Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Tunaweza kuwaza nadharia nyingi. Pia inawezekana ni mtu malaria imepanda kichwani akafanya hayo. Baada ya muda tutapata habari kamili.

Hata kama ni Malaria, inawezekana vipi mtu kumiliki silaha ya kivita kama hiyo? huyo atakuwa ni GAIDI. Naomba serikali ya awamu ya sita iwe macho huwenda kuna tukio liko njiani linakuja…
 
Tukio lililotokea leo jijini Dar wote limetuacha na maswali mengi. Wakati vyombo vya usalama vikiendelea kulitakafakari na kujiuliza mengi kuhusu tukio hili la kusikitisha, sisi wananchi tunalilaani sana na tunapongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuchukua hatua za haraka na za kishujaa kulidhibiti.

Pengine madhara yangekuwa makubwa zaidi. Tunawapa pole sana walioathirika na tukio hili kwa namna yoyote ile zikiwemo familia za maaskari wetu shujaa walioripotiwa kuwa wameuawa katika tukio hilo. Inasikitisha sana.. Matukio kama haya yanadhihirisha umuhimu wa serikali kuongeza nguvu katika kufuatilia na kuwatia kwenye mkono wa kisheria yeyote anayetuhumiwa kuhusika na masuala ya uhalifu na ugaidi bila kujali rangi, dini, kabila, cheo wala itikadi yake ya chama.

Yeyote anaweza kufanya uhalifu na yeyote anaweza kuwa gaidi. Kuna wengine wamekuwa wakipima suala la ugaidi na kiwango cha pesa. Wanataka wasikie kiasi cha mabilioni na matilioni yanatajwa. Hivi huyu jamaa wa leo, ametumia matilioni mangapi kufanya alichoweza kufanya? Nasikia hata bunduki aliyotumia amepora kwa askari (kama ni kweli).

Uhalifu na ugaidi uko zaidi kwenye fikra kuliko kiwango cha pesa. Kwa anayekamatwa vyombo vya sheria ni bora kuhakikisha kuwa sheria inatumika kwa usahihi na anayepatikana anapewa adhabu kali kwelikweli. Ni nani aliyejua kuwa huyo jamaa angeweza kufanya tukio hilo lililoshtua jiji na nchi nzima.?

Hakuna anayeweza kusema kwa uhakika wa nafsi yake kuwa fulani siyo mhalifu, au fulani siyo gaidi. Hakuna, si askofu, si mfuasi wa chama, si mwanafamilia, si yeyote. Hakuna. Muhimu ni kuacha vyombo vya usalama na upelelezi kufanya kazi yao na sheria kuchukua mkondo wake.
 
Walimdanganya aigize ugaidi watampa nusu iliyobakia, alipoomba po wakamuua.
Tanzania hakuna ugaidi, free Mbowe.
 
Aliyekwambia yule ni gaidi nani boya wewe yaani mnatengeneza sinema feki then muwaaminishe watu kuwa kuna ishu, hakuna ishu pale ni mwendelezo wa sanaa za Siro na kampani yake lijamaa liko kwenye magari ya polisi kila siku kwenye doria leo linajiita gaidi? aibu wangetumia hata mtu mwingine ambaye hafahamiki Dar, Hopeless and shameless police, imevuja hii wala hamdanganyi mtu tena , kuna jambo Mungu anataka awaonyeshe polisi
 
Si huwa kuna askari muda mwingi hapo kwenye kona ya kuelekea Masaki?

Hata Usalama wa Taifa si mbali sana hapo, kituo cha polisi Selander kipo karibu pia, hapo nyuma nyumba za O'bay kuna wastaafu kadhaa wa JWTZ
Huko Tz kwa kweli Askari bado sana, ni vile tu nchi imetulia hebu check huyo Mtu mmoja alivyosumbua hapo, anatembea tu free kabisa kabla ya kufikiwa na askari?
 
Back
Top Bottom