Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge wachane maccm yanaonea watu.Ccm wamezoea magoli ya mikono leo msikubali pambana mpaka Lowasa apate haki yake.ccm ni mafisadi na wadhurumu haki

Nape alipenyeza Goli la mkono kwa kula njama majina ya makongoro Nyerere na bilali yakaondokewa top 5 kienyeji wakapachika Membe na January ili awape Goli la mkono lakini wajumbe wakawaumbua, Nape kahamia Kwa Magufuli kinafiki tu lakini halikuwa Chaguo lake.
 
Najua Nape atasema mzee kafilisika kisiasa

Majibu ya Nape hata Kama yatatoka mbinguni Kwa Mungu hakuna kwenye Akili zake atayaamini , kwani Nape anajulika yupo Kwa magufuli kinafiki tu baada ya Chaguo lake Membe kutupwa vibaya licha ya kujaribu kumpa Goli la mkono Kwa kulikata jina la makongoro Nyerere akampachika kienyeji , Mzee kingunge kasema Ukweli Hata nape aje na majibu gani Ukweli utabakia kuwa kweli .
 
yaan Leo ningekuwa mm n lowasa ningehama chama yaan hakuna dhambi mbaya kama uwoga

Lowasa hana haraka ya kuhama chama ametulia kwanza atafakari Kwa kiina magumashi aliyofanyiwa na cc , huku watanzania nao wakitathimini mapungufu ya mchakato mzima ulivyokwenda . Kingunge kaanika Ukweli sasa ni jukumu la wapenda Haki kulitizama hilo Kwa jicho la tatu.
 
Kingunge anajichanganya, kamati ya maadili inaandaa ripoti kwa ajili ya kamati kuu yes na ndo ilichofanya.

Inawezekana pia kamati kuu kutokana na muda wakaomba kamati ya maadili iwasaidie kuchuja makapi yote. na ndocho walichofanya.

Kingunge alitaka mambo yaende kwa shinikizo la kuhadaa kwa kutumia media kama anavoendelea kufanya. Haipendezi mtu mzima kama yy kushabikia kundi ndani ya chama tena kundi lenyewe sio la watu wasafi

Hizo ni hisia na mawazo yako. Taratibu zao hazisemi hivyo!
Tukubali tu kuwa maneno ya mzee Kingunge ni facts. Hata hivyo namshangaa, ubatili huu ulikuwepo tangu Bunge la Katiba ila yeye alikaa kimya, nae huyu mzee ni walewale. Sioni tofauti ubatili huu ausemao leo kuhusu mchakato wa kumpata mgombea na ubatili ule wa kupata Katiba inayopendekezwa. Zote ni batili kwa maana kutofuatwa taratibu sahihi. Waandishi wa habar walitakiwa wamuulize kuhusu hilo, hili limemuumiza kwa kuwa alikuwa na maslahi nalo. La katiba ameona ni sawa, nae ni mnafiki pia!
 
Mzeee wachane pambana.Goli la mkono usikubali kuchakachuliwa
 
Wale wote 38 waliokatwa majina Yao wanalalamika chini chini lakini wengi ni wanafiki sana, wanaogopa kulalamika Kwa uwazi wakihofia kukosa Vyeo , Ubunge na Uwaziri kwenye Serikali ijayo ya magufuli , Unafiki ni sumu kubwa na cha Ajabu hapa Tanzania Msema Ukweli huwa Adui lakini Msema uongo na mpenda magumashi huwa rafiki wa wengi, Mzee kingunge kasema Ukweli na habari ndiyo hiyoo asiyekubali atabakia kuwa Mnafiki milele.
 
Hizo ni hisia na mawazo yako. Taratibu zao hazisemi hivyo!
Tukubali tu kuwa maneno ya mzee Kingunge ni facts. Hata hivyo namshangaa, ubatili huu ulikuwepo tangu Bunge la Katiba ila yeye alikaa kimya, nae huyu mzee ni walewale. Sioni tofauti ubatili huu ausemao leo kuhusu mchakato wa kumpata mgombea na ubatili ule wa kupata Katiba inayopendekezwa. Zote ni batili kwa maana kutofuatwa taratibu sahihi. Waandishi wa habar walitakiwa wamuulize kuhusu hilo, hili limemuumiza kwa kuwa alikuwa na maslahi nalo. La katiba ameona ni sawa, nae ni mnafiki pia!

Kaamua kusitaafu unafiki kajiludi na kuamua kuweka uwazi na Ukweli ili watu wapate Somo.
 
Mchakato kuwa batili; kingunge kusema ukweli, vyote bure. Hapa ni habari ya "mbwa kala mbwa". Si CCM wala kingunge anayetuletea la maana. Wanafiki wamezidiana kete, period.
 
Ukiachilia mbali mahaba ya Kingunge kwa Lowassa na sababu zake za utetezi ambazo sizo at least kwa dhana aliyojengewa mgombea wake na kushindwa kujitofautisha yeye mwenyewe ndio kabisa; wachina wanamsemo wao bora ukae kimya wakufikirie mpumbavu, kuliko kufungua mdomo wako na kuwthibitishia upumbafu wako. Timu ya Lowassa kuelekea uchaguzi ndio imetufanya wengi kukubali tuhuma zinazotolewa juu yake, binafsi nimeshangaa kuona Karamagi bado anaingia NEC.

Having said that bado hoja yake ya mchakato ulivyoenda ndivyo-sivyo inabaki ni ya msingi sana ndani ya chama chao na inabidi wakae wafikirie wakikutana wanasawazisha vipi kwenda mbele. Kanuni na sheria zipo kwa sababu ya maelekezo ya ufanyaji mambo na uwezi badilisha kwa manufaa yako things dont work that way or else utazua migogoro tu na watu wa nje kuwaombea hiyo migogoro ijitokeze kwa faida yao.

Hakuna kipindi kigumu kwenye chama chochote cha siasa duniani kama wakati wa kubadili leadership ya juu, kazi yote ya kamati ya maadili, sijui whips huko dunia zingine wanavyoitana ni kuhakikisha chama kinabaki salama kipindi kama hiki maana makundi ayakosekani.

CCM mbona kasheshe lake dogo sana kipindi hiki kulinganisha na migogoro inayozuka China tofauti yao na CCM labda wao wakishaamua huyu ndio wetu kama ukileta ukaidi awasubiri muda wa kuchagua kiongozi ufike uyumbishe chama chenye wanachama zaidi ya millino saba hiyo kamati yao ya maadili inaanza na wewe kabla awajafikia hatua hizo.

Lowassa na Apson nawafananisha na 'Bo Xilai' ambaye alikuwa ni challenger 'Xi Jinping' na 'Zou Yongkang' ex spy no suprises kwa sababu ya utawala wa vyama vya kijamaa. Na issue ni hii hii Sura ya chama jamaa walivyoleta ukaidi wala hakuna haja ya kukatana wakijua wanasupport ya wanachama wanaweza leta migogoro 'Bo Xilai' anaozea jela sasa hivi na mkewe ana suspended death sentences; huyo wausalaa walimvutia muda na yeye sasa hivi lupango makosa yao ushahid wa ufisadi wa zamani.

Chama akiwezi tishiwa nyau na makada wake ndio maana kuna kamati za maadili ambazo kazi yake ni kuhakikisha wanachama wanaowania nafasi za juu wanasifa sahihi na vision sahihi na kuna muda mrefu sana wakufikia hatua za kufikirwa kutokana na groomed procedure na mafanikio yako sio tu kwenye kufanya kazi bali uwezo wako wa kukiunganisha chama na wanachama wakisema huyu ni kuwa ana tick all the boxes sio tu hana makundi ndani ya chama.

Huu mchakato uligubikwa na majungu, poor succession planning ambayo aijulikani nani anafaa kwa sifa zipi kutokana na mahitaji ya watanzania na kukijenga chama, binafsi nina mashaka sana na uwezo wa Magufuli kama raisi nilitegemea zaidi ya uchapakazi bali vision pia.

In short the whole thing and several part machines needs services na Kingunge anaposema muundo wa chama umewekwa majaribuni nakubaliana naye kabisa. Way forward ni kuacha kufanya vitu kwa mazoea tu ya kuendesha nchi na previlege za usalama walizonazo hila CCM inabidi ijipange upya na iangalie safu yake ikibidi watu kama kina Wilson Mkama warudi tu kama awapo kwa sasa bado skills zao zinahitajika na kupanga safu mpya yenye mawazo mapya kwa sasa hawa watu wengi wafanya maamuzi na strategists are weak na namna alivyoenguliwa Lowassa sio ingawa end justifies the means that the only justification of the their wrong doings.

Maandishi yako yooootee hayawez kuondoa ukweli wa alichokisema mzee Kingunge. Hayo mambo ya kiimla ya China hayatuhusu hapa kwetu. Sisi tuna sheria zetu tofauti na za China. China ukila rushwa unatwangwa risasi, hapa kwetu unafungwa, fine au hata kudunda mitaani. Hivyo hayo mambo ya Kichina hayatuhusu, ukweli wa mzee Kingunge hakuna hata mmoja ataweza kuukanusha. Mzee huyu anakuwa mtu wa Tano katika watu waliopinga mchakato ulivyoendeshwa:-
1.Dr Nchimbi
2.Mama Sophie Simba
3.Kimbisa
4.Dr Kakokola
5.Mzee Kingunge

Watu hawa wote hawawez kuwa waongo!
 
Lowasa wetu tunamtaka,Pombe ni wa mfukoni kwa wazeee tumewekewa boya la kikwete hatutaki
 
Mropokaji hatumtaki.Mgombea wa mfukoni kwa kikwete hapana.Magufuliss big no
 
Hongera mzee Kingunge kwa kuwa katika ubora wako wa enzi zile za chama kushika hatamu. Nakusifu kwa kuzienzi zile ahadi za mwana TANU za kuusema ukweli daima. Ni kweli kamati ya maadili ilipoka mamlaka na madaraka ya NEC na kunyima haki ya kuwasikiliza wagombea. Haki haikuwepo zaidi ya kuburuzana. EL usife moyo ikimbie ccm kwani si mama yako useme utampata wapi mwingine. Kuwa mzalendo kwa kutoa mchango wako kivingine ili kuwaletea wananchi maendeleo. Hongera tena Kingunge kwa kutuweka wazi.
 
Yap, haiwez ikasababisha uhalali wa kilichotokea huko Dodoma hata kama yeye naye ni batili!
ivi ni lazima lowasa ndio awe raisi wa Tanzania? kwanini mapovu yanawatoka kwa ajili ya Lowasa tu? mbona wengine wamekaa kimya? ivi mmesahau hkuwa hata kikwete alifanyiwa ivi na alaikubali matokeao? huyu babu anazeeka vibaya na vijisenti anavopewa vinamchanganya sana. yampasa kuwa mshauri na sio kuwa sehemu ya makundi yanayo kitafuna chama. hakuna mtu mwenye hati miliki ya tanzania na wala Lowasa hakuzaliwa ili awe raisi wa wa tanzania.
 
Alikuwa wapi asiongee wakati wa mchakato kule Chimwaga, aje kuongea baada ya Magufuli kuteuliwa?

Hana lolote. Mnafiki tu.
 
Team Magufuli wajipange.
Safari ya matumaini haijaisha bado.Aluta Continua..
 
Kingunge anajichanganya, kamati ya maadili inaandaa ripoti kwa ajili ya kamati kuu yes na ndo ilichofanya.

Inawezekana pia kamati kuu kutokana na muda wakaomba kamati ya maadili iwasaidie kuchuja makapi yote. na ndocho walichofanya.

Kingunge alitaka mambo yaende kwa shinikizo la kuhadaa kwa kutumia media kama anavoendelea kufanya. Haipendezi mtu mzima kama yy kushabikia kundi ndani ya chama tena kundi lenyewe sio la watu wasafi

Mkuu Ngundengunde.
Kwa dhana hiyo (Kamati kuu ku-delegate kazi zake kwa kamati ya maadili) ili kurahisisha kazi zake, itakuwa imefanya kosa la msingi na la kihistoria, ikizingatiwa unyeti wa suala lenyewe.
 
Hivi alikatwa mtu mmoja tu au zaidi ya watu 30??????

Yes alikatwa mmoja,
wengine walmsindikiza huyo mmoja aliekatwa koz walijua tangu mwanzo wakati wanachukua fomu kuwa wasingeweza kushinda.
Una swali lingine mkuu?
 
Back
Top Bottom