Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani, Freeman Mbowe ametengwa au amejitenga?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Tangu serikali ya awamu ya 5 iingie madarakani sijawahi kumshuhudia KUB Mbowe akitimba Ikulu iwe kwa niaba yake au ya chama chake.

Leo maalimu Seif ametimba Ikulu na hii ni mara ya pili.

Leo Prof Lipumba ametimba Ikulu na hii ni mara ya pili.

Leo mh Mbatia katimba Ikulu.

Mzee Lowassa akiwa Chadema aliwahi kutimba Ikulu.

Ndiposa najiuliza kwanini mh Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani hajawahi kwenda Ikulu?........ Je, hapati mwaliko au hatoi ushirikiano?

Ni hayo machache.

Maendeleo hayana vyama!
 
Huyo ni mpinzani wa kupinga hivyo ni lazima apingwe kuingia white house

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lipo kwa Rais Magufuli. Mbowe ndiye aliyetoa wito mara mbili kwa Rais. Lakini Rais anaamua akutane na wale wenye impact ndogo kuliko kukutana na CHADEMA, chama ambacho kimsingi ndiye mshindani mkuu wa CCM.

Nadhani kuna chuki binafsi, ukabila na guilty consciousness. Lakini bila kukutana na uongozi wa CHADEMA, yote itaonekana ni unafiki, na hakuna dhamira ya kweli. Lakini nina mategemeo atakutana naye mwishoni kabisa. Ameanza na wadogo kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…