TUPAMBANE SANA
Member
- Nov 21, 2018
- 29
- 26
Ni muda sasa tokea Mkandarasi alipomaliza kuondoa udongo wa zamani na kuweka udongo mpya na kushindilia barabara hiyo lakini tokea waliposimama ni muda sasa.
Awali kulisikika kelele au maneno kwamba wamesimama kwa sababu ya mvua lakini wachunguzi wa mambo tumegundua sio mvua kwa maana tokea walipoanza ni muda mrefu na kuna kipindi mvua zilikata na mpaka hivi sasa mvua zimepungua sana na wakati mwingine hakuna.
Pia cha kujiuliza mbona miradi mingine ya barabara za sehemu zingine zinaendelea? Mbona Mradi wa treni nao unaendelea? Je huko hakuna mvua?
Material. Kwakweli nikipita pale Zakhem naona material yote yapo nondo zipo kokoto zipo cement zipo.Swali langu ni kipi kinachelewesha mradi kukamilika? Ni nani anachelewesha? Sasa cha kushangaza baadhi ya sehemu zingine zimenaanza au zimeshaharibika kutokana na magari bodaboda kupita maji kujaa.
Ushauri wangu kwa Mkandarasi siku nyingine ukipata mradi jitaidi kujenga kipande kutokana na mpunga uliotolewa na serikali Mfano kulikuwa kuna haja gani ya kushindilia baadhi ya sehemu kutoka Mbagala mpaka Kariakoo.
Kwanini usinge anza na kipande mfano kutoka Mbagala mpaka pale Msikitini ili kwa kipindi hicho mnachosubiria mpunga utoke watu waanze kutumia kipande hicho kupunguza foleni.