Wanabodi
Nijitambulishe tena na tena, kuwa japo mimi Paskali Mayalla, ni mwandishi tuu wa Habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na mtangazaji wa kujitegemea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea, hivyo kupitia uasanasheria wangu, nina mamlaka ya kuikosoa mahakama kwa kutotenda haki, na nimekuwa nikiandika sana makala kutoa elimu ya katiba, sheria na haki kupitia safu yangu ya kwa Maslahi kwa Taifa, sasa safu hii haishii kuandika tuu magazetini na mitandaoni, safu hii sasa inakwenda hatua moja mbele, inakwenda hewani kupitia kipindi cha TV cha "Kwa Maslahi ya Taifa", kitakuwa kinarushwa hewani kila siku za Jumapili Saa: 3:00 usiku na marudio siku za Jumatano Saa 9:30 alasri kupitia Channel Ten, ni kwa kuanzia tuu, baadae kipindi hiki pia kitarushwa na TBC, ITV, Star TV, na Azam TV, ili elimu hii ya Katiba, Sheria, Haki na Wajibu, iwafikie Watanzania wengi zaidi.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=uSiW3_dfU58l3B-V
Kipindi cha kwanza ni mahojioano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Elieza Mbuki Feleshi kuhusu uwezo wa Mahakama zetu kutenda haki.
Siku za nyuma niliandika makala 5 mfululizo za kilio cha Haki, na miongoni mwa hoja zilizoniibua kumtafuta Mwanasheria Mkuu, Jaji Feleshi, ni baada ya moja ya makala hizo ku challenge uwezo wa Mahakama zetu kutoa uamuzi wa haki.
Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
Mtamsikia wenyewe AG, Jaji Feleshi akijibu, ila hii hali ya Mahakama zetu kutotenda haki kwa kitu kinachoitwa legal technicalities, kinaendelea! na mfano mzuri wa haki kutotendeka kwa legal technicalities ni hii hukumu ya kina Halima Mdee na wenzake 18!
Paskali.