Siamini kama Iran anaweza kuwa na air defense ya aina ya S400, Patriot na hizi Iron dome kulinda anga lake maana tayari ameonyesha udhaifu mwingi kwenye technolijia, kama ana uwezo huo asingeweza kutumia Helicopter ambayo ni made in USA kumbeba Rais huku akiwa na vikwazo vyakununua spare parts.
Zile drones bado sana mkuu aisee, drones zake kamikaze nyingi zimeprove failure Russia, na hata hizi tunazosema zimepenetrate air defence ya Israeli inawezekana ni ile tunasema huwezi kuwa na 100% efficiency, zipo drones za Turkey ambazo angeweza kuzinunua na kutumia wataalam wake kucopy na kupaste akafanya mass production.
Kuwa na missiles launcher sio shida, kama huna satellite zinakuwa rahisi sana kukamatwa au hata kuwa diverted kwenye targets.
Anachofanya/alichofanya Iran ni kurusha missiles nyingi kama mvua ili kuoverwhelm air defense na makombora kadhaa yaweze kufika lakini hii unaweza kuipangua kwa kuongeza number za batteries, kumbuka pia unaposhambulia nawe unashambulia hakuna kusubiliana maana uwe na uwezo wa kushambulia na muda huo huo ujilinde.
Narudia tena, Iran awe mtulivu ajenge technolojia yake kwanza kupambana na hizi superpower, uwezo wake bado sana.
Mkuu kuna maeneo umedanganya.
-Kamikaze drone za Iran hazikufeli Russia,zimeprove kuwa na ufanisi na zishapelekwa zingine zinatumika.
Drone iloshambulia Tel Aviv kwa kutumiwa na Houthi haikuwa detected mpaka ikafanya shambulio it means iron dome ilifeli kuigundua,na hiyo ni Iranian made.
Drone zote ambazo anatumia Hizbollah Lebanon kumshambulia Israel ni Iranian made.Na hazikuwahi kufeli zote zimeshambulia Galilaya kwa ufanisi na kuleta damage.
-Makombora anayotumia Hizbollah ambayo ni guided ballistic missiles ambayo yalionesha kukwepa air defence system na kushambulia Northern Israel kikamilifu na yalirushwa guided missiles 680 tokea October yote yalipenya succesfully na hakuna hata moja Iron dome waliweza kulidungua.Na yote hayo ni Iranian made.
-Iran ana varieties of missiles ambazo zina uwezo tofauti tofauti nenda kafuatilie mkuu,yale makombora alotumia Iran dhidi ya Israel hayakua guided missiles,Na cha kushangaza ni light unguided missiles licha ya mataifa manne kumsaidia Israel kuya intercept bado makombora 7 yakapenya.Jiulize kama Iran angetumia kombora lenye usanifu kama lile alilopiga kwenye kambi ya USA Iraq 2018 lingetokea nini.
Tukirudi kule kuhusu teknolojia ya ndege,mkuu teknolojia ya drone na aircraft hazifanani.
Huwezi ukafananisha uundaji wa drone na helikopta au ndege kamili.
Iran ana teknolojia kubwa katika uundaji wa kamikaze drone ila uundaji wa aircraft bado haijajipambanua.
Kuhusu ADS kazifuatilie BAVAR-373 na Khordak air defence systems.
Ndizo zilidungua drones za upelelezi za USA.
Pia usisahau kipindi cha Obama 2013 kuna drone za USA zilishushwa pasi na kulipuliwa ndani ya anga la Iran,je hiyo ni tech ndogo mkuu.
Shambulio la Haniyeh lilifanyika ndani sio nje ya mipaka ya anga.