Tunamshauri tu msanii aepuke matatizo yasiyo ya lazima. Mnamshangilia sasa, kuumia ataumia mwenyewe wala hamtakuwepo. Kwa nini mnamdanganya mtu. Si ukae kimya tu. Lazima uchangie? Msimjibie acheni ajibu mwenyewe. Kama wenzako wanakwazika yeye kula hata nyama, Mtume Paulo alisema "Sitakula nyama kamwe". Namfahamu Kipanya. Ni msanii mzuri, mshereheshaji mzuri ni mwezeshaji mzuri wa masuala ya kijamii. Bora angeiweka sanaa yake ku-address masuala mengi ya kijamii na maendeleo. Aiweke kuelimisha jamii juu ya mambo mengi tu yenye tija kuliko mapambano ya kisiasa. Kuna maeneo mengi ya kuiweka sanaa yake hiyo adimu. Kwa mfano anaweza kuwafikia vijana walio na vidonda katika nafsi zao na kutumia sanaa ya uchoraji kuwaletea uponyaji (psycho-social healing). Hiyo imefanyika Ethiopia, Uganda na mahali pengine. Kupambana kisiasa kwa Msanii wetu si mahala pake. Tunamshauri aipeleke mahali panapofaa zaidi. Sio kwenye siasa. Sanaa za kisiasa awaachie wasanii wa kisiasa. Yeye amekwisha jitambulisha na jamii yetu kuwa ni msanii wa kimaendeleo.