Kipindi cha uchaguzi, vyama vyenye wagombea tu ndivyo viruhusiwe kufanya mikutano ya kisiasa, ambavyo havishiriki visubiri baada ya October.

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
20,711
Reaction score
31,331
Ni vyama vile ambavyo vitashiriki uchaguzi mkuu na kuwasilisha wagombea na ratiba za kampeni ndivyo viruhusiwe kufanya mikutano ya kisiasa. Hii itaondoa mvurugano na vurugu zisizo na msingi, na pia kuimarisha ulinzi na usalama

Wahuni wengine wasubiri kwanza watu wanaotumia haki yao ya kikatiba waitumie kikamilifu
 
😂😂 hoi spina ya Lissu imekuwa hatari.... Hivyo vyama mnavyotaka kuingia navyo kwenye uchaguzi ni vipi?. Yaani chama unachotaka kushindana nacho huwa kinapata kura moja Nchi mzima ndio kishindane na ccm kinachoiba kura?.
 
Kulingana na kifungu kipi cha katiba ya nchi??
Kila chama kinapeleka orodha ya wagombea wake na ratiba zao za uchaguzi kwa Tume ya uchguzi, na Tume inapeleka ratiba hizo Polisi
 
Kwa katiba ya nchi hii mikutano ya kisiasa inaweza kufanyika wakati wowote. Hakuna kifungu cha katiba au sheria za nchi kinachovitaka vyama vya siasa kupeleka ratiba zao za uchaguzi kwa tume au polisi. Hizo ni taratibu zilizoanzishwa na CCM tu.
 
Ndio utajua hujui sasa, viwanja vyote vya kufanyia kampeni vitakuwa booked, ni high season kisiasa
 
Ni vyama vile ambavyo vitashiriki uchaguzi mkuu na kuwasilisha wagombea na ratiba za kampeni ndivyo viruhusiwe kufanya mikutano ya kisiasa. Hii itaondoa mvurugano na vurugu zisizo na msingi, na pia kuimarisha ulinzi na usalama

Wahuni wengine wasubiri kwanza watu wanaotumia haki yao ya kikatiba waitumie kikamilifu
kuongezea na wananchi wale watakaowasilisha nia ya kupiga kura ndio wahudhurie mikutano ya kampeni, wengine tuonane baada ya uchaguzi
 
Bado Mapandikizi hayajaleta matokeo mliyotarajia nini?🤣🤣🤣

Si mlisema CHADEMA inakufa???? Kiko wapi??😅😅😅😅

Kweli CCM hali tete sana kwenu mwaka huu😅

Tulieni tu! Mwaka huu ni mwaka wa Mungu kuikomboa Tanzania.
 
kuongezea na wananchi wale watakaowasilisha nia ya kupiga kura ndio wahudhurie mikutano ya kampeni, wengine tuonane baada ya uchaguzi
Kwamba mikutano ya kisiasa ihudhuriwe na raia wenye vitambulisho vya kupiga kura tu?
 
hii itaondoa ule uhuni wa watu kusombwa na magari ili kuhudhuria mikutano ya kampeni
 
Ni vyama vile ambavyo vitashiriki uchaguzi mkuu na kuwasilisha wagombea na ratiba za kampeni ndivyo viruhusiwe kufanya mikutano ya kisiasa. Hii itaondoa mvurugano na vurugu zisizo na msingi, na pia kuimarisha ulinzi na usalama

Wahuni wengine wasubiri kwanza watu wanaotumia haki yao ya kikatiba waitumie kikamilifu
Hayo ni mwazo yako au ni kanuni za uchaguzi, kama ni mawazo yako, nchi haiendeshwi kwa takataka kama hizi
 
Back
Top Bottom