Kiongozi anasimama anasema foleni inasababishwa na magari machafu yasiyo na AC

Hamna cha ugumu. Shida ni kwamba viongozi hawana utashi wa kuchukua hatua sahihi. Wamebaki kupiga siasa tu na kubwabwaja hovyo.
Uchawa ukizidi unakuwa chizi au huwaoni mkuu?
 
Aache ujinga dawa ya foleni ni kujenga barabara za kutosha.
 
Mi naongelea upande wa Magari, AC na namba zisababisha vipi foleni?
Tumia common sense, unafeli wapi? Au ubongo wako umezoea kulalamika tu kila jambo?

ukiruhusu hovyo magari ya zamani wamiliki wa magari wanakuwa wengi hence foleni barabarani, kinyume chake ukihamasisha magari mapya au ambayo siyo ya zamani sana wamiliki watakuwa wachache (sababu ya bei kubwa ya gari) hence kupungua kwa foleni

Sasa umeshaona wapi kila aina ya chombo cha moto kiingie katikati ya mji? Kuna baadhi ya miji hata hilo gari lako mpya haliruhusiwi kuingia katikati ya kkoo au Posta mpya
 
Msidhani Watanzania ni wale wa mwaka 47. Tutajie hiyo miji ambayo gari zinaruhusiwa au kukatazwa kutumia barabara fulani kulingana na plate number ya gari.

Huyo Chalamila ukimnyang'anya gari ya serikali, sidhani kama ana hata hicho kicorolla kisicho na AC.
 
Wapunguze kodi lukuki ili watu waweze kumudu kununua magari ambayo siyo ya zamani sana.
 
Matokeo ya kula na kuvimbiwa, halafu kutapikia wananchi wanaompa chakula!
 
Wajinga bado wapo kumbe.

Mfumo wa usafiri wa Dar es Salaam tulishashauri humu suluhu yake ni wajenge trams.

Na kuongeza lanes za barabara , hizi siasa zingine ni upumbavu Chalamila atembee duniani "RETRO CARS" zinauzwa bei ghali sana kwenye minada kuna watu wanapenda kupata ile "nostalgic feeling" ya magari asiwapangie waendeshe kipi.


View: https://youtu.be/W5tQm8HBB2Y?si=1Xz670dRKU4au2vj
Hivyo vibarabara vyenu vya lanes mbili hata hakuna pedestrian path na bado kila kukicha ni kutamba tu tuna rasilimali nyingi hadi mabeberu wanatuonea wivu, sasa hizo rasilimali mbona hatuoni matunda yake?
 
Umeona ulivyo mwehu sasa? Wewe choo kikijaa nyumbani kwako huwa unawaambia wapunguze kula ili wasinye sinye ovyo? Au huwa unaboresha miundombinu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…