Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
-
- #61
Kuna jinai za aina mbili, jinai za public na jinai za private, jinai za public ni polisi wakisikia tuu taarifa za kiinteligensia wanaingilia kati wenyewe, ni jinai against public. Na jinai za private ni zile jinai against private entities kama wizi, ubakaji, forgery mhusika ni lazima uripoti polisi ndipo uchunguzi ufanywe!.Ndiyo utaratibu? polisi wanasubiri maelekezo toka juu, kesi ya Lissu wanasubiri apone atoe ushahidi sijui angekufa kusingekuwa na uchunguzi.
Na issue ya Lissu wanasubiri nini? angekufa?Kuna jinai za aina mbili, jinai za public na jinai za private, jinai za public ni polisi wakisikia tuu taarifa za kiinteligensia wanaingilia kati wenyewe, ni jinai against public. Na jinai za private ni zile jinai against private entities kama wizi, ubakaji, forgery mhusika ni lazima uripoti polisi ndipo uchunguzi ufanywe!.
Hili sakata la hawa wabunge, Chadema wanasema tuu kuna forgery lakini hawajaripoti popote ili uchunguzi wa kijinai ufanyike, sababu ya Chadema kutoripoti polisi, mimi naijua ila naomba nisiiseme for now!.
P
Hiyo tenda ya kurusha kipindi wameipataje? CCM iliipata chaneli 10 kwa mtindo wa nipe nikupe, haram.Mkuu Hismastersvoice, kwanza asante kuchangia uzi wangu
It's true, Channel Ten ni kituo cha TV, mali ya CCM, hivyo CCM ni chama kinachowajali Watanzania, hiki kipindi ni kipindi cha kuwasaidia Watanzania, kwa kuwaelimisha elimu ya katiba, sheria na haki hivyo kulisaidia taifa.
P
Issue ya Lissu, wameshindwa kwasababu wahusika sio watu wasiojulikana bali ni watu 'wasiojulikana' Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana na pia nikashauri wale wenye uwezo wajitolee kusaidia WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?Na issue ya Lissu wanasubiri nini? angekufa?
Unapokuwa ni mhitaji wa kusaidiwa kitu fulani, akitokea msamaria mwema kukusaidia, wewe jukumu lako ni kushukuru, na sio kuhoji msaada umetoka wapi na umepatikana vipi!.Hiyo tenda ya kurusha kipindi wameipataje? CCM iliipata chaneli 10 kwa mtindo wa nipe nikupe, haram.
Kwenye news na show business, prominence na big names makes news, Kwenye National hierarchy ya JMT, baada ya Rais, VP na PM, anafuata Spika na CJ. Hivyo huyu ni mtu muhimu na Mkuu wa mhimili. Kipindi cha kuzungumzia maslahi ya taifa bila Serikali, Bunge na Mahakama hakina maana.Nilikuwa nakuunga mkono ila ulipomtaja Tulia Akson nikaona kipindi hakina maana.
Labda uwe unachanganya na mchiriku huenda tutaangalia hasa kwenye biti za mchiriku.Unapokuwa ni mhitaji wa kusaidiwa kitu fulani, akitokea msamaria mwema kukusaidia, wewe jukumu lako ni kushukuru, na sio kuhoji msaada umetoka wapi na umepatikana vipi!.
Watanzania ni wahitaji wa elimu ya katiba, sheria na haki, Mwanasheria, Wakili, mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, Pasco Mayalla amejitolea kusaidia kwenye hili, naomba mpokee tuu msianze kuuliza maswali!.
Ni muda mrefu nilishauri humu jf turushe vipindi kwenye mainstream media Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako! angalia nilichojibiwa!.
Naendelea kusisitiza Watanzania tuwe ni watu wa shukrani kwa madogo ili tupatiwe makubwa!.
P
Napokea maoni ya maboresho, hili nimelipokea, kipindi kitaanza na mchiriku, kati tutaweka mchiriku na mwisho tutamalizia na mchiriku.Labda uwe unachanganya na mchiriku huenda tutaangalia hasa kwenye biti za mchiriku.
Wanabodi
Nijitambulishe tena na tena, kuwa japo mimi Paskali Mayalla, ni mwandishi tuu wa Habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na mtangazaji wa kujitegemea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea, hivyo kupitia uasanasheria wangu, nina mamlaka ya kuikosoa mahakama kwa kutotenda haki, na nimekuwa nikiandika sana makala kutoa elimu ya katiba, sheria na haki kupitia safu yangu ya kwa Maslahi kwa Taifa, sasa safu hii haishii kuandika tuu magazetini na mitandaoni, safu hii sasa inakwenda hatua moja mbele, inakwenda hewani kupitia kipindi cha TV cha "Kwa Maslahi ya Taifa", kitakuwa kinarushwa hewani kila siku za Jumapili Saa: 3:00 usiku na marudio siku za Jumatano Saa 9:30 alasri kupitia Channel Ten, ni kwa kuanzia tuu, baadae kipindi hiki pia kitarushwa na TBC, ITV, Star TV, na Azam TV, ili elimu hii ya Katiba, Sheria, Haki na Wajibu, iwafikie Watanzania wengi zaidi.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=uSiW3_dfU58l3B-V
Kipindi cha kwanza ni mahojioano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Elieza Mbuki Feleshi kuhusu uwezo wa Mahakama zetu kutenda haki.
Siku za nyuma niliandika makala 5 mfululizo za kilio cha Haki, na miongoni mwa hoja zilizoniibua kumtafuta Mwanasheria Mkuu, Jaji Feleshi, ni baada ya moja ya makala hizo ku challenge uwezo wa Mahakama zetu kutoa uamuzi wa haki. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
Mtamsikia wenyewe AG, Jaji Feleshi akijibu, ila hii hali ya Mahakama zetu kutotenda haki kwa kitu kinachoitwa legal technicalities, kinaendelea! na mfano mzuri wa haki kutotendeka kwa legal technicalities ni hii hukumu ya kina Halima Mdee na wenzake 18!
Paskali.
Mkuu Nguruvi3 , naunga mkono hoja kwamba mwamko wa Watanzania kutafuta haki ni tatizo, na kwa utafiti wangu, tatizo kubwa sio Watanzania hawajui kutafuta haki, bali Watanzania hawazijui haki zao!. Hawazijui haki zao kwasababu hawaijui katiba yao, na hawazijui sheria zao!. Hivyo kitu cha kwanza cha kuwasaidia Watanzania ni kuwaelimisha, elimu ya Katiba, Sheria, na haki, ili sasa ndipo wahamasishwe na wapate mwamko wa kuzidai haki zao.Ni kweli pia kwamba mwamko wa Watanzania kutafuta haki ni tatizo,
Tuna utawala wa kipuuzi haswaIssue ya Lissu, wameshindwa kwasababu wahusika sio watu wasiojulikana bali ni watu 'wasiojulikana' Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana na pia nikashauri wale wenye uwezo wajitolee kusaidia WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?
P
Mkuu Matrix.Host wa kipindi mwanaccm
Invitees CCM tawi kuu na CCM B
Broadcasting media - CCM afaffiliated.l
Jina la kipindi kwa maslahi ya taifa.
Taifa lipi hilo lisilo na diversity?
Wakili who is fooling whowhomk
Pascal something is not right here.Mkuu Matrix.
View: https://youtu.be/VZlHxInJWfI?si=jpu7EpmZDAj6CBffComposition
CCM ni mmoja tuu Rais Samia !.
- Rais Samia- CCM
- Prof. Lipumba -CUF
- Askofu Mwamakula - Dini
- Wallece Mayunga- ADC
- Ali Omar Juma - Chauma
- Juma Duni - ACT Wazalendo
- Abdul Nondo- ACT Wazalendo
Kesho angalia kipindi,
Manguli wa Siasa, Zitto Kabwe, Stephen Wasira, John Cheyo, Kuunguruma Kwenye Kipindi cha KMT cha Channel Ten, Kila Jumapili Saa 3:00 Usiku, Usikose!
Lineup ni hii
CCM ni mmoja tuu Mzee Stephen Wasira!.
- Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mzee John Memosa Cheyo, " Mzee wa Mapesa",
- Mwanasiasa Mkongwe wa CCM toka enzi za Nyerere, Mzee Stephen Wasira,
- Mwanasiasa Kijana Machachari, na Kiongozi Mkuu, wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe
- Dorothy Semu wa ACT Wazalendo,
- Mrajis Azasi Zanzibar, Ahmed Khalid Abdullah,
- Profesa wa Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Bernadeta Killian
- Pascal Mayalla
P
Mayalla jitambilishe kuwa wewe pia ni kada wa CCM!! I have every reason to believe that you are a ccm surrogate.Wewe umeishajitambulisha kama chawa hivyo wenye uelewa hatuwezi kuangalia ulaghai wako kupitia channel ya CCM
Maridhiano yalimalizika wakafikia makubaliano ya kitu kinachoitwa kugawana nusu mkate, lakini kabla makubaliano hayo hajasainiwa, Lissu akatua nchini, akatibua makubaliano hayo Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?Pascal something is not right here.
Je yale maridhiano aliyosema Samia ilikua kiini macho?
Sioni watu kama Lissu hapo au Mnyika kulikoni?
Mkuu Bulesi , japo kizungu nakimanya, ila hizi ni lugha za watu hivyo maneno mengine siyamanyi. Sentence hii "I have every reason to believe that you are a ccm surrogate" inamaanisha nini?.Mayalla jitambilishe kuwa wewe pia ni kada wa CCM!! I have every reason to believe that you are a ccm surrogate.
Njaa itakufikisha kubaya uzeeni mwako!
Kama unakimanya kiingereza usichoelewa hapo nini? Kuwa wewe ni kiumbe wa CCM sio tofauti na Mwashambwa ingawa unavunga na uwakili wako!! Ni mnafiki.Mkuu Bulesi , japo kizungu nakimanya, ila hizi ni lugha za watu hivyo maneno mengine siyamanyi. Sentence hii "I have every reason to believe that you are a ccm surrogate" inamaanisha nini?.
p
Mtu kuwa CCM sio ndio kiumbe wa CCM!. Binadamu wote ni viumbe wa Mungu, hakuna kiumbe wa chama chochote!.Kuwa wewe ni kiumbe wa CCM
Wana CCM tuko wa aina nyingi, kuna washabiki, wafuasi, wanachama, makada, wakereketwa, wafurukutwa na siku hizi kuna machawa!, mimi ni CCM wa Nyerere type CCM sio baba yangu, sio mama yangu!.sio tofauti na Mwashambwa ingawa unavunga na uwakili wako!!.
Hujanijibu swali langu nimeuliza kwanini wewe kama host wa kipindi cha kwa maslahi ya taifa kwanini hujawaita mtu kama Lissu na Mnyika?Maridhiano yalimalizika wakafikia makubaliano ya kitu kinachoitwa kugawana nusu mkate, lakini kabla makubaliano hayo hajasainiwa, Lissu akatua nchini, akatibua makubaliano hayo Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Hivyo Chadema, wakasusa tena!.
Kikao kingine kimeitishwa tarehe 3 na tarehe 4 January Mlimani City, kwenye promo za Mkutano huo, wamewasheheneza Chadema kwa picha za Mbowe, Lissu, Mnyika na Halima Mdee, hivyo nimewaomba Chadema wasisuse Baada ya maridhiano kuna haja kuendele kususa na kuzira? Njooni mezani, tukae pamoja, tuwe wamoja, twende pamoja!
P