Kipi kinafanya wasafiri wengi kupendelea kukaa dirishani wakati wa safari?

Kipi kinafanya wasafiri wengi kupendelea kukaa dirishani wakati wa safari?

Secretly hako ni kamlango ka emergency
It works best both ways too, mkipata side impact au roll over watu wa dirishani ndio wanakuwa wa kwanza kupotea .
Rejea ajali ya abood miaka ya 90 pale bwawani , iligongana na lori liliobeba kijiko, wengi waliokufa walikuwa wamekaa dirishani
 
Ndugu zangu, kwanini wasafiri wengi hupendelea zaidi kukaa dirishani iwe kwenye basi ndege hata meli wakati wa safari?

Kuna watu wakikosa siti dirishani wapo tayari kuairisha safari.


View attachment 2623130
Mimi ni mmoja wapo,kabla sijakata tiketi nasisitiza siti ya pembeni naniione ndo nitoe nauli

Sent from my SM-S920L using JamiiForums mobile app
 
Napenda kukaa dirishan kwa sababu ya kufungua dirisha nipate upepo yaan sipedi dirisha lifungwe kabisa huwa naona kama hewa haitoshi
Sasa ukute mtu dirishan na hafungui dirisha tunakosana kabisa
 
Ndugu zangu, kwanini wasafiri wengi hupendelea zaidi kukaa dirishani iwe kwenye basi ndege hata meli wakati wa safari?

Kuna watu wakikosa siti dirishani wapo tayari kuairisha safari.


View attachment 2623130
Binafsi nikisafiri sipendi kukaa na watu, nakaa VIP na kama ikitokea nakaa na watu nakaa dirishani ili nipumue vizuri (fresh air) kwani sipendi harufu ya mdomo ya watu na kikwapa ambayo hapa Tanzania ni fashion kunuka sehemu za siri, makwapa na mdomo.
 
Napenda sana kuangalia na kuutafakari uumbaji wa Mungu ninapokuwa ninasafiri,kwahiyo napendelea zaidi dirishani....
 
Kukaa siti zilizo koridoni(sijui tuiite hivyo?) la basi ni kero.Kila anayepita mara nyingi lazima akubamize na mizigo au sehemu ya mwili.Na ikitokea usafiri umezidi watu wengi,waliosimama hawakawii kukuegemea ili apate stance nzuri.Kwangu ni kero.
Vilevile,msafiri aliyekosa siti na akakosa sehemu ya kuweka mizigo yake ujue atakubebesha.Hata mtoto atakupa ubembeleze.Hapo ndipo huwa sitaki siti za koridoni isipokuwa dirishani.
 
Kama nikiendaga mikoa ya mbali napenda kukaa dirishani kuangalia mademu wakila mkoa Aswa nikianza kuiacha Dodoma kuelekea singida kuna totozzz
 
Back
Top Bottom