Kiongozi anapohamasisha ongezeko la bei ya vyakula, anaelewa Madhara yake?

Kiongozi anapohamasisha ongezeko la bei ya vyakula, anaelewa Madhara yake?

Bei za Vyakula zimewahi watoa wakuu wengi wa nchi baada ya kupanda na kushindwa kudhibitiwa.

Tumewahi kushuhudia hata bei ya Mkate tuu imeshawahi kuleta matatizo kwa tawala mbalimbali.

Je, hii kauli ya mheshimiwa Rais Magufuli anaelewa madhara yake iwapo itafuatwa?

IMG_20200531_075503.jpg
 
Tatizo lenu mnachukua ka sentensi kamoja ka Rais mnaanzishia hoja ndio maana mnazidi kupwaya

Rais alikuwa anazungumzia kuwapiga bei wale walio ji lockdown wakati wa Corona akimaanisha Nchi jirani

Kuna ubaya gani kuhamasisha Raia wako kuwapiga bei ya Juu nchi za jirani ili kuimarisha uchumi wao?
 
Jibu la kwa nini sukari imekuwa bei juu limepatikana...!!
 
Tatizo lenu mnachukua ka sentensi kamoja ka Rais mnaanzishia hoja ndio maana mnazidi kupwaya

Rais alikuwa anazungumzia kuwapiga bei wale walio ji lockdown wakati wa Corona akimaanisha Nchi jirani

Kuna ubaya gani kuhamasisha Raia wako kuwapiga bei ya Juu nchi za jirani ili kuimarisha uchumi wao?
Kauli ya kiuongozi mkuu wa nchi Ina impact kubwa. Hiyo hiyo sentennsi moja inaweza kuwa na madhara kuliko hutuba mzima. Ngoja tusubiri tuone.
 
Tatizo lenu mnachukua ka sentensi kamoja ka Rais mnaanzishia hoja ndio maana mnazidi kupwaya

Rais alikuwa anazungumzia kuwapiga bei wale walio ji lockdown wakati wa Corona akimaanisha Nchi jirani

Kuna ubaya gani kuhamasisha Raia wako kuwapiga bei ya Juu nchi za jirani ili kuimarisha uchumi wao?
Kwa maana nyingine wakulima si watataka kuyauza soko la nje ili waifidike kuliko kuyauza ndani kwa bei rahisi. So lazma yatapungua kwenye soko la ndani kwa maana mtaishia kununua sawa na mkenya anapoyanunua. Mfano si juzi mmeyapeleka zimbabwe na bado tukaishia kununua unga bei mara mbili.
 
Ataelewa wapi na wakati kila kitu anakipata bure! Angekua na yeye akiamka asubuhi anaandaa bajeti ya siku nzima kama sisi makapuku, angeelewa mapema sana madhara ya hicho alichokisema.

Na ndiyo maana simshangai anapojiamulia tu kwa utashi wake binafsi kuwaumiza wafanyakazi kwa kuwanyima stahiki zao za msingi mfano kupanda madaraja kwa wakati ili tu ajenge miradi ya kumuongezea ujiko.

Angekuwa na yeye anafanya kazi huku akitegemea mshahara kuendeshea maisha yake kama wafanyakazi wa kima cha chini wa nchi hii, asingeongea hivyo! Bahati mbaya kuna fungu la kutosha tu hupelekewa hapo Ikulu kila mwaka ili aweze kuishi maisha ya peponi! Ni lini atazijua shida za wengine?

Amalize muda wake vizuri akapumzike tu! maana hakuna mfanyakazi mwenye akili timamu anaweza kumfagilia Rais Magufuli kwa uonevu wa wazi anaotufanyia. Bora hata ya JK alijitahidi kututhamini. Ila siyo huyu mwalimu wa zamani. No ajira mpya, no salary incriment, no promotion!
 
Watanzania tunapaswa kuzidi kumshukuru Mungu. Tumepata Rais ambaye anagusa kila kundi na makundi hayo yamekuwa yakinufaika sana na uongozi /mwongozo wa Rais wetu. Eee Mungu Baba tulindie kiongozi wetu ili azidi kutuongoza vyema. Ikikupenda wewe na awe kiongozi kwa miongo mingi zaidi. Hakika huyu anatufaa.
 
Tatizo lenu mnachukua ka sentensi kamoja ka Rais mnaanzishia hoja ndio maana mnazidi kupwaya

Rais alikuwa anazungumzia kuwapiga bei wale walio ji lockdown wakati wa Corona akimaanisha Nchi jirani

Kuna ubaya gani kuhamasisha Raia wako kuwapiga bei ya Juu nchi za jirani ili kuimarisha uchumi wao?
Wewe nae ni mpuuzi tu wapenda kupindisha maneno; miji ya nchi za jirani :zilizofungwa wanafanya biashara siyo kulima. Wewe ukiwafungia watu Dar ndiyo Mpanda na Kyela hawatalima? Uchumi imetushinda miaka yote hayo kuwapita ndo leo tuwapite kwa mwezi mmoja?
Nairobi, Mombasa au Kampala wanalima mazao gani?
Ujinga umewajaa kwelikweli.
 
Back
Top Bottom