Serikali inapochoka kushughulikia matatizo ya wananchi wake na ikatukuza ufisadi, humuoana kila mwananchi/raia mpenda haki na ukweli kuwa ni adui mkubwa, hasa anapojitokeza kudai haki na kueleza ukweli. Madai ya madaktari ni mapana na yanagusa ustawi wa jamii. kwa mfano wanaposema vitendea kazi havipo, je ni kosa? mbona wao matumbo yakiunguruma tu, tunawasikia INdia. Hoja kwamba serikali haina pesa ni uongo wa mchana kweupe. Tujiulize serikali isiyo na pesa inakuaje na mabilioni ya pesa benki za nje kama uswisi n.k, serikali isiyo na pesa inakuaje ripoti ya CAG ionyeshe mabilioni ya pesa yakiwa yamepotea/yameliwa na taasisi moja tu/mtu mmoja,serikali isiyo na pesa inakuaje viongozi wake kila kukicha kiguru na njia kwenda ng`ambo kwa kisingizio cha kuona utendaji kazi wa balozi zetu,ooh mara kutafuta wafadhili wa bajeti, mara kutafuta wawekezaji, mara marafiki(sijui wa kike au kiume), mara kutangaza utalii. hiyo ni serikali ambayo viongozi wake wamechoka kufikiri, na viongozi wanaofikiri wapo uraiani na hao ndio wapambanaji wakweli. sas kazi ni moja tu, nayo ni kung`oa magugu yote ya CCM