Kipi cha kuanza pindi unapopata ajira: Kuoa, nyumba, biashara au gari?

Mkuu umeuliza kitu kizuri sanaa.. Binafsi baada ya kuajiriwa nilikosea na kujifunza kwamba kuna mambo yanatakiwa uyape kipaumbele kama hujafikia/ kutimiza.
1. Kuwa na makazi. Kama upo single unaweza kujenga ndani ya mwaka mmoja hadi miwili. Hatakama hujamaliza kujenga utakua umefikia umefika hatua flani NB: uwe na lengo moja tu lakujenga.
2. Kuwa na biashara ambayo unauzoefu nayo au unaijua NB: fanya unachokipenda pia nashauri biashara inayoweza kukupa senti kila siku.
NB: Biashara inataka moyo mgumu. Kama uwezi wekeza vingne.
3.Kuoa. Hapa sina comment sana, ila omba mungu akupe mke mwema. Mimi baada ya kuoa mke kila kitu kilivurugika, mke alienda kutoa vitu vya ofini alivunja had kufuri mzee. Omba yasikukute hayo
4. Usafiri. Hii Muhimu sanaa mkuu.. ata kama huna rout nyingi ila kuwanayo muhimu. Unaweza kuwa na pikipiki au Gari (Baiskel iwe kwa ajili ya watoto)
5.Kipaumbele chako. Hii ni uamuzi wako kama unaongeza nyumba au biashara nk
 
Asante kwa deep analysis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…