Kipi kilichomvutia Rais Samia kumpa Biteko Unaibu Waziri Mkuu?

Makonda kama kweli anakubarika kwao,kwanini alikimbilia kugombea ubunge Kigamboni?
Watu kama Makonda wamepitwa na wakati,tena ni bora ale pensheni yake taratibu kwani wapo watu waliumizwa sana na mtu huyo
Makonda hawezi pitwa na wkt km wew sukuma gang yoyote hawezi pitwa na wkt amini usiamini
 
Wenzake ndiyo hawafai bora hata yeye
 
PK na Msoga?? Unajisoma na kujisikiliza lakini?
 
Hii wizara ingesimamiwa na Rais mwenyewe, na ingeshindanishwa na kampuni binafsi za nishati,pia serikali ingewekeza kwenye umeme wa mvuke, jua,upepo alternative energies
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu kwenye madini Kuna mageuzi makubwa lakini mbona mchango wa waziri binafsi ni mdogo sana kwenye hilo jambo? Maana sote tunajua nini kilitokea awamu ya tano ili yatokee hayo uliyosema kulikuwa na nguvu kubwa sana ya maelekezo na namna ya kufanya toka Kwa raisi mwenyewe hivyo yeye kama yeye napata tabu kumpa credit Kwa hilo.
 
siyo kila anayetoka Kanda ya Ziwa anakuwa na Influence kule. A total miscalculation
 
Wasukuma hawana jina la Biteko, Biteko sio msukuma na hawakirishi wasukuma walioko kanda ya ziwa lakini hata waliosambaa maeneo tofauti nchini. Mheshimiwa anampenda kwa sababu chochote akiambiwa kufanya anafanya hata kama ni kibovu ndio maana alisikika akisema "..ujio wangu wizara ya nishati sio kuja kufukuza au kubadilisha mipango iliyopo ila ni kusimamia ufanisi...."

Utasimamiaje ufanisi wa kazi kama watumishi ni wabovu na mipango iliyopo haitekeleza kwa matokeo chanya kadri ya matazamio ya watumiaji umeme?

Je, kuna tofauti gani kati ya MGAO wa UMEME na RATIBA ya kupata UMEME?

Alimkwepa Kalemani kwa sababu yule hayumbishwi na hakubali kupelekeshwa kwa manufaa ya viongozi wa juu. Kalemani alisimamia bei ya umeme ibaki TZ 27,000 na kasi ilikuwa inaenda vizuri na sababu ya bei ya chini ni kwamba kukiwa na wateja wengi wanaoilipa kipato cha TANESCO kilnakuwa kinatabirika lakini bei ya juu utakuwa na wateja wachache, matumizi makubwa huku wengine wakijiiunganishia kwa njia zisizo za uhalali hivyo kusababisha serikali kupata hasara ya mapato stahiki lakini hawalioni wanakazia ndoto za ALINACHA.

Mkumbuke, Biteko ni swahiba mkubwa wa spika aliyetimuliwa isivyo halali J Ndugai ndio maana alimteua kuongoza kamati ya uchunguzi kubaini ni namna gani serikali ilikuwa ikipoteza kipato kwenye sekta ya madini na ripoti yake ndio iliyopelekea JPM akamteua kuwa waziri wa madini.
 
Unazikumbuka kamati za zungu na biteko. Ambazo baadae zilizaa marekebisho madogo ya 2017 ya sheria ya madini ya 2010?
 
Unazikumbuka kamati za zungu na biteko. Ambazo baadae zilizaa marekebisho madogo ya 2017 ya sheria ya madini ya 2010?
Sawa kwenye zile kamati biteko alikuwa Nani na kwenye zile kamati hata terms of reference walipewa na rais
 
Huyu amewekwa ili kutughilb sisi wa kanda ya ziwa lakini tunasema hivi:- HATUDANGANYIKI.
 
HATUDANGANYIKI
 
Ili aonekane anawapenda watu wa Kanda ya Ziwa kwa maandalizi ya uchaguzi 2024 na 2025. Hakuna la maana zaidi ya hilo, hata hivyo ameishia kuwa wa kutumwa kazi na PM.
 
Ili aonekane anawapenda watu wa Kanda ya Ziwa kwa maandalizi ya uchaguzi 2024 na 2025. Hakuna la maana zaidi ya hilo, hata hivyo ameishia kuwa wa kutumwa kazi na PM.
Kama ishu ni Kanda ya ziwa si kampiga chini mabula alafu ni kweli kwamba doto ana ushawishi huo Kanda ya ziwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…