Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Serikali , TISS siyo wajinga kumteka Ulimboka na kumfanya hicho na kumuchia. Wamefanya mengi bila hata kujilikana. Wangetaka kumteka na kumpiga wangefanya hivyo wakati mgomo haupo.
MAT ina viongozi / kamati , kwa hiyo siyo rahisi kwa Ulimboka kwenda peke yake kwenye mkutano wowote ule.
Lazima tuseme ukweli kuwa wanaopata madhara ni wananchi .
Kama kuna mtu kapoteza mpenzi wake, mzazi wake atakuwa na hasira gani?
 
Mda mfupi ujao atahamishiwa hospital ya mikocheni..NI MAJONZI
 
Kuna kila dalili serikali itakuwa imehusika moja kwa moja, na imefanya hivyo kwa kufikiria yafuatayo

Kutumia Uzoefu wao wa Huko Nyuma
Serikali imewahi kufanya vitendo kama hivyo siku za nyuma kulipowahi kuwa na migomo ya Wanafunzi. Waliwahi kumteka Raisi wa wanafunzi wa chuo kikuu UDSM Bwana Bazigiza na katibu wake, na kumpa mateso kwa siku 21 wakaja kumwachia siku ya graduation baada ya wanafunzi wengine kutangaza wasingeshiriki kwenye sherehe hizo mpaka Rais wao aonekane. Hawana wasiwasi kuwa wananchi wanaweza kufanya chochote dhidi ya matendo kama hayo kwa sababu hawajawahi kufanya hivyo hata mara moja


:

Umesema vema mkuu. Nakumbuka wakati wa miaka ya mwishoni mwa 80, kulikuwa na mgomo pale UD na mwanafunzi wa Engineering alichinjwa akiwa chumbani kwake pale Hall 2 akafa.

Ilisemekana sana tu kwamba Usalama wa Taifa walihusika. Kuna wakati jamaa wa Usalama wa Taifa alikamatwa akijichanganya na wanafunzi kwenye mgomo, na wanafunzi wakataka kumsulubu vibaya sana.

Alipiga risasi hewani lakini wanafunzi bado hawakuogopa, akaokolewa na baadhi ya viongozi wa Daruso. Na pia mgomo uliofuata Raisi wa serikali ya Wanafunzi wakati huo aliyekuwa mstari wa mbele kwenye harakati za madai ya wanafunzi, Harun Kimaro, ambaye alikuwa akisoma Muhimbili Campus wakati huo, alionywa kwamba maisha yake yalikuwa hatarini na baadhi ya watu wa Usalama wa Taifa ambao hawakumpenda Mwinyi (Mwinyi alikuwa akiwa-ignore maofisa wa usalama wa Taifa wa enzi za Nyerere akawa akitumia wa kwake na ikaleta mgawanyiko kati ya maofisa wa Usalama wa Taifa).

Harun Kimaro ilibidi atorokee Zimbabwe na akamalizia masomo yake huko. Hakurudi rasmi tena Tanzania akaishia kufia ugenini Zimbabwe (ikisemakana akiwa na uhusiano wa karibu na chama cha MDC!)
 
Hizo si taarifa rasmi. Rasmi zinaenda kwa maandishi.
 
There are currently 1936 users browsing this thread. (352 members and 1584 guests)

Mie nina ugomvi na guests hawa......hawa ndo wanatuteka kisha wanasikilizia wananchi tunasemaje. Waone.....hapa wabunge kibao na blackberry zao.
 
Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI
‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous'

Source
 
Pole Dr. Ulimboka.. Wana JF naona kila member anakuja na conclusion yake hapa.. Cha muhimu kila moja ni kuungana na kupinga matukio ya kuwapiga wenzetu.. Tusubiri uchunguzi wa Polisi (japo credibility yao ina shaka).. Kama Dr. Ulimboka aliwasiliana na huyo engineer wa utekaji basi itakuwa rahisi kupata namba ya simu ya huyo jamaa.. Na hata ikitokea akaitupa hiyo simu bado itakuwa rahisi kwa Polisi kugundua kwa kupitia imei ya simu husika.. Hakuna sababu ya wao kushindwa kugundua who's behind this barbaric act..
 


Sheria itumike. Serikali imefata sheria, kwenye mgogoro inatakiwa uende kwenye vyombo vya sheria, vyombo vya sheria vimesitisha mgomo na vimetowa amri, bado unaleta ukaidi?

Sasa ataijuwa Serikali ni nini, ingawa yeye kwa gonjwa linalomsumbuwa anaona kuwa hana cha kupoteza, lakini hii itakuwa ni fundisho kwa wengine wajuwe kutumia sheria na kuheshimu mahakama.


nakushangaa sana, leo unaona sheria zinavunjwa heee?
Mbona kwenye sakata la uamsho haukuse wana vunja sheria?
 
We punguani nlichosoma mimi kinahitaji akili mara kumi ya akili inayohitajika huko medicine(what i earn in a month ..hao Madoctor inawihataji 1 year and a Half kufikia)...

Kuwa Doctor hakukufanyi usiwe kilaza ..hawa madoctor si wanawafanyia watu opresheni za kichwa wakati walitakiwa wafanye opresheni za miguu ?...

Pia katika mgomo uliopita waliwakejeli wananchi badala ya kuwahudumia wakakata roho mbele yao! sasa hawa madoctor kama sio vilaza ni nani ? for your record ,na wewe ni kilazaaaaaaaaaaaa

Acha ndoto za mchana kujifariji hapa JF wakati unaishi chini ya dola moja kwa siku...ten times kitu gani wewe
 
kuna kiongozi mmja alikuwa anaitwa dr kombe kama sikosei naimbieni nimelisahau jina .serikali ilimfuatilia toka DSM NAKWENDA KUMUULIA MOSHI MJINI TOKA dsm mkewe akakimbilia kwenye mahindi .nikumbusheni
 
hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwa sababu hapumui vizuri,

Kweli tumefikia hatua hii!
 
Ati Naibu Spika anamuuliza Kiwia kama anauhakika na hilo!
 
Back
Top Bottom