Kanyama, huo ni mtizamo wako kuhusu Biteko, si wote tuna mtizamo wa aina yako.
Kumchaguwa Mrema kipindi kile akiwa waziri wa mambo ya ndani kuwa naibu waziri mkuu kulikuwa na sababu za kiutendaji. Baadhi ya mawaziri wenzake walikuwa wakilalamika kuwa anawaingilia kwenye maeneo yao ya kiutendaji. Alifauru au hakufaulu baada ya uteuzi, hilo ni jambo lingine lakini sababu ya wazi ya uteuzi ilikuwepo. Ni tofauti na unaibu waziri mkuu wa Biteko. Ni sababu hipi kiutendaji kama waziri wa nishati itamzuia kutekeleza majukumu yake bila kuwa naibu PM? Ndiyo maana tunakwambia, uteuzi wake kwenye hiyo nafasi ya naibu PM imekaa kisiasa zaidi kuliko utendaji.
Kuongoza nchi kwa mafanikio kuna tegemea vitu vingi, ikiwemo coordination, taasisi imara, aina ya viongozi wanaokuzunguka, nk nk. Biteko ata kama ni mtendaji mzuri anategemea mfumo uliopo. Kama ni huo mfumo ni mbovu, usitegemee yeye atakuwa bora.
Japo unadai kwamba alirekebisha kwenye madini, lakini nikuakikishie, uko kwenye madini ndiko tunakopigwa fedha nyingi Sana. Mikataba iliyovunjwa kiholela yeye akiwa waziri kipindi cha jpm inatugharimu Sana. Sitaki kugusia maeneo mengine kwenye madini ambako hadi leo ni shida tupu.
Tusikae chini tukabweteka, kwa aina ya viongozi tulionao na mfumo uliopo bado tuna safari ndefu.