Kipato cha Tsh. 3000 kila siku ni poa au napoteza muda na nguvu?

Make ifike elfu 30,000 nunua reflector na tengeneza kitambulisho cha kuonyesha wewe ni Afisa Afya wa Halmashauri uliyopo.

Pita maduka ya eneo lako kagua bidhaa zilizopita muda ukiikuta iliyopita muda au iliyopigwa marufuku chukua rushwa sepa.
 
Mnaosema jamaa anafanya kazi yenye maslahi madogo, nadhani hamjui hizi mambo za kukosa kazi. Mimi asisee nilikuwa mtaani tu sina hili wala lile, nikaja kuitwa nikawasaidie kazi kwenye sherehe huko yaani kusevu vyakula aisee nikaliowa 10k nikasema afadhali kuliko kukaa tu bila ramani.
Nikawa kila siku naenda pale kazini ikifika jioni napewa 3k ikawa ndio mchezo wangu kila siku naenda.
Maombi ya kazi nimetuma sehemu nyingi sana lakini nimekosa.
Nikaendelea na kazi ya kusaidia wapishi mpaka boss akatokea kuniamini nikapandishiwa nikawa napokea 5k kwa siku
 
Ni haitoshi ila haihalalishi kuacha kama hauna mchongo
 
Unataka kusemaje?
90K kwa mtoto wa kiume sio mshahara rafiki. Piga hesabu average chakula, kodi, umeme, maji, mawasiliano, hujavaaa, home hawajapiga simu, demu hujamzingatia bado akiba na gharama za dharura zisizotegemewa
 
Uza mishikaki ndugu,au hata karanga au kuwa winga
 
90K kwa mtoto wa kiume sio mshahara rafiki. Piga hesabu average chakula, kodi, umeme, maji, mawasiliano, hujavaaa, home hawajapiga simu, demu hujamzingatia bado akiba na gharama za dharura zisizotegemewa
Unajibana🤣
 
Weka 1000 kila siku, na ufanye kazi hapo Kwa miaka mitatu utakuwa na akiba ya sh.1,095,000

  1. Kiasi unachowekea kila siku: Tsh 1,000
  2. Idadi ya siku kwa mwaka: 365 (tukizingatia bila miaka ya leap)
  3. Miaka: 3

Kwanza pata kiasi unachowekea kwa mwaka:

1,000 \times 365 = 365,000

Sasa zidisha kwa miaka 3:

365,000 \times 3 = 1,095,000
Kidding😜
Hizi hesabu mnazoweka hata gari haliwezi kufanya kazi siku zote hizo bila changamoto yeyote ndio Ije binadamu aisee..
 
Back
Top Bottom