Kiongozi anasimama anasema foleni inasababishwa na magari machafu yasiyo na AC

Kiongozi anasimama anasema foleni inasababishwa na magari machafu yasiyo na AC

Sio rahisi hivyo bosi hasa kwa mji ambao ulishajengeka kiholela.
Pendekeza hizo hatua sahihi upate zawadi ya shs 10,000,000. Zawadi hiyo inashindaniwa mwezi huu wa tatu.
Siwezi kupoteza muda wangu kwa hilo. Kwa hiyo wanajenga barabara, njia za mwendokasi huku hawajui njia za kutatua foleni. Sasa wamekuwa wanafanya nini ofisini?
 
Mnaoendesha vigari vitakataka kama vikorola namba A nafikiri mmemsikia vizuri mhe. Chalamila.
DSM tunataka namba E tu, umri wa gari siyo muhimu-iwe gari ya 1980 au 1990 au 2000 mradi ina namba E inaruhusiwa kuja Dar.

Namba E haimaanishi ni gari la bei kubwa au ni gari mpya.
Vipaso au vivitz vya 2003 -2013 vyenye namba E vipo.
Ndiyo huwa najiuliza. Tanzania ukiondoa magari ya kifisadi ya viongozi wa serikali, yaliyobaki asilimia kubwa ya magari yaliyopo barabarani ni ya miaka 10+
 
Wewe ndiyo mwehu, unaleta mfano usiohusiana kabisa na nilichokufundisha

Choo na magari mabovu wapi na wapi?

Issue hapa ni magari mabovu na ya zamani kuingia katikati ya mji

Huwezi kuruhusu kila mtu kila kitu kifike mjini katikati umewahi kuona wapi Mji wa hovyo hivyo?

Badala watu waweke bidhaa madukani wanapangana barabarani hata kupishana ni vikumbo na mijasho ndiyo mji gani huo!?
Kumbe ndio una Low IQ kiasi hiki?

Mbona mfano upo clear? Kama miundo mbinu ikizidiwa ifanyie maboresho. Sasa choo kikijaa, au barabara ikizidiwa, unafanya maboresho au unazuia watu wasitumie? Kwamba kuanzia leo kukzeni pizza na burger tu, sii mnakula makande kujaza choo tu, ndio kama usema vicorrila namba A visitumie barabara..
 
Wajinga bado wapo kumbe.

Mfumo wa usafiri wa Dar es Salaam tulishashauri humu suluhu yake ni wajenge trams.

Na kuongeza lanes za barabara , hizi siasa zingine ni upumbavu Chalamila atembee duniani "RETRO CARS" zinauzwa bei ghali sana kwenye minada kuna watu wanapenda kupata ile "nostalgic feeling" ya magari asiwapangie waendeshe kipi.


View: https://youtu.be/W5tQm8HBB2Y?si=1Xz670dRKU4au2vj

Hivyo vibarabara vyenu vya lanes mbili hata hakuna pedestrian path na bado kila kukicha ni kutamba tu tuna rasilimali nyingi hadi mabeberu wanatuonea wivu, sasa hizo rasilimali mbona hatuoni matunda yake?

Angetembea angejifunza na kuelewa mambo mengi

Ova
 
Angetembea angejifunza na kuelewa mambo mengi

Ova
Naam, sasa mtu kakulia huko vijijini na Dar es Salaam ndio jiji lake la kwanza kubwa kufika na hajatoka tena hawezi kujua trams na metro/subway kwenye majiji yaliyoendelea.

Hawezi pia kuona hizo retro/vintage cars za bei mbaya kabisa hata kuliko magari mapya watu wanaendesha.

Katika video hiyo hapo kuna gari za 1970 zinatembea vizuri na ni bei mbaya kuliko hata gari anayotembelea huyo mshamba Chalamila.
 
Inabd arudshe vyeti vya Taaluma

Nazan TCU ,nacte necta veta waweke sheria kuwa ukitenda na kuongea boko wafute vyeti vyako atakama ulishamalz chuo
 


Mnyalukolo Chalamila, tuheshimiane.
Nimekutangulia hapa mjini wakati uko huko Kilolo Iringa ukilima viazi.

KiCorolla changu ndo kila kitu
-nimeolea kiCorolla hiki
-mitaa ya Mwananyamala na Sinza kwa wajanja, natamba
-Engine ya kiCorolla changu ni IST, mafuta naweka mara moja kwa wiki.
-hivi vi Corolla ni vya mission town, vinaingia madimbwi ya Mombasa, Ukonga na kutoka bila taabu
-usione moshi wa exhaust, na AC hazifanyi kazi, natafuta spare zake zitakazo bomolewa toka gari za serikali kule Temeke.
Wiki ijayo tuko sambamba mjini.
 
Nafikiri serikali ingeshusha ushuru wa kuingiza magari kwa magari mapya au ambayo hajatumika sana ili iwe rahisi wananchi kununua magari mazuri. Kwa sasa mtanzania kumiliki gari ni jambo gumu hatari. Ushuru na gharama nyingine unakuta ni 100% ya bei ya kununulia gari. Au ingeshusha ushuru wa kuingiza gari na kuweka toll gate kila wilaya kufidia ile kodi itakayopotea.
 
Kwa nini kubanana hapo hapo mjini? Serikali itafute eneo jingine barabara ya lindi au kibaha au bagamoyo ujengwe mji mwingine wa kisasa.

Mifano ipo mingi:
1. Delhi vs New Dell
2. Hyderabad vs Secunderabab
3. Tri cities: Richland vs Pasco vs Kennewick
 
Back
Top Bottom