Kipi kimeukumba mradi wa barabara ya mabasi ya mwendokasi Mbagala?

Kipi kimeukumba mradi wa barabara ya mabasi ya mwendokasi Mbagala?

NISHAPITA MKUU ILA KUNA KIPANDE KATI YA ZAKHIEM NA KIZUIANI WAMEANZA KUTANDAZA ZEGE MKUU.NA HADI MUDA HUU NIMEPITA WATU WANAFANYA KAZI
Unao uhakika? Mbona yadi yao imefungwa siku nyingi na hivyo vipande viwili vya zege ni vya siku nyingi, kimoja Kizuiani na kingine Zakhiem.
 
Ccm wasanii sana
Mvua ni nyingi sana imekuwa ikibomoa madaraja na miundombinu iliyojengwa na kinachosubiriwa ni mvua isimame.
Wiki iliyopita kamati ya CCM iliyokagua mradi huo ilisifu maendeleo ya kazi ya ujenzi japo walikusanya watu wachache waonekane wakijenga!

In God we Trust
 
Mbagala hipo sehemu jamani ?

Leo nimegundua kumbe mimi sijuhi vitu vingi !
 
Tumepeleka misaada China kwenye Corona, mtoa mada tuache kwanza!!
 
Kwanini usinge anza na kipande mfano kutoka Mbagala mpaka pale Msikitini ili kwa kipindi hicho mnachosubiria mpunga utoke watu waanze kutumia kipande hicho kupunguza foleni.
AISEE ujinga mzigo hiyo ni barabara ya mwendokasi sio ya magari ya kawaida!! Wewe kweli mkazi wa mbagala.Ingekuwa kimara au mikocheni au mbezi uelewa wao uko juu wanaelewa tofauti ya barabara ya kawaida na mwendokasi ,Lakini mwenzangu wewe wa mbagala mmmmm

AKILI HUENDANA NA MAENEO ANAYOISHI MTU UNA AKILI ZA MBAGALA WEWE
 
Ni muda sasa tokea Mkandarasi alipomaliza kuondoa udongo wa zamani na kuweka udongo mpya na kushindilia barabara hiyo lakini tokea waliposimama ni muda sasa.

Awali kulisikika kelele au maneno kwamba wamesimama kwa sababu ya mvua lakini wachunguzi wa mambo tumegundua sio mvua kwa maana tokea walipoanza ni muda mrefu na kuna kipindi mvua zilikata na mpaka hivi sasa mvua zimepungua sana na wakati mwingine hakuna.

Pia cha kujiuliza mbona miradi mingine ya barabara za sehemu zingine zinaendelea? Mbona Mradi wa treni nao unaendelea? Je huko hakuna mvua?

Material. Kwakweli nikipita pale Zakhem naona material yote yapo nondo zipo kokoto zipo cement zipo.Swali langu ni kipi kinachelewesha mradi kukamilika? Ni nani anachelewesha? Sasa cha kushangaza baadhi ya sehemu zingine zimenaanza au zimeshaharibika kutokana na magari bodaboda kupita maji kujaa.

Ushauri wangu kwa Mkandarasi siku nyingine ukipata mradi jitaidi kujenga kipande kutokana na mpunga uliotolewa na serikali Mfano kulikuwa kuna haja gani ya kushindilia baadhi ya sehemu kutoka Mbagala mpaka Kariakoo.

Kwanini usinge anza na kipande mfano kutoka Mbagala mpaka pale Msikitini ili kwa kipindi hicho mnachosubiria mpunga utoke watu waanze kutumia kipande hicho kupunguza foleni.
Hivi mbagala mwendokasi ya nini? Wanaweza kuishi kiugumukiugumu!
 
NIMEPITA SASA HIVI MKUU MAENEO HAYO, NAONA UJENZI UNAENDELEA VEMA WASHAANZA KUWEKA LILE BARABARA LA ZEGE KWA BAADHI YA VIPANDE.ANGALIA KWA UMAKINI WATU WANAENDELEA NA KAZI BAADHI YA VIPANDE
Barabara la zege hilo lina zaidi ya mwezi, na ni kisehemu kidogo tu, kama cha mita 50 Hapo zakhiem!! Ki ukweli mradi umesimama, cjui nini tatizo
 
Mwendo kazi hizi zitakuja kuisha Kujenngwa mwaka 20100, sisi tutakuwa tume kula kona siku nyingi.
 
Kwanini usinge anza na kipande mfano kutoka Mbagala mpaka pale Msikitini ili kwa kipindi hicho mnachosubiria mpunga utoke watu waanze kutumia kipande hicho kupunguza fole
Huna utaalam na masuala ya ujenzi unaleta habari ya kufikirika
Ukipita maeneo ya zakhem kuna kazi ya kumwaga barabara ya zege
Tatizo kubwa ni mvua tu,ina ikisimama itabidi wafanye kazi saa24 kuendana na muda
 
Wakati huo tunampiga vita Zitto kwa kushawishi mabeberu wasitupatie msaada wa fedha[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]


Wakati huo tukipatiwa mkopo wa 3.3 trillion tunasherekea wiki mzima huku tukitembea vifua mbereeee
Usisahau ss no donor kantriii na tunapasaa kutembea kifua mbereeeee

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Back
Top Bottom