Hivi huko MOI nako si kuna mgomo au?? Yeye amepokelewa kama nani (mgonjwa wa kawaida kama wananchi wengine tulionyimwa huduma au yeye ni spesheli??)
Double standards all the way............
Pole Dr. Ulimboka ila yawezekana pia watekaji walitaka kuona je huyu Dr. Ulimboka akipata shida inayohitaji matibabu atahudumiwaje kipindi cha mgomo!? - Just speculating
Una ushahidi gani kuwa ni serikali ndio imetenda hili jambo?Duh! Maskini ya Mungu!!! Hii Serikali ya wauaji...Inatisha sana. Halafu watu wanasema tutumie majina yetu ya kweli hapa JF!!! Mnaona jinsi Serikali hii inavyoweza kabisa kumaliza uhai wako kwa kuandika ukweli jinsi ambavyo imeshindwa kukidhi matumaini mbali mbali ya Watanzania...Sasa kila atakayeipinga ajue maisha yake yako hatarini anaweza kabisa kukolimbwa!!! Pole sana Ulimboka na madaktari wengine wote kwa tukio hili la kusikitisha na kutisha.
Hii ni hatari sana, lazima mtoto wa mkulima atueleze kauli yake "NA LIWALO NA LIWE" ilikuwa na maana gani!
Hao madaktari waliofanya mgomo ilipaswa wananchi tuchukuwe sheria mkononi tukawape kichapo kama tunavyowapa vibaka. Tukiwatandika wawili watatu wengine watarudi kazini au wataacha kabisa udaktari.
Serikali hawa ndio wakuwashughulikia ipasavyo. Sasa fungeni madai yao yote, wakatafute pa kufanya kazi. Na wote wanaogoma wasiruhusiwe kufanya kazi za udaktari hata private hospitals.
kwa sababu gani?hapa lazima m2 ajihudhuru,si mtu tu,mtu mkubwa
Una ushahidi gani kuwa ni serikali ndio imetenda hili jambo?
Bwana Yesu Mwenyewe alisema "auwaye kwa upanga atakufa kwa upanga"!!!ila wahusika wa hili jambo watambue kuwa KILA NAFSI ITAONJA MAUTI
Mkuu wangu coby,
Ni kweli katika tasnia za ukachero si busara hata kidogo kupuuza uwezekano wa aina yoyote katika jambo kama hili. Hata hivyo, labda tu nifanye usahihisho ili kuweka rekodi sawa. Suala la serikali kufanya jambo kama hilo si tu kwamba ni la kitoto bali ni jambo la hatari kuliko hatari yenyewe. Hivyo basi, pamoja na ukweli kwamba serikali inaweza kufanya jambo la kitoto lakini sizani kama inaweza kufanya jambo la hatari kama hilo ambalo madhara yake kwa taswira ya serikali ni makubwa mno. Ni serikali chache sana, ambazo hususani ni za kidikteta wa wazi ndio wanaweza kufanya jambo kama hilo.
Labda niongeze possibility nyingine katika mambo kama haya. Hata wananchi wa kawaida wanaweza kufanya alichofanyiwa Ulimboka. Just imagine, mtu amepeleka ndugu kipenzi halafu akafa kwa kukosa huduma huku yeye akiamini kwamba pamoja na kwamba madaktari wana madai lakini sio busara kwao kuacha watu wanakufa. Mtu au watu wenye mawazo kama hayo wanaweza kumtendea mbaya Ulimboka kama njia ya kulipiza kisasi.
Na wengine wanaweza kutaka kutoa ujumbe kwa Ulimboka na wenzake waone uchungu wa kuuguliwa....! Wahenga wanasema, ukitaka kujua kifo kachungulie kaburi!