Wakati wa awamu ya tano msimamo wa serikali ulikuwa hakuna watoto kurudi shule endapo watapata ujauzito. Kauli hii yakishenzi iliungwa mkono na wanasiasa wakiwemo wabunge na hata viongozi wa dini,taasisi za kirahia na wanazuoni mbalimbali.
Wakati Kigogo mmoja jina linahifadhiwa akiwa kinara wa kuzuia watoto wasirudi shule mwanaye wa kike alipata ujauzito kutoka kwa mwanafunzi aliyekuwa anasoma naye shule moja ya hadhi hapa nchini. Familia hizi mbili za binti na kijana wa kiume waliitana wakakaa kikao na agenda kuu zikiwa kufichiana aibu na kutochuliwa hatua za kisheria kwa mwanaume aliyehusika Kama sheria zinavyotaka. Lakini pia kuona namna ambavyo vijana Hawa wataendelea na masomo ambapo binti aliachishwa masomo bila shule husika kupewa sababu na kijana kuendelea na masomo bila shule husika kutambua kwamba amempa mwanafunzi ujauzito.
Miezi sita tu baada ya binti kujifungua wazazi wamemtaftia shule nje ya nchi kwa ajili ya kuendelea na masomo huku mjukuu akibaki kwenye malezi ya babu na Bibi. Kwa kuona haya na kwakuzingatia namna tulivyoaminishwa kuhusu elimu kwa watoto waliojifungua nikaona nilete mada hii kwa sababu kuu mbili
1. Kwanza wanasiasa na wasomi wetu pamoja na viongozi wa dini wajifunze kuwa wakweli, waadilifu na wanaosimamia haki kwa watu wote bila kujali tajiri na masikini au msomi na asiyesoma.
2. Wazazi ambao hatuna nyadhifa Wala madaraka tusisikilize serikali tukaacha kuwasaidia watoto wetu wa kike, wao wanajua namna yakuficha aibu na kuendelea kupigania maisha ya watoto wao bila kuzingatia ujauzito na kadhia nyingine. Hoja kwamba tuwaadhibu watoto wetu hazina mashiko Cha msingi tuangalie ustawi wa familia zetu. Hawa wtu waliosoma na wenye nyadhifa si kila Jambo wanalosimamia wanaliamini Bali baadhi ya mambo wanafanya kupata ujira wao.