Kipi kilichomvutia Rais Samia kumpa Biteko Unaibu Waziri Mkuu?

Kanyama, inavyoonekana wewe ni mpiga debe mwenye mihemko. Na wewe kweli unawadharau wengine kwamba siyo great thinkers? Ni kuulize, kuna uhusiano gani kati ya performance ya Biteko na huo unaibu waziri mkuu? Kwamba nini kingemzuia kuperform hapo nishati bila kuwa naibu waziri mkuu. Nani alimzuia Makamba kuperform hapo nishati ambae dawa yake ni kumpa unaibu Biteko. Hili jambo liko kisiasa zaidi na si utendaji!!
 
Kaka inawezekana siasa zimo lakini ukiangalia zaidi nia ya mleta mada alikuwa na maana hiyo kwamba huko anakotoka hajafanya chochote ukilinganisha na chochote walichowahi kufanya akina Salim Ahmed Salim na marehemu Lyatonga Mrema.
Tujiulize manaibu waziri wakuu waliotangulia walifanya nini very special hasa katika kusaidia jamii ya wakati huo kuweza kujikomboa Kiuchumi?. Inawezekana ilikuwa ni kuruhusu mitumba iingizwe nchini au kuzuia wizi na uchawi?.
Nini walifanya kubadili mifumo ya kuliongezea taifa kipato na kuondoa umaskini wa Watanzania wa enzi zao?.
Mkuu Mbussi huyu kiongozi tumwombeeni kwa Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya njema na maono na Imani ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kumaliza kero za nishati na madini hatimaye zipate mwarobaini.
Wachafuzi wapo na wataendelea kuwepo lakini kama nilivyosema huyu kiongozi ukiwahi kukaa nae karibu kwa saa moja ukamweleza kero yako au ushauri wa nini afanye ili kusaidia jamii ya wengi, ndipo utajua kwamba kuna watu huwa wanazaliwa na karama ya uongozi.
Anasikiliza mtu yeyote, tena kwa makini and he doesn't pretend akiwa anakusikiliza.
Tumpeni ushirikiano na muda tutaona matokeo soon
 
Hii ni ndoto niliyoota usiku wa kuamkia leo Jumanosi!
Simu inaita.....
Ngriii...ngriiii ngriii !

Mimi:Hello!
Simu: Voicer vipi?
Mimi: shwari..nambie Babu!
Simu:....Aisee ni hiviii...
...Kwamba muenendo wa CCM kisiasa nchini kwa sasa 2023.Ni kama ule wa 2015 chini ya Uenyekiti wa JK.Ambapo CCM ilivuma kwa ufisadi na mambo mengi yaliyoifanya kuchungulia kaburi la kisiasa.
Hatimae CCM ikaja na Mbinu ya kugeuzia gia Dodoma na kumsimika Magufuli na karata zikawabeba CCM kupitia "Chagua MAGUFULI".

Naona mtindo huu unataka kujirudia tena 2030.
kwa sababu CCM inaporomoka kwa kasi miongoni mwa Jamii ya wapiga kura wa nchi hii.Ndio sababu
CCM inamuandaa Biteko ili ikibidi waweze kumtumia kama gia ya angani pale Dodoma.2030.
Endapo Kipara wao atabuma!
Biteko anatokea kanda ya Ziwa ambapo ni hazina kubwa ya wapiga kura wa CCM.
Biteko atatumika ili kuwavuta wafuasi wa Marehemu JPM ili kuiunga mkono CCM tena!.

Ulinzi mkubwa wa Biteko
Unatokana na hofu ya
CCM kutokana michezo michafu waliyonayo baadhi ya Wahafidhina ndani ya chama chao.

Hivyo kuhofia kwamba huenda Akaumizwa na lile kundi ambalo linajikusanyia mapesa kwa hila zote ili kuusaka uraisi ifikapo 2030.
Na hivyo kumuona Biteko kama kikwazo chao kikubws Sambamba na ilivyo kwa PM-Majaaliwa.

Lakini pia kuna hofu nyingine kwamba Biteko amepewa wizara nyeti ambayo Marope aliitumia kufanya kila aina ya uozo kujikusanyaia pesa haramu kupitia mikataba ovu yenye harufu za ufisafi kila kona.

Na kwa Biteko kuwa pale ....
Mambo mawili yanaweza kutokea!
Anaweza kuamua....
Moja ni...
kuamua kuwa mshirika wa Kipara baada ya Mazungumzo baina yao na kumuingiza kwenye kundi lao naye Alambe Asali.
Na pili ni...
kukataa mambo yao kina kipara na kuamua kuifumua Tanesco na kuyaanika Madudu yote ya mtangulizi wake.
Jambo ambalo Kipara hataweza kulifurahia.
Sababu litaharibu taswira na ndoto yake kuusaka uraisi wa JMT 2030.

Hivyo wanaweza kutumia njia yoyote kuhakikisha hilo halitokei.
Na hii ndio hasa inaweza kuwa siri ya ulinzi mkali kwa Biteko tunaouona kwa sasa.

U-NAIBU Waziri Mkuu wa Biteko.!
Ni njia pekee ya kuhakikisha anapewa ulinzi wa uhakika dhidi ya makundi yoyote yatakayo kusudia kufanya mchezo wowote mchafu dhidi ya Biteko."
Ghafla nimeshtuka toka Usingizini na kusikia adhana toka msikiti jirani na makazi yangu.......

Sabato Njema!
 
mie nimeona cha ziada alichonacho MWKuu ndugu doto biteko.

Ni kwamba yuko very soft, ukimtumbua akamweka nje ya mfumo hawezi kufurukuta wala hawezi kusumbua. ni rahisi sana kudhibiti, huhitaji nguvu kubwa kumuhandle.

Nionavyo mie Mzee Mpango ataomba kuachia ngazi come 2025, then haka kajamaa katawekwa pale.

Huwez muweka msaidizi wako akawapawaful au muerevu zaidi yako atakusumbua Lazima uweke mtu ambae sio mzito ili uwe juu yake wakat wote.
 
Hata hivyo mkuu mtu kuwa makamu wa rais ndio hadi awe naibu kwanza!? Mbona hata Marais tuliopata kuwa nao huanzia ngazi za kawaida tu mkapa, mwinyi ,kikwete tena wamechukua hizo nafasi wakishindana na mawaziri wakuu wastaafu. Sembuse makamu wa rais!?
 
Kanyama, huo ni mtizamo wako kuhusu Biteko, si wote tuna mtizamo wa aina yako.

Kumchaguwa Mrema kipindi kile akiwa waziri wa mambo ya ndani kuwa naibu waziri mkuu kulikuwa na sababu za kiutendaji. Baadhi ya mawaziri wenzake walikuwa wakilalamika kuwa anawaingilia kwenye maeneo yao ya kiutendaji. Alifauru au hakufaulu baada ya uteuzi, hilo ni jambo lingine lakini sababu ya wazi ya uteuzi ilikuwepo. Ni tofauti na unaibu waziri mkuu wa Biteko. Ni sababu hipi kiutendaji kama waziri wa nishati itamzuia kutekeleza majukumu yake bila kuwa naibu PM? Ndiyo maana tunakwambia, uteuzi wake kwenye hiyo nafasi ya naibu PM imekaa kisiasa zaidi kuliko utendaji.

Kuongoza nchi kwa mafanikio kuna tegemea vitu vingi, ikiwemo coordination, taasisi imara, aina ya viongozi wanaokuzunguka, nk nk. Biteko ata kama ni mtendaji mzuri anategemea mfumo uliopo. Kama ni huo mfumo ni mbovu, usitegemee yeye atakuwa bora.

Japo unadai kwamba alirekebisha kwenye madini, lakini nikuakikishie, uko kwenye madini ndiko tunakopigwa fedha nyingi Sana. Mikataba iliyovunjwa kiholela yeye akiwa waziri kipindi cha jpm inatugharimu Sana. Sitaki kugusia maeneo mengine kwenye madini ambako hadi leo ni shida tupu.

Tusikae chini tukabweteka, kwa aina ya viongozi tulionao na mfumo uliopo bado tuna safari ndefu.
 
Dotto hana influence yoyote Kanda ya ziwa. Dotto amepewa zawadi kwa ulinzi anaendelea kufanya kulinda "Kitalu C" huko Mererani. Kitalu C maarufu kama shimo la mwarabu au Tanzanite One inamilikiwa na Msoga gang. That's all!
 
Dotto hana influence yoyote Kanda ya ziwa. Dotto amepewa zawadi kwa ulinzi anaendelea kufanya kulinda "Kitalu C" huko Mererani. Kitalu C maarufu kama shimo la mwarabu au Tanzanite One inamilikiwa na Msoga gang. That's all!
Tupia kaushahidi mkuu
 
Usipotoshe kamanda. Wakati mabadiliko madogo ya sheria ya madini ya 2017 Yanafanyika Biteko hakuwa waziri. Kumbuka aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati iliyokwenda kuchunguza madini ya Tanzanite ni kwa nini sisi Tanzania tulikuwa exporters wa tatu ukilinganisha na Kenya na India.
Kamati ile ilileta MAPENDEKEZO ambayo yaliiwezesha nchi kufanya reforms kisheria juu ya MDAs(Mining development Agreement) au mikataba kama ulivyoisema. Baadhi ya manufaa yalipatikana achilia mbali leo kupelekwa mahakamani au ndege kukamatwa ni pamoja na 16% FCIs, Madini kuwa mali ya umma tofauti na hapo awali ambapo mwekezaji Alikuwa akipewa leseni ya kuchimba basi madini yanakuwa yake na anaweza kuleta private jet akapaa nayo. Faida nyingine ilikuwa ni 50/50 Profit sharing ktk uzalishaji. Zimezaliwa kanuni za local content ambapo wawekezaji hawa wanalazimika kununua bidhaa na huduma kutoka kwa local suppliers.
Target kubwa ya mwisho ikawa ni umiliki wa uchumi wa madini kwa wazawa kazi ambayo imefanyika kwa kusimamiwa kikamilifu na biteko.
Mkuu inaonekana umekariri kwamba kwenye madini tunapigwa. Taarifa ya waziri wa madini Anthony Mavunde leo alipokuwa anahojiwa na Tbc amesema sekta hii ndio inaleta fedha za kigeni kwa 56% kutokana na mauzo ya madini nje. Mifumo yote hii imeimarika kipindi hiki.
Kwa hiyo kaa kwa Kutulia soon Utaanza kuona mabadiliko
 
Sina shida na Imani yako juu ya Biteko. Nilichosisitiza kwenye comment yako ya awali ni mfumo wa utendaji serikali nzima ndio utakaomfanya Biteko awe mtendaji mzuri. Tena umeeleza vizuri, kwamba reforms ktk Sheria za madini zilifanyika kabla hata Biteko hajawa Waziri. Kwa maana nyingine mifumo ililekebishwa na yeye akaisimamia kwa uaminifu na weledi. Na hii yote ilitokana na mitizamo ya aliyekuwa mkuu wa nchi kwa wakati ule. Ndiyo maana nikakwambia, kwa nchi kama yetu hii ambayo mambo mengi uendeshwa kwa utashi wa Rais, mafanikio ya Biteko yatatokana na mfumo siyo cheo chake kama naibu waziri mkuu. Hivyo kuteuliwa kwake ktk cheo hiki ni jambo la kisiasa zaidi kuliko utendaji.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Sina shida na Imani yako juu ya Biteko. Nilichosisitiza kwenye comment yako ya awali ni mfumo wa utendaji serikali nzima ndio utakaomfanya Biteko awe mtendaji mzuri. Tena umeeleza vizuri, kwamba reforms ktk Sheria za madini zilifanyika kabla hata Biteko hajawa Waziri. Kwa maana nyingine mifumo ililekebishwa na yeye akaisimamia kwa uaminifu na weledi. Na hii yote ilitokana na mitizamo ya aliyekuwa mkuu wa nchi kwa wakati ule. Ndiyo maana nikakwambia, kwa nchi kama yetu hii ambayo mambo mengi uendeshwa kwa utashi wa Rais, mafanikio ya Biteko yatatokana na mfumo siyo cheo chake kama naibu waziri mkuu. Hivyo kuteuliwa kwake ktk cheo hiki ni jambo la kisiasa zaidi kuliko utendaji.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Baki na hoja moja basi ya mfumo usiunganishe zote mkuu. Nimekuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…