alioufanya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, tena kwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Aende zake kaishiwa cha kuongea.