It’s called money management.
The core principles of personal finances are: income, savings, spending, and investment.
Ukiishi ndani ya uwezo wako kulingana na kipato chako, halafu ukawa na nidhamu ya kujiwekea akiba hata kama ni kidogo kidogo, huku pia ukiwa na nidhamu katika matumizi yako, utajiweka katika nafasi nzuri [sana] kiuchumi.
Kuna mtu namjua anafanya kazi kwenye hizi payday loans places.
Huwa ananiambia kuwa baadhi ya watu ambao huenda kuchukua hizo payday loans, huwezi kuamini kazi zao!
Kuna mawakili, wahasibu, manesi, n.k., watu ambao kazi zao kwa wastani, ni za vipato vya juu.
Cha msingi zaidi, ni jinsi unavyozi manage hela zako kuliko kiasi ambacho unakipata.