Kiongozi anasimama anasema foleni inasababishwa na magari machafu yasiyo na AC


Mnaoendesha vigari vitakataka kama vikorola namba A nafikiri mmemsikia vizuri mhe. Chalamila.
DSM tunataka namba E tu, umri wa gari siyo muhimu-iwe gari ya 1980 au 1990 au 2000 mradi ina namba E inaruhusiwa kuja Dar.
 
Serikali ya mihula hii miwili imesahau jukumu la msingi la serikali ni kupanga...

Huwezi kukosa foleni endapo umeutapanya mji pasipo master plan...

Nyumba za makazi zipo magharibi, shughuli muhimu za watu zipo mashariki halafu kati yao wanaungwa na barabara kubwa moja tu...

Waende miji kama Barcelona, Paris au Beijing wajifunze namna mji unavyopangwa kuanzia barabara hadi makazi...
 
Namba E haimaanishi ni gari la bei kubwa au ni gari mpya.
Vipaso au vivitz vya 2003 -2013 vyenye namba E vipo.
 
Usidanganye watu Nchi yetu kwa sababu hatuna bara bara zenye ubora ndio maana tunakataza Truck zisifike Mjini niliwahi kuwaambia madereva ingekua SA wanakataza kama kwetu kazi tungekua nayo maana kufika baadhi ya maeneo ili gari ikapakie lazima upitie mjini Tanzania unashangaa magari makubwa yanayopakia mizigo bandarini yanasumbuliwa wakati hapa Durban gari ya mzigo inaheshimiwa kwa sababu inaleta pesa Tanzania parking za mtaani watu wanalipia tena hela nyingi tu ukienda na gari mjini SA parking kokote ardhi ya Wananchi sio ya mabeberu ila ukipeleka maeneo yaliyojengwa kwa ajili ya parking ndio utalipia tumekua masikini sana mpaka akili zimedumaa na tunakua na maamuzi ya hovyo hovyo tu..
Hapa ni mjini na Truck yenye mzigo inapita hapa nitaweka picha au video baadae..
 
Yule jamaa ni mjinga sana anaropoka ropoka ovyo hajitafakari au anajua gani ni kama kalio kila mtu analo au anaweza kulimudu. Awe na adabu akiongea. Namdharau sana mtu mwenye elimu ya darasani ila akili ya maisha tu box tupu
 
Ila hii nchi tunapitia mengi, mnamkumbuka yule wa IST?
 
Tayari sgr imeanza kubeba contena za mizigo, bandari kavu zinaanza kufanya kazi

Muda si mrefu malori hayataingia tena mjini

Watanzania wengi ubongo wao umejaa kulalamika kila jambo, hawajawahi kuona zuri lolote la serikali
 
Umeona ulivyo mwehu sasa? Wewe choo kikijaa nyumbani kwako huwa unawaambia wapunguze kula ili wasinye sinye ovyo? Au huwa unaboresha miundombinu?
Wewe ndiyo mwehu, unaleta mfano usiohusiana kabisa na nilichokufundisha

Choo na magari mabovu wapi na wapi?

Issue hapa ni magari mabovu na ya zamani kuingia katikati ya mji

Huwezi kuruhusu kila mtu kila kitu kifike mjini katikati umewahi kuona wapi Mji wa hovyo hivyo?

Badala watu waweke bidhaa madukani wanapangana barabarani hata kupishana ni vikumbo na mijasho ndiyo mji gani huo!?
 
Tayari sgr imeanza kubeba contena za mizigo, bandari kavu zinaanza kufanya kazi

Muda si mrefu malori hayataingia tena mjini

Watanzania wengi ubongo wao umejaa kulalamika kila jambo, hawajawahi kuona zuri lolote la serikali
Ili kuondoa foleni ni kujenga bara bara za miaka 50 mbele ikiwezekana kiwa na mpango wa kuwalipa baadhi ya wakazi kwa ajili ya kujenga bara bara mpya maana mji unakua kwa kasi harafu bara bara bado ni changamoto hatuna bara bara hapo na hayo magari tunayaona mengi nj machache sana ni vile tumejibana sehemu moja..
 
Matokeo ya kula na kuvimbiwa, halafu kutapikia wananchi wanaompa chakula!

Pimbi Chalamila , keshaanza kulewa madaraka.
Ma LC300 yanayotokana na kodi zetu yameanza kumlewesha, na magari hayo hajui kuwa ni kodi za hao wenye vicorolla vinavyotembea barabarani vikisaka tonge.
 
Hamna cha ugumu. Shida ni kwamba viongozi hawana utashi wa kuchukua hatua sahihi. Wamebaki kupiga siasa tu na kubwabwaja hovyo.
Sio rahisi hivyo bosi hasa kwa mji ambao ulishajengeka kiholela.
Pendekeza hizo hatua sahihi upate zawadi ya shs 10,000,000. Zawadi hiyo inashindaniwa mwezi huu wa tatu.
 
Yupo sahihi,tatizo wabongo hatupendi kuambiwa ukweli.!
Ni ngumu sana Kuongoza watz

Hawaoni zuri hata 1

Mtu anataka kupanga Mji uwe mzuri na MUONEKANO wa kistaarabu watu wanamtukana

Watu wa Nchi hii wengi wanachojua ni kupinga tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…