secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 2,998
- 4,948
Search line,Show Time, J3,J5 na Ijumaa na Sindano tano za moto na Fred Waah kila Jumamosi asubuhi!
Jumapili tukitoka kanisani tunawahi kusikiliza Sitasahau!
Pia ilikuwepo Search Line!
SintosahauKilichokuwa kikileta story za Gamboshi
Weekend FeverWakuu nimekaa nikakumbuka miaka hiyo kipindi cha SITOSAHAU cha RFA. Ilikuwa ikifika hiyo mida ni kukaa karibu na redio mfano wakati wa simulizi ya Gamboshi [emoji23] asee?
Wahenga kipindi kipi mnakumbuka? Au ulikuwa ukikipenda?
Hakika mkuu.Maregesi ni wa siku hizi, Deokaji na akiona Jackson pajo nyamsuka, Deokaji makomba pamoja na yusuf magasha ni wa kitambo kidog
Hicho kipindi kilikuja kuharibiwa na watangazaji fulani vichwa maji ambao hata Kiswahili hawakijui vizuri utafikiri wametokea shimoniWeekend Fever
Matukio (asubuhi)1.mambo mambo
2.show time
3.search line
4.sinto sahau
Kitambo sanaaaMatukio (asubuhi)
Darubini ya Leo (zamani kilikuwa linaanza Kila siku saa 1:30 usiku hadi saa 2:00 ambapo kipindi cha michezo kinaaza, baadaye walibadisha)
Ile jingle ya Deokaji Makomba kwenye kipindi cha michezo Kila jumapili asubuhi "ni katika michezo na burudani"1. Je, huu ni uungwana la hasha huu si uungwana na Fredwaaaa.
2. Usiku wa mahaba na Erick Maganga na ile sauti yake iliyotulia usiku wacha kabisa
3. Sitasahau
Hiki kipindi kilinifanya nigombane sana na maza kuhusu mambo ya kanisani, zile story za zablon na yule jamaa wa south zilikuwa hotHiki cha "sitasahau" watu walikua wanasimama barabarani kusikiliza kama njia moja ya kupumzika maana boda ya zamani ni miguu
Oya mzee zama zikienda hazirudiKitambo sanaaa
True..Oya mzee zama zikienda hazirudi
RFA ilikuwa vizuri Kila angle kuanzia habari, burudani na michezo, kuwasaidia wenye shida (kipindi cha ushauri wako).True..
Mungu akupe nini kwankunikumbusha majina kama Rahabu fredi, Muhuza na Zuberi msabaha(alipenda kujiita Zubegh).Wazee wa hip hop Mtakumbuka kipindi cha Weekend fever kikiongozwa na Uncle Sam....jamaa alivumbua vipaji vingi vya hip hop hakuna kipindi cha redio cha hip hop kama kile.
Halafu kuna RFA bonanza alikuwa anatangaza huyu jamaa Sky walker wa simulizi na sauti alikuwa anauwa sana.
Vodacom Burudani zaidi
Ndani yake kulikuwa na session ya sindano 5 za moto chini ya Marehem Freduwah.
Sitosahau- hichi kipindi kiliwateka watu wengi sana,mimi ile stori ya jamaa wa Gamboshi pamoja na Rojaz aliyezamia SA lakini hakutoboa akarudi bongo na kufungua Saluni.
Duniani wiki hii-kipindi kilichokuwa kina kusanya matukio yaliyotokea duniani kwa wiki Nzima~ Mtangazaji alikuwa kama Rahab Fred kama sijakosea.
Bolingo time chini ya Marehem u Zuberi Msabaha.
Show time ya kina kidbway Glory Robinson Mtoto wa Mama Sabuni.
Kipindi cha michezo na kina steve Moyo mchonge na Baruani Muhuza.
Nadhani hii ndio redio bora ya miaka ya 2010 kurudi nyuma ilikuwa imesheheni vipaji vya waandishi na watangazaji hodari sana...
Sijui walifeli wapi?
Nafasi yake ikachukuliwa na mawingu FM, pamoja na EA Radio ambayo ilikuwa na watu wenye vipajo vya kufa na kuona kama George Bantu, Rwenyagira, George David AKA Kampista, Mkuwe Isale mwite mamy baby nk.Nadhani hii ndio redio bora ya miaka ya 2010 kurudi nyuma ilikuwa imesheheni vipaji vya waandishi na watangazaji hodari sana...
Sijui walifeli wapi?
Weekend flevaWakuu nimekaa nikakumbuka miaka hiyo kipindi cha SITOSAHAU cha RFA. Ilikuwa ikifika hiyo mida ni kukaa karibu na redio mfano wakati wa simulizi ya Gamboshi 😂 asee?
Wahenga kipindi kipi mnakumbuka? Au ulikuwa ukikipenda?
Ndio ndio mkuu ni tano za moto na zilikua moto si kitotoNi vodacom Burudani zaidi ndani yake ndio kulikuwa na session ya Sindano 5 za moto.
Bonge la Pindi na mwamba mtangazaji Fred Fedilis (Fredwaa)-RIP.... Alikuwa ananikosha sana huyu mwamba...Je huu ni uungwana? La hasha huu si uugwana.