Kwakweli Warioba ni mfano wa kuigwa! Nilitegemea mzee Kingunge angejikita kuimarisha chama na kuondoa kero za katiba ya JMT!
Babu hatumiki wala havihitaji hivyo vikao kwani ndivyo vimefanya mambo ya Ajabu , babu kaamua kutokuwa Mnafiki kaamua kuanika Ukweli japo anajua wengi hawapendi Ukweli na watampinga sana lakini wajanja wamejua Ukweli ngoja wabishi waendelee kumkejeli .babu hivi haujui vikao halali vya kuongea mambo ya chama ndani ya chama?
je kama mzee unazani wazee wengine hawana cha kusema au wewe ndo uanjua zaidi?
umeanza kutumika kama wele wengine wenye recodi za kutumika?
babu kweli ndo maana hauna dini nazani mashetani yako ndo yalikuwa yanakuongoza,
Pole sana kwa mawazo yako mgando,leo hii ndio mnamuheshimu Mzee Warioba na kumuona Kingunge anazeeka vibaya,mmesahau mlivyomfanya Warioba kwenye mchakato wa Katiba Mpya?.
Mzee Kingunge yupo right kabisa na nashukuru sana Mungu mchakato huu wa Urais wa CCM unafanya tunaijua CCM ilivyo na pia ni Watu gani wanaoiharibu Nchi hii kwa maslai yao na familia zao.
Muda mrefu tulikuwa tunasubiri ni nani atamfunga Paka[CCM] kengele kwa bahati Mzee Kingunge ameweza kumfunga Paka Kengele kwa kuongea yale walioshindwa watu wengi.
Sikatai Mzee Kingunge ana mapungufu yake kama Binadamu,lakini kwa hili tunapaswa tumuunge mkono sababu naamini huu ni mwanzo wa kuthubutu na hatimae kuwavuruga na kuliondoa hili Dubwasha CCM linalonyonya damu za wanyonge wa Tanzania. Big up Kingunge.
Hakuna mwingine mwenye uwezo wa kuelezea udhaifu wa mfumo wa ccm na udhaifu wa wajumbe wake kama alivyofanya Mzee Kingunge.
Haya ni maandalizi tu ya safari maana hata safari yeneyewe haijaanza, njooni wenyewe ccm mtueleza na udhaifu wa mgombea wenu!
Tanzania ni Nchi ya ajabu sana eti mtu akisema Ukweli anakuwa Adui ya wale waliokosolewa ? Hii ni ajabu sana badala ya kujifunza kupitia hayo mapungufu Yao wanakaa kumkejeli kingunge ! Kwa kweli nampongeza huyo Mzee kwa kusema ukweli japo najua watamwandama kwa mengi lakini nina imani Mungu atamlinda sana , Unafiki usipokemewa mapema utazidi kukuwa na huenda tukawa na wanafiki wengi Nchi ikaendelea kudumaa kimaendeleo.
Kingunge anajichanganya, kamati ya maadili inaandaa ripoti kwa ajili ya kamati kuu yes na ndo ilichofanya. Inawezekana pia kamati kuu kutokana na muda wakaomba kamati ya maadili iwasaidie kuchuja makapi yote. na ndocho walichofanya. Kingunge alitaka mambo yaende kwa shinikizo la kuhadaa kwa kutumia media kama anavoendelea kufanya. Haipendezi mtu mzima kama yy kushabikia kundi ndani ya chama tena kundi lenyewe sio la watu wasafi
Kingunge hamlilii mtu wala hataki chochote yeye alichofanya ni kuanika ukweli ili watu wajue na kujifunza kuwa Hata cc huwa kuna magumashi na hii ndiyo imepelekea Nchi hii kutoendelea miaka yote, Ukweli unauma sana, lakini wenye Akili zao hautawauma bali watautumia kama somo kujifunza kupitia hayo mapungufu .Mzee Kingunge, Katiba inayopendekezwa ni zao LA njama. Hukukemea wala kujali, badala yake mkacheza kiduku. Maoni ya wananchi yalipuuzwa nanyi akiwamo huyo El. Mfumo ule ule umekula kwenu, sijui mnamlilia nani? Kilio chenu hakina mashiko, hamtetei haki , mnatetea ufisadi. Mzee Kingunge wa Secretariat ya Propaganda hakuwa hivi. Sio siri kuwa Jua limekuchwea, kapumzike.
Ni kweli unachosema lakini nadhani sasa Mzee kingunge atakuwa anajutia hilo ndiyo maana kaamua kujivua Gamba la UNAFIKI kaanika ukweli ambao nadhani utazua Gumzo weekend yote hii,Wapinzani wanavyolalamika Katiba ya nchi kuvunjwa kwa manufaa ya chama Tawala Kingunge hujawai kukemea.
Kanuni za Bunge zinapovunjwa wazi wazi kwa manufaa ya serikali ya ccm Kingunge hajawahi kukemea.
Polisi wanapovunja Sheria kwa kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tena vilivyofuata taratibu zote za kisheria Kingunge hajawahi kukemea.
Mahakama zinavyotoa hukumu kwa maslai ya chama Tawala Kingunge hajawahi kukemea.
NEC inapopendelea chama cha Ccm waziwazi na kukandamiza vyama vya upinzani Kingunge hajawahi kukemea.
Sasa leo yamemkuta mwenyewe sisi Watanzania wapenda Demokrasia tufanyeje ikiwa huko nyuma hakuwahi kuonyesha kuchukizwa na uvunjifu wa Katiba, sheria na Kanuni mbalimbali za kuongoza nchi.
Kingunge lazima ajue maumivu anayoyapata na kuyasikia kwa kuvunjwa kanuni za Chama chake ni zaidi ya maumivu wanayoyapata watanzania kwa kutofuata katiba na sheria za nchi kwa watawala.
Wewe unalia na Lowassa sisi tunalia na Tanzania yetu ya leo na ya baadae.
Wewe wamegusa maslai yako, sisi wanagusa maslai ya nchi.
Pole Mzee Kigunge, mlianza kwa kukiuka katiba ya nchi kwa kuruhusu mijadala bungeni kinyume cha kanuni za bunge leo yamewarudia mnapata mgombea wenu kinyume cha sheria na taratibu zenu.
Mwalimu alisema ; "ukianza kula nyama za watu huwezi kuacha Ona sasa mmeanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe.
Okei, huyu babu yawezekana kuna kitu anakijua ambacho sisi raia hatukijui.
Kwani nin maana ya kamati ya maadili?tena kama wewe ni mwana CCM ishukuru sana hiyo kamati coz kama ingempitisha EL the demise of CCM would be around the cornerKingunge ameamua kusema Ukweli na ukweli pekee ndio unaweza kuwaweka huru wanaCCM. Japokuwa simuungi Mkono Lowassa lakini hakutendewa haki kabisa.
Kama kweli Lowassa na wenzake wenye nguvu na ushawishi ndani ya CCM waliokuwa wanagombea walikuwa hawafai, ilikuwa ni busara sana kuwapa nafasi wajumbe wa Kamati kuu, Halmashauri Kuu au Mkutano Mkuu kuamua hilo na sio kuwakata majina yao kwenye kamati ya Maadili kinyume kabisa na kanuni, taratibu na Katiba ya CCM.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.