Kiongozi anapohamasisha ongezeko la bei ya vyakula, anaelewa Madhara yake?

Kiongozi anapohamasisha ongezeko la bei ya vyakula, anaelewa Madhara yake?

Wanunuaji ndio hao hao watumishi wa umma wanaopigishwa kwata la nyongeza za mishahara kwa miaka minne kavu makato ya bodi ha mkopo kodi n.k
Wakiongezewa ndo chakula hakitapanda au kitapanda pia?
 
Kama zaidi ya 75% ya watanzania ni wakulima (kama inavyosemekana) huoni kua anapigania maslahi ya walio wengi.

Angesema vinginevyo unadhani comments za wakulima zingekuaje?
Poleni sana...ila ipo siku utaacha hii dhambi.
Hivi kila mtu akipandisha bei ili awapige wanunuaji au walaji nini kitatokea..
Mwenye shule apandishe ada,mwenye chakula apandishe bei,mwenye shell za mafuta apandishe bei,mwenye gari apandishe bei..Je ,raia ambao awana mali kama hizo itakuaje?
Sukari tu watu wamepandisha kwa shilingi mia tatu...imekua kilio.
 
"Watwangeni Kweli Kweli" Kauli ya rais wa nchi wa wakulima, wafanyakazi, machinga, mgambo na hata wanafunzi. sawa!
 
Anatakiwa anyang'anywe madaraka haraka sana. Yeye anakula bure chochote atakacho ila ana jeuri ya kutaka wengine wauawe kwa njaa kwa sababu ya kushindwa kununua chakula. Yeye ameshawahi kununua sukari kwa 5000? Kuna jamaa alisema "nchi imekabidhiwa washamba na malimbukeni" . Simkumbuki ni nani ila naamini alikuwa sahihi.
 
Amewasahau akina kangomba wamesha nunua na kuhifadhi mazao cku nyingi
 
Nyie muda wa shamba mlikuwa mnacheza pulltable
Mpambane na hali zenu
Mkuu, unadhani nchi yote hii ni ya wakulima? Unadhani ni sahihi kiongozi kuhamasisha bei ya sukari ipandishwe juu?
 
Misimu karibu miwili mfurulizo wakulima tulishindwa kumudu ghalama za kilimo/pembejeo kwasababu ya soko baya Sana. Lkn sikuona mtu anawatetea wakulima
Sasa Kama bei itakua nzuri msimu huu itakua zamu ya mkulima kunufaika
Anatakiwa anyang'anywe madaraka haraka sana. Yeye anakula bure chochote atakacho ila ana jeuri ya kutaka wengine wauawe kwa njaa kwa sababu ya kushindwa kununua chakula. Yeye ameshawahi kununua sukari kwa 5000? Kuna jamaa alisema "nchi imekabidhiwa washamba na malimbukeni" . Simkumbuki ni nani ila naamini alikuwa sahihi.
 
Kazi yenu kupotosha sikuiz imekua ya kijinga Sasa magufuli amesema wakipima wasiuze mazao Yao kwa hasara waangalie Bei wewe unakuja kumkosoa ivi unajua wakulima wanavyo nyonywa
Wanaolima ni wa vijijini mashambani wa mjini hununua na kutumia toka shamba
Ebu twambia
Nani Mnunuzi anayetwangwa hapo kama sio wakazi wa mjini hata kuuza nje ya nchi mkulima hauzi nje.anayeangalia bei ni mfanyabiashara sio mkulima
 
Acheni kulialia, basi nendeni mkalime.... upo mjini na huwezi kumudu ‘chakula’ tu nawe unajiita wa mjini..!!
 
Sasa taratibu naanza Kuamini kuwa wengi ya wale wanaomchukia Rais Dkt. Magufuli huwa wanakuwa wanakurupuka katika Kumuelewa asemacho.
Nani kakwambia kila anayemkosoa anamchukia? Unajua maana ya vyama vingi? Haya tueleze tusicho elewa kwenye hili.
 
Si kila mkosoaji ni chadema ukiandika pumba zitapuuzwa hii ni Jf sio vikao vya kijani


Mijitu mijinga Sana Hasa ya chadema ingekua na akili saiz ingechangamkia fulsa hamjui wakulima wanafanya kazi kwa ugum kias Gan Kama huna hela ya kumudu nenda kalime uje uwauzie wenye uwezo Sio mnalia Lia tu
 
Zaidi ya asilimia 75 ya watanzania ni wakulima Sasa huoni anawapigania watanzania wengi? Acha kukaa maskani na kucheza pool table ingia shambani ulime halafu uje ufungue Tena nyuzi nyengine
Nani kakwambia najua hata kucheza pool? Nani kakwambia uongo huo wa %75 ya watanzania ni wakulima, ina maana mazao yanauzwa kwa asilimia 25 tu? Nani kakwambia kila mkulima analima vyote na kujikidhi na vyote? Tumia akili acha kujiabisha, wenye akili wanajua ninacho kisema.
 
Kazi yenu kupotosha sikuiz imekua ya kijinga Sasa magufuli amesema wakipima wasiuze mazao Yao kwa hasara waangalie Bei wewe unakuja kumkosoa ivi unajua wakulima wanavyo nyonywa
Ni nyie mnao potoshwa na yeye kirahisi, kwa nini aseme watwangeni, unajua maana yake? Rais gani atasema hivyo kwa raia wake? Tumia busara na akili zako mwenyewe.
 
Nyie muda wa shamba mlikuwa mnacheza pulltable
Mpambane na hali zenu
Kwa taarifa yako anaepata faida ni mfanyabiasha mwenye uwezo wa kutunza mazao (kagomba) hata mwaka mzima.

Mkulima anauzia shambani hivyo sahau mkulima kufaidika.
 
Back
Top Bottom