Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Nimeiona pia kenye Nipashe sasa hivi online, ipo kama breaking news

Wednesday Jun 27, 2012


BREAKING
NEWS »
Dk. Ulimboka akimbizwa hospitali
Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini Tanzania Dk.Steven Ulimboka amefikishwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), akiwa mahututi baada ya kuokotwa eneo la Mabwepande.
 

umetoka nje ya mada...., kwahiyo haya niliyosema yanatosha!
 

sasa hii ni jf dokta,MMU au siasa.?
 
"Solidarity forever...." nimeunganishwa kwenye simu madaktari wanaimba wakimsindikiza Ulimboka anapoondoka kwenda MOI baada ya MRI. Yaan, weacha tu! Mi sijui kinachofuata. Nahisi harufu ya panya aliyekufa juzi. Serikali inaelekea imehusika, sababu yasemekana mtu mmoja alimpigia simu wakutane, halafu walipokutana wengine wakawa wanaongezeka na ghafla akafungwa kitambaa usoni na kuanza mikong'oto na mapanga. Ati wanaulizana,"tumchome sindano ya sumu nini, au tukamtupe barabarani aonekane kakanyagwa na gari?" Baadaye wakamwacha wakidhani kafa.

Wakati anafikishwa Muhimbili, mwandishi mmoja wa habari akanaswa anaongea kwenye simu, "Aisee hajafa yule jamaa bwana, yuko hai ndio kaletwa hapa sasa hivi, tulikosea mahali fulani" Waliokuwapo jirani wakamrukia kama nyuki na kumpa kichapo karibu afe kama sio wasalama wa Muhimbili kumdaka na kuondoka naye, lakini suti yake nyeusi ikiwa nyang'anyang'a.

Habali ndo hiyo.
 
ulimboka kasema ni CCM
mtu yeyote anaweza kukupa kichapo halafu akasema yeye ni CCM. Hizi ndio mbinu zinazotumika na wapinzani, CDM wameweza kuuwa wenzao itakuja kuwa huyu doctor?
 
"sasa kunakila sababu ya kuingia barabara barani liwalo na liwe" tweet FB haya maneno kwa mwenzako leo ulimboka kesho mgaya, keshokutwa Makene, Mtondogoo slaa na wenginewe the time is now........
 
serekali wala haihusiki na hilo tukio, hili jambo limesha kuwa la kisiasa na njia moja nzuri ya kuichafua serikali ni kufanya vitendo kama hivi, hii itakuwa ni CHADEMA.

Ukiruhusu akili ndogo iitawale akili kubwa ni jambo la hatari sana.
 
Umeongea vema jemedari wangu,kwangu mimi sina sababu ya kumumunya maneno,hii ni njama ya serikali.Lakini kama serikali yetu imefikia hatua ya kutatua migogoro kwa njia hiyo,na wananchi ambao tumeipa serikali madaraka tumekaa kimya,natamani nisingezaliwa tz,watu wamekosa moyo wa uthubutu. Kwani lazima tufike 2015.Nyie viongozi wa upinzani hasa cdm ambao ndio jicho letu,sikio letu na midomo yetu,kwanini msituambie wananchi nini cha kufanya kabla ya 2015.Amani ambayo ccm imekuwa ikitumia miaka nenda rudi kuwahadaa wananchi iko wapi. nasikitika
 
Kweli watu wamedhamiria!Wameenda mahakamani wameona pagumu iliyobaki tuu huyu mwenyekiti!Kuna viongozi wapo kwenye utawala huu hawaitakii mema nchi hii kwa 100%.Yani wanata vita itokee tu!
 
Wataweza kuua mwili tu, lakini ROHO iko salama, na mwenye kuamua ukomo wa maisha wa mtu ni MUNGU na wala sio Mwanadamu, kwetu sisi hio ni changamoto tu, wote tutakufa na hata hao wauwaji watakufa, suala ni muda tu. MUNGU ninaemwamini na kumtumikia atamponya tu. Amen
 
This is going too far now. Serikali inashindwa kutatua matatizo madogo kama haya, na kuamua kuwatumia wanausalama kuangamiza wahanga wa ubovu wa serikali yao...
 
Mungu amponye, na surely wamefanya a wrong move
 
Habari nilizozipata punde kutoka kwa mtu wangu wa karibu na wakuaminika ni kwamba Dr. Ulimboka amemtambua mtu mmoja kati ya watatu waliomteka akiwa kitandani MOI, huyo jamaa ni afisa usalama alievaa kiraia na kujifanya mwandishi wa habari kwenda kuhakikisha kama kazi waliotumwa ya kumaliza Ulimboka imekamilika ndipo Ulimboka alipomtambua na Madaktari kuweka zana zao za kazi chini na kuanza kumshughulikia kikamilifu kama mbwa mwizi mtu alie husika na mateka ya Ulimboka....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…