Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Tunajua hili lazima ni suala la uanaharakati wa kidini kwa huyu kijana msomali kuua asjari wawili wa polisi.
Nimesikitikia utayari wa polisi wetu waliokuwa lindo, kuvamiwa na silaha kuchuliwa na wao kuuwawa.
Halileti picha nzuri kwa utayari wa askari wetu.
Hata hivyo RIP vijana wetu.
Ila ingekuwa wameambiwa wakadeal na chadema hakika ungefurahi mwenyewe
 
Guys I am informed there’s a guy shooting randomly near Stanbic Bank, anyone with more news?

Inadaiwa kuna watu wameuawa. Ni Karibu na Makao Makuu ya Stanbic.

========

Mtu mmoja ambaye alionekana kufyatua risasi karibu na Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam amedhibitiwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Simon Sirro amethibitisha kuuawa kwa askari wawili kwenye mapambano ya kurushiana risasi yaliyotokea eneo la Daraja la Salenda jirani na Ubalozi wa Ufaransa, Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 25, 2021 baada ya mtu mmoja ambaye hajafahamika kuzua taharuki baada ya kufyatua hewani risasi huku akisikika akisema kuwa anawatafuta polisi.

Akizungumza katika kikao kazi cha maofisa wa polisi, Sirro amesema mtu huyo naye ameuawa kwa kupigwa risasi.

“Mmeziona clip zinaruka sasa hivi akaingia barabara kubwa akawa anatamba na SMG na yeye amepigwa risasi na askari wetu hivyo, askari wetu wamefariki na yeye amefariki” amesema IGP Sirro.

Ameeleza kuwa wanaendelea kufuatilia kufahamu mtu huyo ametokea wapi na baadaye watatoa taarifa kamili.

IGP Sirro amenukuliwa kupitia kipande cha video kilichorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa Wasafi Fm.

PIA SOMA:
1. Mashuhuda wasimulia tukio la aliyekuwa akipiga risasi

UPDATE:
Jeshi la Polisi limesema idadi ya Watu waliouwawa na Mtu mwenye Bunduki aliekua akifyetua risasi ovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa Dar es salaam ni Watu wanne huku kati yao Watatu wakiwa ni Polisi na mmoja ni Mlinzi wa Kampuni binafsi ya ulinzi.

"Leo August 25 2021 tumekutwa na tukio baya kabisa, tukio la kihalifu ambalo limepoteza maisha ya Watu wanne na watatu kati yao ni Askari Polisi, limetokea katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni Askari wetu walikua kazini akatokea Mtu akawashambulia kwa Bastola na alipowashambulia na kuanguka alichukua Bunduki za Askari hao na kuanza kurusha risasi ovyo kuelekea Ubalozi wa Ufaransa"


View attachment 1907510
View attachment 1907511


View attachment 1907519


Hii ni developing news…

Kuna mtu mmoja, kapigwa risasi na kuanguka katikati ya barabara
View attachment 1907602
View attachment 1907621
View attachment 1907645View attachment 1907646
Huyu anadaiwa kauawa.
Muanze sasa kupambana na magaidi halisi sio wa kubumba.

Mmoja tu lakini kafanikiwa kuua askari wawili wenye silaha tena mchana,aibu sana
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi ametoa taarifa mpya kwamba mpaka sasa idadi ya waliouawa ni watu 4 , askari watatu , mmoja ni mlinzi wa kampuni binafsi ya SGA , huku jeshi la polisi likimuua Mshambuliaji na kufanya waliofariki kufikia wanne

Waliojeruhiwa ni watu 6 .
Uyo wa 4 atakua ni yule alie enda kindezi na mguu wa kuku bila tahadhar yoyote
 
Tunajua hili lazima ni suala la uanaharakati wa kidini kwa huyu kijana msomali kuua asjari wawili wa polisi.
Nimesikitikia utayari wa polisi wetu waliokuwa lindo, kuvamiwa na silaha kuchuliwa na wao kuuwawa.
Halileti picha nzuri kwa utayari wa askari wetu.
Hata hivyo RIP vijana wetu.
Ngoja wawakute mkiwa watu 10 mnajadili katiba Mpya. Wanawaita Waandishi wa habari na kuutangazua umma kwamba wamekamata Magaidi.
 
Waliouawa hawakuwa traffics,ni askari wenye silaha na tena walinyang'anywa silaha.

Waendelee kupambana na wapinzani na Magaidi feki,ila magaidi halisi wakipiga simu pokeeni msikimbie maana wameanza kwa kubeep kwanza.
Gaidi mmoja ananyanganya watu wanne siraha na kuwaua? inamaana wangekuwepo askari wengi zaidi jamaa lingewamaliza
 
Back
Top Bottom