Kipindi unafurahia kulipwa mshahara mkubwa wakuanzia mil 3-5, basi tambua kuna watu nchi hii wanalipwa mpaka mil 13-27 private sector

Umeongea point mtu kazi, more money more problems

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
It’s called money management.

The core principles of personal finances are: income, savings, spending, and investment.

Ukiishi ndani ya uwezo wako kulingana na kipato chako, halafu ukawa na nidhamu ya kujiwekea akiba hata kama ni kidogo kidogo, huku pia ukiwa na nidhamu katika matumizi yako, utajiweka katika nafasi nzuri [sana] kiuchumi.

Kuna mtu namjua anafanya kazi kwenye hizi payday loans places.

Huwa ananiambia kuwa baadhi ya watu ambao huenda kuchukua hizo payday loans, huwezi kuamini kazi zao!

Kuna mawakili, wahasibu, manesi, n.k., watu ambao kazi zao kwa wastani, ni za vipato vya juu.

Cha msingi zaidi, ni jinsi unavyozi manage hela zako kuliko kiasi ambacho unakipata.
 
Hao wa kipato cha juu wengi wanakuwa wamejiaminisha kuwa wao wana uwezo wa kutengeneza pesa, hivyo na matumizi yao yanakuwa ya juu. Mpaka wanaanza kutumia pesa ambazo hawajazipata bado (mikopo, heavy credit card debt, etc.)

Na hapo ndipo panapokuwa na mtego.
 
Hahahha Kuna watu wako Tanzania Cigarettes Company (TCC) hapo hatari tupu.
Tumbaku ina siri gani? Ofkoz jamaa hata viwanda vyao viko vizuri kwa kuangalia tu. Ni kwamba tumbaku kuna mzigo sana au ile tu expert huyo ndio mana mzigo mnene? Kuna kampuni moja kubwa ya mitandao ya simu niliona board of directors wanavokula madolali ya kutosha sio poaa
 
Kwahiyo akikumbuka asifurahie? Watu maskini bwana, hapo unaumia kweli kweli mtu kulipwa milioni tano
Kama ulikuwepo. Pengine alikuwa anadhani milioni 3 anayopata yuko kwenye class ya juu, kuja kuona wenye hizo milioni 20+, akajisikia mnyonge ghafla. Anachotakiwa kujua ni kuwa hata hiyo mil 20 anayodhani ni kubwa, siyo kitu kabisa, na kuna wanaopata nyingi zaidi. Bado huja-count wafanyabiashara wanaoingiza zaidi.
 
Hii issue ya payments ipo sawa kabisa, kuna mahali nilikuwa nalipwa kiasi ila niliweza kujikimu na kuendesha vizuri maisha yangu, baadae ulikuja kuongezeka kidogo kama mara mbili yake, lakini bado tofauti sikuiona japo mwanzo ilikuwa vizuri sababu nilizoea kusave asilimia 30 mpaka 45% ya ninachopata ulipoongezeka niliona kibubu kimejaa ghafla

Lakini baada ya miezi kadhaa nikajikuta nipo vile vile, matumizi yamedouble na hata ule mpya bado inabidi mishe zingine nisikilizie mwezi mpaka mwezi

So ni kweli kabisa,
 
Kitanzania, milioni bado yupo class ya juu kama unazungumzia mshahara na kipato halali.

Wenye kupata hizo 20m halali, pengine hawazidi 0.001% ya watanzania wote wenye vipato halali.

Ukirudi kwenye ulingo wa SURVIVAL OF THE FITTEST sasa, nusu ya wakazi wote wa Dar es salaam wanaendesha Range na Discovery, BMW, Maybach, G-Wagon, RR, LC, GXR, Harrier, Ford, Prado, Forester...

Hakuna la chini ya hiyo 25m
 
Ukishalipwa pesa ya madafu tu utemi wako unaishia Vingunguti.

Kuna siku nilikuja likizo Bongo, nikabadili dola nyingi sana kwa matumizi yangu, mpaka likizo ilipoisha nikawa sijamaliza zile shilingi za Tanzania kutumia. Nikajisahau nikapanda nazo ndege kurudi New York City.

Nikasema ngoja nitafute Bureau de Change ya New York City inayoweza kununua hizi hela za Tanzania na kunipa USD.

Nilizunguka sana watu wanaziangalia pesa za bongo kama makaratasi tu, hawazitambui.

Na uhaba huu wa US dollar unaweza kuwa TZS ukakosa USD. Yani hela ubabe wake unaishia kwenye mipaka ya nchi sanasana utatesa nchi jirani. Ukiingia viwanja vya kimataifa proper hela ya kibongo inakuwa kama stamp tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…