Kipato cha Tsh. 3000 kila siku ni poa au napoteza muda na nguvu?

Kipato cha Tsh. 3000 kila siku ni poa au napoteza muda na nguvu?

Weka 1000 kila siku, na ufanye kazi hapo Kwa miaka mitatu utakuwa na akiba ya sh.1,095,000


  1. Kiasi unachowekea kila siku: Tsh 1,000
  2. Idadi ya siku kwa mwaka: 365 (tukizingatia bila miaka ya leap)
  3. Miaka: 3

Kwanza pata kiasi unachowekea kwa mwaka:


1,000 \times 365 = 365,000


Sasa zidisha kwa miaka 3:


365,000 \times 3 = 1,095,000
Kidding😜
Muachage utoto jamni 😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Piga kazi kuliko kukaa bure, safari moja huanzisha nyingine... Unaweza ukajitengenezea connection zako huko huko, who knows?...

Mimi niliwahi kukaa sehemu nikawa nalipwa elfu tano kwa siku, hiyo ni nauli pamoja na kula asubuhi na jioni, mchana unakula ofisini, mwezi wa kwanza ulikua mgumu ila baadae nilisoma mchezo wa pale ofisini Kila siku nikawa sitoki bila afu 30 or 20 halali katika mfuko wangu.

Ingawa hayo yote yanategemeana na aina ya kazi unayofanya lakini pia location uliyopo imechangamka kiasi gani (Mimi location ilikua ni kariakoo, ofisi ya designing and branding), mambo ya kina Poor Brain

kwahiyo kuna wakati hata anaekuajiri anajua kwamba ukikaa kwenye ofisi yake haukosi hela ya ziada ila hakwambii moja kwa moja.
Mkuu niunganishe sasa na mimi nifanye kazi kariakoo unajua mpaka sas anashangaa naishi ishi tu hata pesa sijui natoa wapi ila.najikuta nalipia frem .. chumba changu cha kuishi na chumba cha kukaa mtu wa kulinda vtu vyangu...

Nashangaaa sana pesa natoa wapi
 
Najua unafanya kwakua hujapata kazi nyingine na ukaona kuliko kukaa bure ni bora ujishughulishe, kwanza nakupongeza kwa kutokukubali kukaa bure unaweza ukawa unapata hela ndogo lakini kupitia hapo ukapata connection nyingine tofauti na ungejifungia ndani.

Sasa nikikwambia ni utoto alafu sina msaada wa kukupa kazi nyingine itakua nakupoteza zaidi, we endelea kufanya huku unapambana kuangalia njia nyingine.
 
Kuna watu wanalipwa 500,000 kwa siku na haiwatoshi..
Pesa kuwa nyingi au ndogo inategemea matumizi yako..
Usikurupuke kudharua kitu ulichonacho kwa matamanio ya kitu ambacho huna bado
 
Kuna watu wanaweka mkuu amini, Tena anaweka ndani ya miaka mitano!
Acha bana 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 acha.mkuu
😂😂😂😂😂 Tuishie hapa kwa leo kaka imetosha bana 😂😂😂😂
 
Mkuu niunganishe sasa na mimi nifanye kazi kariakoo unajua mpaka sas anashangaa naishi ishi tu hata pesa sijui natoa wapi ila.najikuta nalipia frem .. chumba changu cha kuishi na chumba cha kukaa mtu wa kulinda vtu vyangu...

Nashangaaa sana pesa natoa wapi
Si unatoa kwa mshangazi wako Dori 😂😂...

Kwa hapo ulipofikia kuajiriwa utakua unajirudisha nyuma, labda kama utataka uende kwenye hizo office ili ujitengenezee clients wapya na wakudumu.

Coz kariakoo madesigner wengi wanafanya kazi kwa mazoea so wanalipua sana ila ukienda ukawa serious wateja wote wakija wanakufuata wewe, hata usipokuwepo simu lazima ziite na ukihama office wanahama na wewe. (na wewe kwakua unapenda mishangazi basi mashangazi wote wa kariakoo watakua mali yako😂😂... jokes).

Kwahiyo kama utataka hiyo naweza nitakutumia namba za designers wawili watatu mkabadilishana mawazo coz Mimi nimetoka muda sana huko.
 
Bora ujiajir unweza pata ata 10k mkuu apo utotomber uto nunua nguo utovuka popote huu ndo muda wa kurisk huna cha kupoteza pambana hakuna wa kukusave we ndo unatakiwa kusave familia
 
Unajua hiyo elfu 3 wafanya biashara wengi ndio wanayoipata ila kama mtu hu calculate faida yako unakuta unapata 10k kwa siku , nauli 2000 , chakula mchana 2000 usiku 2000 chai buku
 
Usiangalie mlo wa siku moja, angalia mlo wa mwezi mzima na unakula kitu gani.

2000 × 30 = Tsh 60000/- na ukumbuke kuwa siyo kila siku atakula 2000 kuna mda itafika hadi 3000 kwa siku.

. Sasa chukua hiyo 40000 Nenda sokoni kahemee
. Dona ya 10000/- kg 10,
. Mchele 20000/- kg 20
. Maharagwe 5000/-
. Mafuta ya 5000/-

Unabakiza 20000 kwa ajili ya kubadilishia mboga baadhi ya siku, ukichoka kula maharagwe.

Faida
1. ni kula chakula unashiba vizuri kabisa, kuliko kula chakula cha kupimiwa.
2. Pia kuna kiasi cha akili hukua kulingana na kujipikia mwenyewe.
Anapikia nini? Au Pastor Tony yupo?
 
Back
Top Bottom