Kiongozi wa machifu Tanzania ataka Serikali iwatambue rasmi machifu

Kiongozi wa machifu Tanzania ataka Serikali iwatambue rasmi machifu

Namsikiliza huyu Rais amekubali ombi lao na amesema anaandaa kikao akutane na mchifu Tanzania nzima 🤣 🤣 🤣 🤣🤣

Amesema pia anandaa na tamasha la machifu Tz, watashindania kombe linaloitwa Hangaya, ambalo ni Jina la Kisukuma alilopewa Samia likimaanisha nyota

Huyu mama nilidhani kwa kuwa ni mzanzibari (Mswahili) hataendeleza haya mambo ya ukabila, kumbe sikuwa sahihi
Uchifu ubaki symbolic, akiufufua itakuwa tabu. Loyalty ya watu itakuwa kwao kuliko hata kwa mifumo ya serikali
Somebody amuambie rais kuwa Amani na Utaifa uliojengwa na Nyerere ulitokana na kuvunjilia mbali vitu kama uchifu.
Samia akivirudisha vitatuzingua sana
 
Leo hapo bujora watamsiliba Kwa kila aina ya tunguli , kila Raisi lazima apite hapo sjui kuna nini , aah wakatoliki wanajua
 
Acha kutudanganya na wewe, wazaramo wanatoka wapi?
Dar wa kuhesabu walishahamia mkoa wa pwani kwa kuuzia wageni maeneo yao utawakuta kisarawe nk maeneo ya mkoa wa pwani.Dar ni wachache mno
 
Leo hapo bujora watamsiliba Kwa kila aina ya tunguli , kila Raisi lazima apite hapo sjui kuna nini , aah wakatoliki wanajua
Yako maeneo mawili hilo hapo la bujora na bagamoyo.Lazima maeneo hayo wapite
 
Wanataka turudi enzi za ujima!
Huko Mwanza na kanda ya Ziwa ni balaa kwa ushirikina, nenda Gamboshi.
Jinsi unavyoisikia Gamboshi na jinsi ilivyo ukifika huko ni vitu viwili tofauti kabisa, Gamboshi ni kijiji kizuri na kina maendeleo mazuri tu, na ukisema masuala ya uchawi sasa hivi majiji makuu ndio yanaongoza kwa uchawi, acha kabisa !!!
 
Uchifu ubaki symbolic, akiufufua itakuwa tabu. Loyalty ya watu itakuwa kwao kuliko hata kwa mifumo ya serikali
Somebody amuambie rais kuwa Amani na Utaifa uliojengwa na Nyerere ulitokana na kuvunjilia mbali vitu kama uchifu.
Samia akivirudisha vitatuzingua sana
Huyu mama hajiamini, naona anajilazimisha au analazimishwa kufuata umagufuli, maana haya mambo ya uchifu yalianza kuibuka awamu ya Magufuli namsikia Mwanza anajilazimisha kuongea kilugha na wasukuma,
 
Machifu na viongozi wa dini waendelee na shughuli zao kwenye jamii kama kawaida kwenye makanisa, misikiti etc hao wengine waendelee na mila zao .jando, harusi etc nchi haina dini wala kabila wakae huko huko, na wakuu wa wilaya hicho cheo kivunjwe kabisa kisiwepo hakuna wanachofanya zaidi ya kazi za chama chao kwa pesa za wananchi
 
Kwa hiyo hata wachaga waliohamia Dar siyo watu wa Moshi? hopeless kabisa
uraia wa moshi walishaukana Tanzania haturuhusu uraia pacha ndio maana wachaga kibao hugombea ubunge Dar
 
Kiongozi wa machifu Tanzania ataka serikali iwatambue rasmi machifu akisoma risala mbele ya Raisi Samia kwenye Takashi la Utamaduni Mwanza


Je anataka ukatili na serikali za kikabila urudishwe?
Uchifu,Utemi na Ufalme ni uimla na chanzo kikuu cha Ukabila.Mwl.Nyerere alivifuta ili kuimarisha Umoja,Usawa na Utawala wa Kidemokrasia(Hata hivyo hakufanikiwa kivile).Je,CCM baada ya kuua mfumo wa vyama vingi na Upinzani ndiko mnakotupeleka sasa?Machifu wa kazi gani tena?
Watanzania tudai Katiba ya Wananchi ili kulinusuru Taifa letu.Hawa wenzetu wamelewa madaraka waliyopora na wapo chakari.Hawana mbinu Mpya na wapo totally desperate na hatari sana.A dying Horse...
 
Kiongozi wa machifu Tanzania ataka serikali iwatambue rasmi machifu akisoma risala mbele ya Raisi Samia kwenye Takashi la Utamaduni Mwanza


Je anataka ukatili na serikali za kikabila urudishwe?

It will be a fatal mistake....Mama Samia, please don't do it. Hawa watahangaisha sana mbele ya safari. Kuna sababu maalum kwanini waliwekwa kando.
 
Kurudisha, kurasimisha na kuutukuza uchifu kutafanya turudi kwenye ukabila kwa spidi ya mwanga. Kuna sababu ya msingi sana kwanini huo mfumo uliuliwa na kutupiliwa mbali. Rais asiendekeze huo ujinga.
 
Back
Top Bottom