Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Nimeiona pia kenye Nipashe sasa hivi online, ipo kama breaking news

Wednesday Jun 27, 2012


BREAKING
NEWS »
Dk. Ulimboka akimbizwa hospitali
Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini Tanzania Dk.Steven Ulimboka amefikishwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), akiwa mahututi baada ya kuokotwa eneo la Mabwepande.
 
ni afadhali ningekuwa mfanya maamuzi ningekuwa natoa maamuzi ya msingi wala isingefikia huku ilikofofikia leo
hii tunaongelea masuala ya watu kutekwa.kwani madai ya madaktari yote yapo ndani ya uwezo wa serikali.

Unataka kusema serikali haina uwezo wa kununa scanner au vifaa?kuwapa madr green cards za bima,mbona wanawapa
mpaka mahouse girl wao?,hawawezi kuongeza posho ya wabunge na madiwani zinatoka wapi au kwa sababu ni
wanasiasa watapiga kelele juu ya uovu wao?,

pesa zinazotumika kukimbiza mwenge nchi nzima mbona ni nyingi,
je tuna sababu ya kukimbiza moto kwa mabilioni ya pesa badala ya kuwalipa madaktari...........!!!!!!!.think twice!!

umetoka nje ya mada...., kwahiyo haya niliyosema yanatosha!
 
Khaaa serikali yetu inaufinyu wa mawazo na kwahili wameongeza matatizo na sio kutatua wala kupunguza tatizo. Watanzania tuamuke na tusimame kidete ktk hili!
JINSI YA KUMSINGA (massage) na KUMSUGUA (scrub) MWENZA WAKO KWA KUTUMIA VITU ASILIA.
Binadamu wote lazima tuchoke wakati fulani na kupata maumivu ya viungo vya miili yetu.Basi si kila siku tuwe tunakimbizana kwenye massage spas,siku moja moja unatakiwa umsugue na kumsinga mwenzio nyumba.




















Oga vizuri kabla ya kuanza, shughuli hii inaweza fanywa kitandani au kwenye mkeka. Unaanza kuusugua mwili wote kwanza kwa kutumia unga wa liwa ulichanganywa na maji ya rose pamoja na machicha ya nazi au unga wa manjano uliochanganywa na maji ya rose pamoja na machicha ya nazi. Sugua mwili mpaka uhisi uchafu na nongo zote zimeisha.Baada ya hapo unaoga nakurudi kwa ajili ya kusingwa.Unachukua mafuta ya mzaituni,ya nazi au ya ufuta unampaka mwili mzima na kuanza kumsinga(kummassage) taratibu na kwa upendo alafu unachukua unga wa karafuu na kuunyunyuzia mwilini sana sana sehem za mgongoni na kiunoni(unga huu usiguse sehem za siri,unawasha).Utaendelea kumsinga mpaka utakaporidhika unamuacha akae na ule unga kama dakika 15 hivi,akipitiwa na usingizi muache apumzike akiwa macho*akaoge au ukamuogeshe alafu kitakacho fuata I.T.V hatutaki kujua..........


Kusugua na kusinga mwili inasaidia kuondoa uchafu mwilini,kupunguza maumivu makali mwilini,inakufanya upate pumziko na kuondoa usongo wa mawazo , kutaiwezesha mishipa ya damu kuwa katika hali nzuri na hivyo kurahisisha msukumo wa damu katika mwili wako.Pia huleta furaha kwa wale wawili wapendanao.

MAHITAJI NI KAMA YA FUATAYO



MACHICHA YA NAZI


UNGA WA KARAFUU


UNGA WA LIWA

*MAFUTA YA KARAFUU




*UNGA WA MANJANO

*MAFUTA YA MZAITUNI

MAJI YA MAUA WARIDI

Nyongeza: kwenye swala la mafuta unaweza tumia mafuta ya nazi,ya ufuta au yoyote yale ambayo hayataleta mchubuko wakati wa kusinga. Kusugua na kusinga inaweza chukua dakika 45 mpaka 60 na baada ya hapo pumzika kiasi kisha unaweza kwenda kuoga. Wataalam wanashauri baada ya kuoga utembee kidogo ili kuuweka mwili sawa kabla ya kwenda kulala.

Mafuta ya karafuu unaweza yatumia peke yake*kuchua sehemu zenye maumivu makali*kama kiunoni,shingoni,mgongo na miguu.

KWA ATAKAE HITAJI UNGA WA LIWA,MANJANO NA KARAFUU, MAJI YA ROSE NA AINA MBALIMBALI ZA MAFUTA YA KUSINGA KARIBU SANA DUKANI KWANGU*EmC's CHOICE SINZA MAPAMBANO 0654450200
Evelyne Michael at 4:49 AM
Share

0 comments:
Post a Comment
›
Home
View web version
About Me


Evelyne Michael
I am a Zigua from Tanga,Tanzania.The first born in a family of five children.I am a holder of Bacherol of Law Degree and a Postgraduate Diploma in Human Reso

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

sasa hii ni jf dokta,MMU au siasa.?
 
"Solidarity forever...." nimeunganishwa kwenye simu madaktari wanaimba wakimsindikiza Ulimboka anapoondoka kwenda MOI baada ya MRI. Yaan, weacha tu! Mi sijui kinachofuata. Nahisi harufu ya panya aliyekufa juzi. Serikali inaelekea imehusika, sababu yasemekana mtu mmoja alimpigia simu wakutane, halafu walipokutana wengine wakawa wanaongezeka na ghafla akafungwa kitambaa usoni na kuanza mikong'oto na mapanga. Ati wanaulizana,"tumchome sindano ya sumu nini, au tukamtupe barabarani aonekane kakanyagwa na gari?" Baadaye wakamwacha wakidhani kafa.

Wakati anafikishwa Muhimbili, mwandishi mmoja wa habari akanaswa anaongea kwenye simu, "Aisee hajafa yule jamaa bwana, yuko hai ndio kaletwa hapa sasa hivi, tulikosea mahali fulani" Waliokuwapo jirani wakamrukia kama nyuki na kumpa kichapo karibu afe kama sio wasalama wa Muhimbili kumdaka na kuondoka naye, lakini suti yake nyeusi ikiwa nyang'anyang'a.

Habali ndo hiyo.
 
ulimboka kasema ni CCM
mtu yeyote anaweza kukupa kichapo halafu akasema yeye ni CCM. Hizi ndio mbinu zinazotumika na wapinzani, CDM wameweza kuuwa wenzao itakuja kuwa huyu doctor?
 
"sasa kunakila sababu ya kuingia barabara barani liwalo na liwe" tweet FB haya maneno kwa mwenzako leo ulimboka kesho mgaya, keshokutwa Makene, Mtondogoo slaa na wenginewe the time is now........
 
serekali wala haihusiki na hilo tukio, hili jambo limesha kuwa la kisiasa na njia moja nzuri ya kuichafua serikali ni kufanya vitendo kama hivi, hii itakuwa ni CHADEMA.

Ukiruhusu akili ndogo iitawale akili kubwa ni jambo la hatari sana.
 
Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI
‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous'
Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.
Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa 'agente provocateure' kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all'
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.
Umeongea vema jemedari wangu,kwangu mimi sina sababu ya kumumunya maneno,hii ni njama ya serikali.Lakini kama serikali yetu imefikia hatua ya kutatua migogoro kwa njia hiyo,na wananchi ambao tumeipa serikali madaraka tumekaa kimya,natamani nisingezaliwa tz,watu wamekosa moyo wa uthubutu. Kwani lazima tufike 2015.Nyie viongozi wa upinzani hasa cdm ambao ndio jicho letu,sikio letu na midomo yetu,kwanini msituambie wananchi nini cha kufanya kabla ya 2015.Amani ambayo ccm imekuwa ikitumia miaka nenda rudi kuwahadaa wananchi iko wapi. nasikitika
 
Kweli watu wamedhamiria!Wameenda mahakamani wameona pagumu iliyobaki tuu huyu mwenyekiti!Kuna viongozi wapo kwenye utawala huu hawaitakii mema nchi hii kwa 100%.Yani wanata vita itokee tu!
 
Wataweza kuua mwili tu, lakini ROHO iko salama, na mwenye kuamua ukomo wa maisha wa mtu ni MUNGU na wala sio Mwanadamu, kwetu sisi hio ni changamoto tu, wote tutakufa na hata hao wauwaji watakufa, suala ni muda tu. MUNGU ninaemwamini na kumtumikia atamponya tu. Amen
 
This is going too far now. Serikali inashindwa kutatua matatizo madogo kama haya, na kuamua kuwatumia wanausalama kuangamiza wahanga wa ubovu wa serikali yao...
 
Mungu amponye, na surely wamefanya a wrong move
 
Habari nilizozipata punde kutoka kwa mtu wangu wa karibu na wakuaminika ni kwamba Dr. Ulimboka amemtambua mtu mmoja kati ya watatu waliomteka akiwa kitandani MOI, huyo jamaa ni afisa usalama alievaa kiraia na kujifanya mwandishi wa habari kwenda kuhakikisha kama kazi waliotumwa ya kumaliza Ulimboka imekamilika ndipo Ulimboka alipomtambua na Madaktari kuweka zana zao za kazi chini na kuanza kumshughulikia kikamilifu kama mbwa mwizi mtu alie husika na mateka ya Ulimboka....
 
Back
Top Bottom